Kama Kashfa Escrow ni "Richmond", Then, Lowassa Alionewa?, Kama Ni "EPA!" Then, Wahusika Wasionewe!

Kama Kashfa Escrow ni "Richmond", Then, Lowassa Alionewa?, Kama Ni "EPA!" Then, Wahusika Wasionewe!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Azimio la Bunge kuhusu Escrow, limetolewa leo, na mjadala wa Escrow, umefungwa rasmi, wakati mjadala huu unaanza, nilisema humu, Hata ikithibitika Fedha za Escrow ni za Wizi, Nawahakikishia Hakuna Atakayewajibika!. Jee leo baada ya mjadala kumalizika, vipi kuna yeyote aliyewajibika?!.

Kwa vile Bunge hili limeishawahi kushughulikia kashfa mbili, ile ya Richmond, na ile ya EPA,

Kama kashfa ya Escrow ni kama Richmond, then je Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa alionewa?!.

Kama wizi huu ni sawa na ule wizi wa EPA, then, Watuhumiwa wa Escrow wasionewe!, kama watu walikwapua mabilioni yale ya EPA na wakasamehewa kwa kutakiwa kurudisha tuu, kwa nini na watuhumiwa wa Escrow wasitakiwa kurudisha tuu yaishe?!.

Kwa nini Bunge na Serikali yetu ifanye maamuzi tofauti kwa like scenario?!.

What a double Standard?!.

Ila pia kwa vile issue ya fedha ni za umma au laa, bado haijapata majibu ya kina, matokeo ya kila kitu, yatategemea matokeo ya kumalizwa kwa utata huu!, na kwa vile hapo kati, Mhimili wa Mahakama ulidhauriwa, baada ya kwisha kwa kikao cha bunge, sasa mahakama itaendelea, hivyo lolote linaweza kutokea!.

Kwa vile bungeni walisigana na mwisho wa siku wakaondoa tofauti zao, na sisi humu jf, kuna watu tulisigana, sasa tumalize tofauti zetu, tusonge mbele!.

Paskali


Soma
 
Soma mapendekezo mapya ya PAC then rudi
 
Pasko, mie naona kuwa UWAJIBIKAJI wa Viongozi waliovurunda unaegemea kwa " Ni kwa kiasi gani VIAZI VIKUBWA Selikarini vimehusika kwenye kashfa husika". Pia yategea KONEKSHN ya hivyo viazi kwenye kashfa tajwa. Hii ya Tegeta eskrouw, labda konekshn ilikuwa mbali na viazi hivyo vilipanga "watu wao" miongoni mwa wabunge kuwakingia kifua.
Makinda kawapiga dongo wabunge "wapendao" kuwekwa mifukoni na wenye hoja na ajenda zao. Amesema: Kataeni watu wanaowalobi. Hili ni kosa la jinai. Halina kinga. Mtawekwa ndani. Mtapoteza ubunge.
Ni kwa kiasi gani hili litamatirioraiz, tusubiri.
 
Hapa LA ana kila haki ya kufanya comparisons na justification kuwa JK alimtosa makusudi kwasababu hakuonekana amechota fedha because Escrow account saga inafanana 100% na ya Richmond ,sasa swali kwanini hakubebwa kama alivyobebwa Mzee wa "BANGO KITITA" Leo?
 
Here we go again!!!!Pasco sisi wanyatiaji wa mambo nyeti tumetulia,so far Ukawa 3 CCM 0,,,,tunavuta pumzi for another level.nakushauri tulia uone sinema mpya inayokuja
 
Lowassa alikua hatakiwi tangu mwanzo,jk alikua hana nia ya kumpa uwaziri mkuu bali ilikua shinikizo la rostam ndio maana jk alimbandua harakaharaka alipo pata mwanya.
 
Lowasa ni mwanasiasa anaweza kuwa alikuwa na hesabu zake na alichanga karata alivyozichanga ngoja tutaona huko mbele
 
madudu kama haya hayataisha CCM na wataendelea kuihujumu nchi kwa ajili ya kumpiga nyoka mkiani wakiacha kichwa.
hata watakaowajibishwa bado wana mizizi mle ndani,waizi wote hasa hawa wajuu hawajawahi kukaa sero hata siku mbili tu,angalia tu Daniel Yona wa lini na mpaka sasa hata kwenye ili list ya escrow yupo,kuwajibishwa imekuwa kujiuzulu,kama huna cheo utakula good time,Lowasa alitakiwa ashitakiwe kabisa amejiuzulu bado mtaani good time ana make it rain.

Mkuu wa nchi awamu ya washikaji zake wamepiga sana.
Rostam alipiga ameondoka
lowasa kapiga ameondoka
Ngeleja kapiga kaondoka
Chenge kapiga sana tu bado yupo anapiga
Jairo kapiga kaondoka
Zakia meji kapiga kaondoka
Masha kapiga
Muhongo wa juzi kapiga anaondoka
Tibaijuka kapiga anaondoka
werema naye kapiga

Wote hao wamepiga mamilion/billions,hata wakiondoka bado kuna mizizi.

Haya tuwasubiri wapya wanakuja kupiga tena.
zamu hii washikaji wote mtapiga sana huu mda wenu pigeni
 
Swala la mtu binafsi kuwajibika linatokana na moyo wake yeye mwenyewe lakini uzuri pamoja na wao kukataa kuwajibika wamelazimishwa na maazimio yamepita hakuna mjadala hata kama hawataki!
 
Lowasa anajua nini maana ya kuwajibika. Hakutaka mijadala ya usiku kucha, aliwaachia wengine waendelee alipokomea. Ila Mzee wa Kimya kimya ameamua kutokuwajibika. Hii inadhihirisha jinsi gani asivyokuwa muwajibikaji. kwangu Pinda sio kiongozi thabiti kwani yuko radhi hali iwe mbaya kwa wananchi wake huku yeye akilinda nafasi yake. Siwezi kumpa ridhaa yangu kiongozi asiyewajibika iwe katika ya furaha au ya machungu.
 
Pasco I can bet. ...muhongo na timu yake hawachomoki....watawajibishwa na Prof.

mapendekezo yaliyotolewa na PAC hayana muhemko kama yale ya Mwakyembe na yanatekelezeka kwa kiwango kikubwa.
 
Hivi serikali ikrudi ikasema yafuatayo itakuaje:

1. Baada ya uchunguzii wa kina imegundulika kuwa sehemu kubwa ya pesa ya ESCRO haikuwa ya UMMA , sehemu iliyokuwa ya UMMA ambayo ni kodi Billion 21 imekusanywa.(Kumbuka Pinda kasema it is not yet clear kama ni za umma)

2.Uchunguzi wa kina wa taasisi za fedha umegundua kwa fedha zote zilizohamishwa zilifuatataratibuzote kibenki na kuwa hakukuwa na cash withdrawal ya 73bio.Hivyo hatuwezi kuitangaza benki ya staic kuwa moneylaundering concern


3.Baada ya uchunguzi wa kina serikali imeshindwa kupata ushahidi wa moja kwa moja kuwahusisha waziri wa nishati na katibu mkuu wake.Hivyo kwa mujibu wa sharia za nchi na haki za utumishi wa umma uteuzi wao hautatenguliwa.

4.Baada ya uchunguzi wa kina imegundulika kuwa baadhi yataarifa katika azimio la bunge hazikuwasahihi.Ila tunaipongeza kamatikwa kazi nzuri.

5. Kulingana na sharia ya uwekezaji serikali imebanwa kisheria kutaifisha mitambo ya IPTL.Na ili uzuia kuiingiza serikali katka mgogoro na wawekezaji mitambo hiyo haitataifishwa

Kumbuka azimio la bunge is just that Azimio...it is not binding to the government

Tutafakari
K
 
Lowasa anajua nini maana ya kuwajibika. Hakutaka mijadala ya usiku kucha, aliwaachia wengine waendelee alipokomea. Ila Mzee wa Kimya kimya ameamua kutokuwajibika. Hii inadhihirisha jinsi gani asivyokuwa muwajibikaji. kwangu Pinda sio kiongozi thabiti kwani yuko radhi hali iwe mbaya kwa wananchi wake huku yeye akilinda nafasi yake. Siwezi kumpa ridhaa yangu kiongozi asiyewajibika iwe katika ya furaha au ya machungu.

Fisadi tu yule
 

Lowasa aliponzwa na papara zake na washauri wake tu laiti kama angekomaa pengine mpaka leo angekuwa PM.

Halafu hata sielewi kwa nini yeye hakuwa supported na wanaCCM kama huyu Mzee wa Maembe?
 

Lowasa aliponzwa na papara zake na washauri wake tu laiti kama angekomaa pengine mpaka leo angekuwa PM.

Halafu hata sielewi kwa nini yeye hakuwa supported na wanaCCM kama huyu Mzee wa Maembe?

Ndugu, EL hakuwa sapoted kwa sababu:
1. Wana CCM walikuwa mapande 2, Walokosa ulaji (Kiongozi Sam 6, na wenzake- Harison, Anna, nk) vs Timu ilo pata kufaidi "Maisha bora kwa kila ...."
2. RosTamu l'Aziz alikuwa ameitega CCM moja kwa moja (alichota pesa za RichMonduli na kumshirikisha EL moja kwa moja).
3. CCM waliingia kwenye sakata hilo na miguu yoote wakashindwa kutoka. Wakamtoa kafara EL.
4. Za KIA Mejgi alisha poteza uelekeo. Huyu Mama mtata kweli kweli.
 
Wanabodi,

Azimio la Bunge kuhusu Escrow, limetolewa leo, na mjadala wa Escrow, umefungwa rasmi, wakati mjadala huu unaanza, nilisema humu, Hata ikithibitika Fedha za Escrow ni za Wizi, Nawahakikishia Hakuna Atakayewajibika!. Jee leo baada ya mjadala kumalizika, vipi kuna yeyote aliyewajibika?!.

Kwa vile Bunge hili limeishawahi kushughulikia kashfa mbili, ile ya Richmond, na ile ya EPA,

Kama kashfa ya Escrow ni kama Richmond, then je Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa alionewa?!.

Kama wizi huu ni sawa na ule wizi wa EPA, then, Watuhumiwa wa Escrow wasionewe!, kama watu walikwapua mabilioni yale ya EPA na wakasamehewa kwa kutakiwa kurudisha tuu, kwa nini na watuhumiwa wa Escrow wasitakiwa kurudisha tuu yaishe?!.
Pasco.

Mkuu

Kwanza naomba nieleze wazi nakubaliana na statement yako katika post yako ile ingine kuwa watanzania ni Ignorants. Hii sio hata revelation mpya. Ni kitu tunakijua enzi na enzi. Ndo maana mpaka leo kama taifa bado tunakubali kuwa tuna maadui watatu wakubwa Maradhi, UJINGA na Umaskini. Hiyo yenye capital letters ndio IGNORANCE kwa umombo, sasa anayepinga sijui anapinga nini. Kama kuna kondoo mmoja kwenye kundi la mbuzi 100,000, huwezi kukosea ukisema "lile ni kundi la mbuzi." Wenye kuelewa na waelewe.

Pili nijibu hoja hizi mbili;

  • Hata ikithibitika Fedha za Escrow ni za wizi, hakuna atakaye wajibika: Ni kweli watu hawaja wajibika YET, na inawezekana mamlaka ya uteuzi pia isiwawajibishe. Lakini ukweli kwa ujumla hili jambo linawezekana kama litaendelea kufuatilia effectively na upinzani likawa na far reaching consequences than kuwajibika kwa a few leaders. There is a significant shift katika public opionion katika hili suala. Uchaguzi mkuu 2015 utakuwa in a very big way shaped by what has happened bungeni katika hizi week za Escrow! Am not saying it will be enough kuiondoa CCM madaraki lakini it will be enough kupunguza majority ya CCM pale bungeni. Bunge linashindwa kuwajibisha sasa hivi kwa sababu CCM wana a very heavy majority. Kuwa na balanced bunge (utawala na upinzani) ndio key ya mabadiliko katika hii nchi. Na discussion ya Escrow either watu wamejiuzulu or not, it will take a toll on CCM come 2015 sio tu kutoka kwa wapiga kura tu bali hata ndani ya CCM kwenyewe. Naomba ulifikirie hili kwa upana wake na ntafurahi sana kupata your take on this look of things.
  • Kama kashfa ya Escrow ni kama Richmond, then je Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa alionewa?!: Jibu ni hapana. Hakuonewa hata kidogo. Baada ya mapendekezo ya kina Mwakyembe, Lowasa hakusubiri raisi amuwajibishe bali alikubali yeye mwenyewe kuwajibika. Kugoma kwa Pinda na wenzake hakumsafishi Lowasa katika issue ya Richmond. Hawa watu bado hatima yao iko kwa Raisi. Weather JK ataamua kutengua uteuzi wao au atawaacha does not change the facts ya hii issue. Kila mtanzania amesikia na kuona kilichotokea bungeni. Kama executive branch itaamua kutochukua maamuzi magumu then bado bunge linaweza ku deal na PM kwa njia nyingine. Watanzania wameona na wamesikia. Ignorancy ni kutokufahamu, katika hili watanzania hawako tena ignorant. Kama hakuna kitakacho fanyika, come 2015 the ball will be on our court. Na kama niliyosema hapo juu, may be raisi ateendelea kutoka CCM but am 100% sure bunge halitabaki with the same ratio iliyopo sasa.

Kama wizi huu ni sawa na ule wizi wa EPA, then, Watuhumiwa wa Escrow wasionewe!, kama watu walikwapua mabilioni yale ya EPA na wakasamehewa kwa kutakiwa kurudisha tuu, kwa nini na watuhumiwa wa Escrow wasitakiwa kurudisha tuu yaishe?!.

Hatuwezi siku zote kubaki na status quo. Change however slow its speed must eventually come. Two wrongs does not make right. Sikubaliani na hoja kuwa kwa sababu haikutokea kwenye EPA na katika hili la Escrow kusitokee kitu. We need to learn and evolve as a nation from our mistakes.
 
GalaxyS3, NAKUBALIANA kabisa na mtazamo wako,bila kupunguza wala kuongeza kitu. Asante sana.
My take: Kuchelewa kuchua ama Kutochukua hatua yoyote ya kuwawajibisha Fisadz, kama ilivyopendekezwa na Bunge ni hatua kubwa zaidi ya kuondoa "UJINGA" wa wananchi (hivyo kuwapa mwamko zaidi) wa kuibwaga CCM katika uchaguzi Mkuu ujao, ama karibu zaidi, katika kura ya maoni ya Katiba ya Sam 6 na wenzake.
 
Back
Top Bottom