Nobunaga
JF-Expert Member
- Mar 22, 2019
- 1,205
- 5,121
Lile sakata la kufutwa gharama za kuonwa/kuhudumiwa hospitali na wahudumu linazidi kuchanja mbuga. Kwanza tuwekane sawa hapa, haiitwi gharama ya kumuona daktari, inaitwa "Consultation Fee" ikimaanisha "Gharama ya Kuhudumiwa" kwa maana utapita mikono ya wataalamu kadhaa siyo daktari tuu.
Baraza lao wanadai hii pesa huwa inaenda kwenye mfuko wa hospitali. Lakini hii ni danganya toto kwani hali ni tofauti kwa upande wa mifuko ya bima.
Baraza lao wanadai hii pesa huwa inaenda kwenye mfuko wa hospitali. Lakini hii ni danganya toto kwani hali ni tofauti kwa upande wa mifuko ya bima.
Sasa ngoja tusanuane, kwa wale wasiojua. Suala la hii gharama ni kweli inaingia mfuko wa hospitali, lakini ni kwa wagonjwa wanaolipa cash tuu. Consultation fees za mifuko ya bima ina mgawanyo tofauti ambao umekaa kiunyanyasji wa hali ya juu sana.
Consultations fees za bima zote, hospitali inachukua 40%, daktari naye anachukua 40%, wauguzi wanachukua 15% na 5% inayobaki wanachukua wengine kama maabara na wahudumu wa afya.
Sasa ukiangalia hizo % hapo juu unaweza ukaona kama ni kitu kidogo, lakini ngoja niweke figure halisi ndiyo utajua hawa madaktari ni kwa jinsi gani wameweka mfumo wa kitumwa kwa kada zingine wanazoshirikiana nao.
Huo mfano hapo juu ni wa consultation fee ya NHIF ambayo ni 25,000/=. Hospitali inachukua 10,000/=, Daktari anachukua 10,000/=, Muuguzi anachua 3,500/= na wengine wanaobaki wanagawana 1,500/= iliyobaki.
Ndiyo maana nasema hii ni janja janja tuu ya siku zote. Kwanza wale wanaolipia cash, consultation fee mara nyingi ni 10,000/= tuu. Hivyo bima ndizo zina consultation fee kubwa na ndizo hizo madaktari wakajitungia ka utaratibu ka kujikwapulia kiasi sawa na hospitali, huku wakiwabakizia wengine kiduchu.
Nimewahi kuleta uzi humu nikielezea ni kwa namna gani hawa madaktari wamejijengea ka empire kwenye sekta ya afya kiasi kwamba hawataki wengine nao waifurahie hii sekta. Wamejimilikisha sekta ya afya utadhani wako peke yao.

Mh. Rais, Wizara ya Afya ni ka "Empire" ka Madaktari, Kuna "Mfumo Daktari" Ulioota Mizizi
Kwanza kwa heshima na taadhima nakusalimu na kukupa pole Mh. Rais kwa kazi nzito ya kuwaongoza Watanzania na taifa kwa ujumla. Mimi sio mwandishi mzuri sana Mh. lakini naomba nikupe hints chache tu ili ujue na watu wajue ni kwa jinsi gani humo wizara ya afya kuna ki empire kimejengwa ambapo kwa...
Hivyo waziri unapoenda kukaa nao chini kaa nao chonjo sana, wanaweza wakapendekeza consultation fee za cash ndizo zifutwe lakini za bima zisifutwe kwa sababu wao wanafaidika nazo.