Kama JWTZ halitowaomba Radhi Raia wasio na Hatia WALIOTESWA KINYAMA na MP wa Lugalo Juzi, nawashauri walishtaki Jeshi

Kama JWTZ halitowaomba Radhi Raia wasio na Hatia WALIOTESWA KINYAMA na MP wa Lugalo Juzi, nawashauri walishtaki Jeshi

Kibano kitaendelea hadi jasho liwatoke hakuna atakayewatetea awe wa ndani au nje ili siku nyingine mjifunze.Hata watoto au familia zao hamuwezi kuwafanya lolote.Jifunzeni kuheshimu majeshi yetu, mnanyonyana korodani sababu ya wao kujitoa mhanga usiku na mchana laiti mngejua mazingira wanayofanyia kazi na hawana pahala pa kulalamikia.Next time mjifunze na kuwa na adabu, hiyo ni trailer msiombe picha ianze
Mmetumwa kujiunga na jeshi? Ninyi ndio kanituma baba. Jeshi ni kujitolea na nidhamu unapaswa kujizuia mambo ya hovyo ipo siku mtapata shida na hakuna mwananchi atakaye wasaidia. Kama hadi sasa unataka ulipwe fadhila kwa kuwa jeshi gumu wewe bado hujawa mjeshi kamili. Mjeshi halalamiki, hajisifii na wala hana makuu lakini ninyi wengi wenu mpo hivyo. Wachache ndio wanajitambua. Inasikitisha sana kuona haya
 
Kibano kitaendelea hadi jasho liwatoke hakuna atakayewatetea awe wa ndani au nje ili siku nyingine mjifunze.Hata watoto au familia zao hamuwezi kuwafanya lolote.Jifunzeni kuheshimu majeshi yetu, mnanyonyana korodani sababu ya wao kujitoa mhanga usiku na mchana laiti mngejua mazingira wanayofanyia kazi na hawana pahala pa kulalamikia.Next time mjifunze na kuwa na adabu, hiyo ni trailer msiombe picha ianze
Kwani wamelazimishwa kwenda huko??
Matokeo nadhanin umeona kwa kanal.
 
Binafsi sijafurahishwa na vitendo vinavyofanywa na wanajeshi hasa kwa raia.

Jeshi la polisi liliwekwa kwa ajili ya kuingiliana na raia na wao ndio wanaohusika na raia direct.
Kitendo cha jwtz kwenda kuingilia uhuru wa raia ni uvunjifu wa sheria hasa kukiuka haki za binadamu.

Jwtz(MPs) msijikute nyinyi ni waungu watu na huo upolisi wenu ni wa huko makambini kwenu na sio uraiani.

Hakuna vita mbaya sana kati ya raia na wanajeshi.

Na siku ikitokea kwa hapa Tanzania basi naamini wanajeshi watakufa wengi sana.

Mnaleta ukontawa kwa raia wakati mkiwa makambini mnakuwa wasafisha vyoo na vijakazi wa jeshini.

Acheni ufala.

Ubabe sio dili.
Mafala sana hawa
 
Alafu ndio wanajiita eti "jeshi la sita duniani" vichekesho kabisa hivi, hao watu wakipeleka kesi mahakamani japo wameonewa lakini kuna uwezekano mkubwa wakashindwa kesi, hiyo ni ile inaitwa "kesi ya nyani hakimu ngedere" cha msingi niku waroga tuu kwa sababu uchawi hauna ushahidi
 
Chukua like mkuu. Nina jamaa yangu wa damu sana wakati ameajiriwa kwa mara ya kwanza akataka kuleta huu ushamba. Tulikua kwenye daladala wote konda akapishana nae kauli kidogo akataka kuleta noma nikamzuia tulivyoshuka nikamchana awe humble atapigana na wangapi.

Now mstaarabu vibaya ile siku alichukia lakini jioni alinipigia simu akaniambia kweli alizingua.
Ni mambo ya kishamba sana ,kutumia nguvu kwenye kila kitu !!
 
Tatizo wabongo tumefubaa, kuprotest hatuwezi ndio maana tunaonewa.

Hii tabia ya kuwalea wanajeshi hadi wameizoea ndio inatugharimu.

Mara ngapi tunasikia hawa wanajeshi wanajichukulia sheria mkononi huku tukiwachekelea.

Tuamue kwanza kuprotest huu tabia yao, then ndio wataweza kufuata sheria.
 
GENTAMYCINE sijapendezwa na Kitendo cha Raia Kato kujichukulia Sheria mkononi na Kumchoma Kisu Afande Lt. Col. Muna na ninalikemea sana.

Ila GENTAMYCINE sijapendezwa na Foolish Approach ya Wanajeshi ( hasa MP wa Lugalo ) ya kuamua Kuvamia hovyo Nyumba za Watu, Kuvunja Milango yao, Kupiga hovyo Watu na hasa hasa Kuwajeruhi vibaya sana Wamama ( tena Watu wazima ) ambao wengi Wao hadi Usiku huu GENTAMYCINE naandika huu Uzi Wanauguza Majeraha yao huku Mmoja wapo alikamatwa na MP hao akiwa Dukani Kwake na kuamrishwa Kuingia Garini huku akiliacha Duka likiwa wazi ambapo Wahuni waliingia na Kuiba Pesa zote za Hesabu na Simu zilizokuweko ndani.

Nijuavyo GENTAMYCINE ni kwamba JWTZ wana Kitengo chao cha Mawasiliano, Mahusiano na Elimu kwa Umma ( Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ) hivyo Kiungwana tu wangejitokeza na Kukiri Mateso haya kufanyika kwa Raia wasio na Hatia na kuomba Radhi ila wamechagua Kunyamaza na pengine hata Kufurahia kilichofanyika

Kuna Taarifa ambazo si nzuri nimezipata Jioni hii ( japo naendelea Kuzithibitisha ) kuwa kuna Wanawake Wawili waliokamatwa Baa ya Igole au ya Bombardier nao Kujumuishwa katika Kundi la Watu 74 Waliokamatwa na kupelekwa Kambini Mwenge kupewa Adhabu Kali za Kijeshi zilizojumuisha Kuchapwa na Virungu na Fimbo Ngumu Migongoni, wakirukishwa Vichurachura, wakibebeshwa Mawe na Kubiringitwa Udongoni Wamekufa ( Wamefariki ) leo.

Na kwa leo Mchana, Alasiri na hata Jioni hii GENTAMYCINE nimeshuhudia Raia kadhaa ( tena Wababa na Wamama ) Watu wazima bila kuwasahau Mabinti wakiwa Wamevimba Miguu, Macho, Ugoko na Pua zao na Wakilalamika sana na Kuhoji Kosa lao hasa hadi Kuteswa na Kupigwa kote kule Juzi Usiku kulikuwa ni nini?

GENTAMYCINE niliamua kwenda mbali zaidi kufanya Mahojiano na baadhi ya Wanasheria ( Mawakili ) juu ya Kilichofanyika na kudai kuwa kilikuwa ni Kinyume na Utaratibu wa Sheria za nchi na kwamba Wahusika wakiungana na kwenda Kushtaki hali itakuwa mbaya Kwao ( JWTZ ) hata kama wale MP wa Lugalo WALIOWATESA KINYAMA RAIA kwa kujua kuwa walichokuwa wanakifanya kilikuwa ni kibaya walivalia Kininja ili kuficha Nyuso zao Wasijulikane.

JWTZ nawapenda ila hapa mmebugi.

Jeshi la tz linafanyaga mambo ya aibu sana jeshi lina act utafikiri kikundi fulani cha panya road au waimba singeli amapiano
Hivi hili jeshi halina shuguli za kufanya au ?kwa hiyo kitendo walichofanya kawe kwao wanaiona operation kubwa huko jeshini siyo.
Vyanzo vyao vingi vinavyoleta mgogoro na raia huwa ni vya kipuuz
Utakuta mara wanagombania madem,au ndiyo ile kupishana kauli na raia kwa mambo ya kijinga tu

Ova
 
Subiri siku akipigwa Baba au Mama ako,njoo na hizi kauli zako za kipumbavu, Jadili hili jambo kama binaadamu mpenda haki,siyo kila muda ni wa kukejeliana tu humu!!
 
Kibano kitaendelea hadi jasho liwatoke hakuna atakayewatetea awe wa ndani au nje ili siku nyingine mjifunze.Hata watoto au familia zao hamuwezi kuwafanya lolote.Jifunzeni kuheshimu majeshi yetu, mnanyonyana korodani sababu ya wao kujitoa mhanga usiku na mchana laiti mngejua mazingira wanayofanyia kazi na hawana pahala pa kulalamikia.Next time mjifunze na kuwa na adabu, hiyo ni trailer msiombe picha ianze
Mtaendelea tu kuuwawa 🤣🤣 huyu ni mjeda wa tatu ! mwingine alifia kilabuni huko Tanga ! kalewa kaanza kujishaua muhuni kakimbilia Panga akamuua !! sifurahii mauaji ila nasikitika kwanini hamjui nafasi yenu kwenye jamii ? We hujui kwamba ni Mwanajeshi ?

kama huyu mwingine aliyekufa nasikia pia alikua na mke na watoto eneo la tukio bado tu halijiamini anataka kujionesha ni mjeda !! hivi kweli mtu una akili na unajitambua unapigana mbele ya mke na watoto 🤣 unataka kuonesha nini ? Pang'ang'a

Ukifika maeneo ambayo yana changanyikeni , shiriki kama wao ongea kama wao ! Hata wakikuita poti au afande isiwe ya hofu iwe ya kukubali kazi unayoifanya ya kulinda mipaka ya nchi.
 
Kibano kitaendelea hadi jasho liwatoke hakuna atakayewatetea awe wa ndani au nje ili siku nyingine mjifunze.Hata watoto au familia zao hamuwezi kuwafanya lolote.Jifunzeni kuheshimu majeshi yetu, mnanyonyana korodani sababu ya wao kujitoa mhanga usiku na mchana laiti mngejua mazingira wanayofanyia kazi na hawana pahala pa kulalamikia.Next time mjifunze na kuwa na adabu, hiyo ni trailer msiombe picha ianze
Tanzania kuna wajinga wengi, duh! Ngoja tusiseme
 
Tatizo wabongo tumefubaa, kuprotest hatuwezi ndio maana tunaonewa.

Hii tabia ya kuwalea wanajeshi hadi wameizoea ndio inatugharimu.

Mara ngapi tunasikia hawa wanajeshi wanajichukulia sheria mkononi huku tukiwachekelea.

Tuamue kwanza kuprotest huu tabia yao, then ndio wataweza kufuata sheria.
Walaaahi wajichanganye waje waguse mtu wa familia yangu.
Hata kama hiyo siku watanitoa roho ila na mimi nitaondoka na baadhi yao.
Huu ni upumbavu kuvumilia unyanyasaji wa aina hii
 
Sio kwamba hawaoni

Sio kwamba hawajui kwamba wamefanya makosa

Sio kwamba wahusika hawajaguswa na hili

Sio kwamba hawawezi kusema

La

Ila kwakuwa washajiona wao miungu watu basi watapotezea

Ukitaka walisemee itokee hivi

Jamii Forums wachapishe taarifa hii katika mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram na twitter juu ya unyanyasaji wao

Trust me lazima watasema Tu

Vinginevyo tuendelee kupaza sauti pengine Mungu atawaadhibu kama anavyo muadhibu kanali huko sakafuni

Tanzania kuna uoga ila Amani tunadanganywa

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
Tunawasubiri mtaani wakistaafu
 
Back
Top Bottom