Kama Katiba Yetu Ingeruhusu Matokeo ya Urais Kuhojiwa Mahakamani, Jee Chadema Wangepinga Ushindi wa Magufuli?!.

Ni lazima tukumbuke yakuwa NASA hawakukurupuka kwani kabla ya hapo waliomba court permit wataalam wao waruhusiwe kuangalia na kuthibitisha ya kuwa matokeo yalichakachuliwa kwa udukuzi wa mitambo!
Baada ya hapo mahakama ilijiridhisha yakuwa kulikuwa na udukuzi ndipo ilipofanya nullification of election sasa je kwa tanzania taarifa za kudukuliwa tulikuwa nazo ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hadi kesho sijawahi kusikia fact yoyote kutoka chadema wameibiwaje...
zaidi ya kukataa ushindi wa JPM na ghafla leo wanamkubali bila ufafanuzi katikati hapo.
 
Japo vi sired vingine ni vya kijinga jinga, lakini amini usiami, vinasaidia sana katika amsha amsha!.

P
 
NATUMAINI JIBU UMELIPATA, WANAOKAIMISHWA ZAIDI YA MIEZI 9, HUWA WANAKUWA WAMESAHAULIKA!.
p
 
Paschal,Nadhani u-mzima sana.
Nina imani kubwa kuwa kati ya hoja 3,mbili zina majibu na nguvu ya hoja.Ya tatu ni mashaka matupu.

Nikianza na "hoja ya kupeleka mahakamani na kuthibitisha ni kweli na ipo.Kitendo cha Kova na polisi wake kuvamia na kuchukua vitendea kazi vya vijana wa UKAWA ni ushahidi tosha kuwa walifanya juu chini kuondoa ushahidi wa kuwasuta.Iweje wazuie upande mmoja na mwingine waachwe? Kama NASA walithibitisha madai yao ya udukuzi kwa kutumia taarifa za "servers" pia UKAWA wangeweza.Tatizo mazingira yangeruhusu? Matukio ya kuuawa mtaalamu wa IT Kenya nalifananisha na uvamii wa kituo cha UKAWA ili ku-pre-empty hoja/ushahidi.

Pili uwepo au kutokuwepo opposition/wanasheria mahiri sina shaka nalo.Bila nguvu ya dola TUME ya uchaguzi wasingeweza kupangua hoja.Angalia Jecha na maamuzi yake.Na kesi lukuki ambazo Jamhuri wameshindwa kuthibitisha dhidi ya Lissu inaonyesha kuwa uwezo upo.Kizingiti ni "JE UWANJA NI TAMBARARE" kwa wote?

Mahakama nchini kwetu ni tatizo ambalo linahitaji mjadala mpana zaidi.Kifupi tu ni kuwa hatuna mahakimu/majaji wa kuaminika.Rejea uamuzi wa mahakama ya Rufaa dhidi ya mgombea binafsi.Ni aibu kudai Katiba inatoa fursa kwa kila mtu kuchagua na kuchaguliwa lakini unazuia mgombea binafsi.Majaji waliobariki ukiukwaji huo leo wanataka wawe viongozi wa kuchaguliwa!
Katiba nzuri ikipatikana mengine yatajipa kwani itatoa nguvu ya ziada(impetus) kwa wapenda haki,demokrasia na maendeleo kudai na kusimamia maslahi mapana ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…