Kama kazi yako nitaitaja hapa chini, nakushauri fanya toba ili kizazi chako kisilaaniwe

ukiwakuta wanafarijiana utafikiri wana dunia yao peke yao wanaishi...ila kweli hapahapa dunia ya leo majibu huanza kabla watu hawa hawajafariki..naamini hivyo pia!
 
Uzi wako umezunguka mkuu,ilikuwa iwe hivi..

1.polisi.
2.polisi.
3.polisi.
4polisi
5.polisi
6.polisi.


Askari mgereza yeye anadili na wafungwa tu wala hajui nani ana hatia na nani hana.

Wanaojua nani ana hatia nan nani hana sanasana ni polisi maana ndio wanadili na mtu tokea akiwa huru,waamkamata na kumpeleka kituoni,wanafanya upelelezi,mahakamani na hatimae kifungo.

So utaona hapo magereza unamuonea,anayejua mchakato wote ni polisi.
 
UKO SAHIHI NINA MIFANO MINGI YA TRAFIKI AMBAO WAKO KATIKA TABU KUBWA NA MATESO, PIA WAFANYAKAZI WA TRA, YUKO MMOJA ALIKUA ANAONA SIFA KUJA KULIPISHA WATU KODI ALIJILIMBIKIZIA MALI LAKINI MWISHO WA SIKU ALIKUFA DHALILI KWA KUKOSA HELA YA MATIBABU
Hawa vijana tukiwaambia ukweli wanapinga.
Watu tuko matured enough. Kanuni za kiroho tunazijua.
 
Kiashiria (A) sio kweli maana Kristu alikwisha kitolea ufafanuzi.Wewe ni nani umzidi Yesu?
Polisi, magereza lazima wawepo ili kaisari aweze kutawala vizuri. Katika maandiko matakatifu kaisari anajulikana na anakubalika.Ya kaisari apewe kaisari.Polisi wana jukumu zuri sana la usalama wa raia.Polisi akilifanya vizuri anakuwa amemtumikia Mungu. Bali tu wana tatizo la kutotosheka na mishahara hapo ndio shida..na vitabu vitakatifu viliwaasa. Lkn endapo wapo watendao kwa haki, hao ni polisi wabarikiwa na kazi yao ni njema.
 
Huyo namba 1, umewaonea.
Sifa yao kuu ya kuajiliwa, ni mtu akose akili kabisa.
 
Ohh husomi Biblia sio
'Nawapatiliza wana maovu ya Baba zao...' hujawahi kuiona?
Hakikisha unaomba toba na rehema kuepushwa na dhambi za wazazi wako

Wewe ndio huisomi biblia ...kumbukumbu la torati 24:16

“Wazazi wasiuawe kwa makosa ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya makosa ya wazazi wao. Kila mtu atauawa kwa makosa yake mwenyewe.

Ezekiel 18.20

"Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake."
 
Ohh husomi Biblia sio
'Nawapatiliza wana maovu ya Baba zao...' hujawahi kuiona?
Hakikisha unaomba toba na rehema kuepushwa na dhambi za wazazi wako
Unaisoma biblia bila ya kuelewa

Aya ina maanisha kuwa watoto watapata athari za dhambi za baba zao vizazi mpaka vizazi.

Mfano ukilelewa katika familia mnayoabudu masanamu basi ni wazi kuwa watoto watarithi mila, desturi na mienendo mibovu ya baba zao . Ila Mungu hana sifa ya dhulma kwa viumbe wake kiasi aje aadhibu kizazi cha nne au cha saba kwa makosa waliyofanya babu zao. Kila kiukbe kinaadhibiwa kwa yale mabaya na maovu kilichoyachuma. Vizazi vijavyo vitapatilizwa tu endapo vitarithi yale maovu ya baba zao
 

Usisikie ya wajinga eti jela ni jeraha
We ndo' kwanza mwaka mmoja wenzio kumi wamekaa
Kwanza muda ushaisha haturuhu tena stori
Naomba urudi bwenini ILA OH, I'M VERY SORRY
NI KWELI INIUMA ILA MI NKO KAZINI
Hey, afande Maku embu warudishe kundini hao
 
7. Anayesimamia uchaguzi na kuhujumu matokeo huku ajira yake ikimnyanyasa na mshahara wake wote amechukulia mikopo
 
unawaacha wapi watumishi wa hizi Halmashauri wanaoshughulika na maswala ya ardhi na wenzao wa wizara ya ardhi hawa ndio laana kabisa
 
8. CCM
9. Wabunge
10. Mawaziri
11. Rais
 
Haya mambo ya kutiana hofu ni upuuzi tu.Kutengeneza hadaa ndani ya imani ya kweli na ikawa sehemu ya mafundisho ya dini,kuitumia dini kama silaha ya kuogofya watu na kuwaibia.Ukilinganisha na hawa askari ni yupi astahili laana zaidi?Mimi naona mwenye laana ni yule aliyeng'ang'ania dini za kimapokeo ambazo undani wake ni utapeli na akili yake imefungwa.Watoto,wajukuu,vitukuu wanarithishwa utapeli huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…