Kama Katiba Yetu Ingeruhusu Matokeo ya Urais Kuhojiwa Mahakamani, Jee Chadema Wangepinga Ushindi wa Magufuli?!.

Kama Katiba Yetu Ingeruhusu Matokeo ya Urais Kuhojiwa Mahakamani, Jee Chadema Wangepinga Ushindi wa Magufuli?!.

Ni lazima tukumbuke yakuwa NASA hawakukurupuka kwani kabla ya hapo waliomba court permit wataalam wao waruhusiwe kuangalia na kuthibitisha ya kuwa matokeo yalichakachuliwa kwa udukuzi wa mitambo!
Baada ya hapo mahakama ilijiridhisha yakuwa kulikuwa na udukuzi ndipo ilipofanya nullification of election sasa je kwa tanzania taarifa za kudukuliwa tulikuwa nazo ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hadi kesho sijawahi kusikia fact yoyote kutoka chadema wameibiwaje...
zaidi ya kukataa ushindi wa JPM na ghafla leo wanamkubali bila ufafanuzi katikati hapo.
 
Wanabodi,
Upinzani wetu bado ni upinzani uchwala!, wanasheria wetu ni wanasheria uchwala, mahakama zetu bado ni mahakama uchwala na baadhi ya majaji wa mahakama zetu pia ni majaji uchwala wakiongozwa na Acting
CJ makini lakini yuko kwenye probation!, ila kwa vile kwa mujibu wa sheria, mwisho wa kukaimu ni miezi 9, na huu ndio mwezi wa 9 tangu alipoanza probation, lets hope mwezi huu, ama atathibitishwa na kuwa CJ, au tutapatiwa CJ kamili!.


Haya ni maoni yangu, vipi wewe mwenzagu, unasema kwa hoja hizi?.

Wasalaam.

Paskali.
Wanabodi,

Kama Mhimili wa Bunge letu tukufu linaweza kufanya mambo shaghalabaghala, Mhimili wa Mahakama ndio ndio uko chini ya Kaimu Jaji Mkuu ambaye mpaka leo ni miezi 9 anakaimu na mwisho wa kukaimu ni miezi 9!, Mkuu wa The Executive ndio huyu anayaikanyaga katiba aliyeapa kuilinda, kuitetea na kuitekeleza, tutegemee nini?!.
Mungu Ibariki Tanzania.
Wasalaam
Paskali
Japo vi sired vingine ni vya kijinga jinga, lakini amini usiami, vinasaidia sana katika amsha amsha!.

P
 
Mkuu umeongea mmbo mengi sana,mi naomba kukuuliza moja tuuu,nani kakuambia mwisho wa Probation/kukaimu ni miezi 9?
mbona kuna watu wengi tuu wana kaimu zaidi ya mwaka/miaka miwili? si anaambiwa bado tunaendelea kukuangalia so Probation extended to 2 years.hata mashirika ya serikali mbona ipo sana hii,Au mimi ndo sielewi?
NATUMAINI JIBU UMELIPATA, WANAOKAIMISHWA ZAIDI YA MIEZI 9, HUWA WANAKUWA WAMESAHAULIKA!.
p
 
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali "Kama Katiba Yetu Ingeruhusu Matokeo ya Urais Kuhojiwa Mahakamani, Jee Chadema Wangepinga Ushindi wa Magufuli?!".

Baada ya Mahakama Kuu nchini Kenya kutengua matokeo ya uchaguzi wa rais, wengi wa wanasiasa, wanaharakati na wana mitandao ya kijamii, wanajielekeza kwenye madai ya katiba mpya inayoruhusu matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani, kwa matumaini kama tungekuwa na sheria hiyo, Chadema Jee Chadema ingefungua shauri mahakamani kuhoji ushindi wa Magufuli kama walivyofanya wenzao wa Kenya?.

View attachment 580135

Kwa swali hili, japo nakuachia wewe kutoa majibu, ila naomba katika kutoa maoni yako, pia naomba uzingatie hoja hizi tatu.

1. Jee Chadema wana hoja za msingi za kuyapinga matokeo hayo mahakamani?.
2. Chadema kama Chama Kikuu cha Upinzani, Jee kina Seriousness ya Kungua Shauri Serious kama Hilo?. Inao wanasheria wenye that capacity kama wanasheria wenzao wa Kenya?.
3. Tuseme Chadema wana hoja za msingi, na wako serious with the capacity kufungua shauri, na wamefungua shauri, Jee Mahakama zetu zenye majaji wanaoteuliwa kwa hisani ya rais, zina uwezo wa kutoa haki kama The Supreme Court ya Kenya?.

Maoni Yangu.
1. Hoja za Chadema.
Baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wetu yaliyompa ushindi Magufuli, Chadema walipinga matokeo hayo, jee walikuwa na hoja?. Jibu langu ni kweli Chadema walikuwa na hoja za msingi kabisa, lakini very unfortunately, hawana uwezo wa kuwasilisha hoja zao, zaidi ya kupiga tuu kelele!. Kama Chadema walikuwa na hoja, lakini katiba yetu hairuhusu matokeo ya urais kupingwa mahakamani, then wangewasilisha hizo hoja zao kwa umma, ili Watanzania tuwaelewe.
Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa ...

Jee kuna any moment ambapo Chadema waliwahi kuwasilisha hoja zao popote?.

2. Seriousness ya Chadema.
Kwa maoni yangu, japo Chadema ndicho chama kikuu cha upinzani kwa Tanzania kwa sasa, lakini Chadema has never been serious hata mara moja katika serious issues zinahusu kwenda mahakamani. Tangu Magufuli ameingia Ikulu, ameanza kwa kuisigina Katiba mwanzo mwisho!. Chadema wangekuwa serious, wangeishakwenda mahakamani!, but they are not!. Kama Katiba imeruhusu mikutano ya kisiasa, Magufuli ameingia madarakani kwa kula kiapo cha kuilinda katiba, halafu akapiga marufuku mikutano ya kisiasa, Chadema padala ya kufungua shauri mahakamani, kupinga huu udikiteta wa rais Magufuli, ndio kwanza wanaunda UKUTA kuhamasisha maandamano na mikutano nchi nchi!. Udikiteta haupingwi kwa maandamano na mikutano, Chadema kingekuwa chama serious, kingefungua shauri mahakamani kuhoji kama katiba inaruhusu mikutano ya kisiasa, Rais Magufuli, amepiga marufuku mikutano hiyo ya kisiasa kwa kutumia mamlaka gani? na kifungu gani cha katiba?.
Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane ...
CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue ...
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...


Hivyo hata kama katiba yetu ingeruhusu matokeo ya urais kuhojiwa Mahakamani, lakini bado Chadema wasingefungua shauri kuhoji matokeo hayo kama wenzao wa Kenya, kwa sababu Chadema hawako serious kihivyo, wangekuwa serious kihivyo, then wangeonyesha seriousness yao katika madogo ambayo sheria zipo lakini they did nothing!. Sasa kama Chadema kwenye hili dogo tuu la udikiteta wameshindwa kuli challenge mahakamani, vipi kwenye kubwa la uchaguzi na matokeo ya urais?.

3. Makamama Zetu Ziko Huru?, Zinauwezo wa Kutenda Haki na Kutoa Haki na Haki Ikaonekana Inatendeka?.

Jibu ni hapana!. Japo mhimili wa mahakama ni moja ya mihili ya dola ambao unapaswa kuwa huru, yaani independence of the Judiciary, lakini kiukweli mahakama zetu haziko huru kivile. Kwanza shauri la kuhoji matokeo ya urais lingewasilishwa, Jamhuri ingekuja na hoja kuwa mjaza pingamizi, awasilishe mabilioni kadhaa mahakamani yalitumika kuandaa uchaguzi, au vikwazo vingine vyovyote, na mfano mzuri zile Kesi za Mchugaji Mtikila (RIP), kuhusu mgombea binafsi!.

Linapokuja suala linalohusu maslahi ya CCM na maslahi ya rais ambaye ndiye mteuzi wa watendani wa mahakama, maslahi ya CCM na maslahi ya rais yanawekwa mbele.
Nani Zaidi Kati ya Bunge na Mahakama?!. The Doctrine of ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki ...
Je, Huu Sio Uvunjaji wa Haki Za Msingi za Binaadamu Unaofanywa na ...
Kaimu Jaji Mkuu wa TZ, pole Prof. | JamiiForums | The Home of ...
Mhe.Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu ...


Hitimisho.
Japo sisi hatuna sheria ya kupinga matokeo ya urais mahakamani, lakini hata kama tungekuwa na sheria hiyo, safari ya kuwafikia wenzetu Wakenya pale walipo, bali ni mbali kwa Tanzania kwa sababu bado hatuna any credible na serious opposition ya kuyafanya waliyoyafanya wenzetu wa Kenya. Upinzani wetu bado ni upinzani uchwala!, wanasheria wetu ni wanasheria uchwala, mahakama zetu bado ni mahakama uchwala na baadhi ya majaji wa mahakama zetu pia ni majaji uchwala wakiongozwa na Acting
CJ makini lakini yuko kwenye probation!, ila kwa vile kwa mujibu wa sheria, mwisho wa kukaimu ni miezi 9, na huu ndio mwezi wa 9 tangu alipoanza probation, lets hope mwezi huu, ama atathibitishwa na kuwa CJ, au tutapatiwa CJ kamili!.

Haya ni maoni yangu, vipi wewe mwenzagu, unasema kwa hoja hizi?.

Wasalaam.

Paskali.
Paschal,Nadhani u-mzima sana.
Nina imani kubwa kuwa kati ya hoja 3,mbili zina majibu na nguvu ya hoja.Ya tatu ni mashaka matupu.

Nikianza na "hoja ya kupeleka mahakamani na kuthibitisha ni kweli na ipo.Kitendo cha Kova na polisi wake kuvamia na kuchukua vitendea kazi vya vijana wa UKAWA ni ushahidi tosha kuwa walifanya juu chini kuondoa ushahidi wa kuwasuta.Iweje wazuie upande mmoja na mwingine waachwe? Kama NASA walithibitisha madai yao ya udukuzi kwa kutumia taarifa za "servers" pia UKAWA wangeweza.Tatizo mazingira yangeruhusu? Matukio ya kuuawa mtaalamu wa IT Kenya nalifananisha na uvamii wa kituo cha UKAWA ili ku-pre-empty hoja/ushahidi.

Pili uwepo au kutokuwepo opposition/wanasheria mahiri sina shaka nalo.Bila nguvu ya dola TUME ya uchaguzi wasingeweza kupangua hoja.Angalia Jecha na maamuzi yake.Na kesi lukuki ambazo Jamhuri wameshindwa kuthibitisha dhidi ya Lissu inaonyesha kuwa uwezo upo.Kizingiti ni "JE UWANJA NI TAMBARARE" kwa wote?

Mahakama nchini kwetu ni tatizo ambalo linahitaji mjadala mpana zaidi.Kifupi tu ni kuwa hatuna mahakimu/majaji wa kuaminika.Rejea uamuzi wa mahakama ya Rufaa dhidi ya mgombea binafsi.Ni aibu kudai Katiba inatoa fursa kwa kila mtu kuchagua na kuchaguliwa lakini unazuia mgombea binafsi.Majaji waliobariki ukiukwaji huo leo wanataka wawe viongozi wa kuchaguliwa!
Katiba nzuri ikipatikana mengine yatajipa kwani itatoa nguvu ya ziada(impetus) kwa wapenda haki,demokrasia na maendeleo kudai na kusimamia maslahi mapana ya nchi.
 
Back
Top Bottom