Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Huwa siamini kama ni wewe wa zamani au mwenyewe alikufa kilaza mmoja akawa anatumia id yake
 
JPM hakuwa ethical. Alitegemea "ubabe" tu. Binafsi, suala la Uwanja wa Ndege wa Chato, ilikuwa indicator ya kwanza kabisa kuwa hayupo ethical kabisa.....mengine yakafuata. Ukabila, ukanda, mauwaji, utekaji, uonevu, udhalilishaji, kutofuata sheria/katiba, kuminya uhuru wa maoni, kuminya uhuru wa habari nk nk. Kwa kipimo changu cha ethicality, JPM hajawahi kupita hata mara moja.

Hii haina maana hakuna mazuri alofanya. Yapo mengi tu. Kama watangulizi wake pia walifanya mengi mazuri na mabaya...naye pia vivyo hivyo.
 
Hayo aliyaanza kikwete na magufuli kaendeleza. Hizo barabaraza kuunga kila mkoa alizijenga kikwete akaondoka ameacha mikoa miwili. Ila nashangaa kila jambo mnampa magufuli kama hata waliyofanya wengine kama vile aliikuta nchi haina kitu hata kimoja.
Leo mnapingana na report ya CAG aliyemteua mwenyewe.
 
Uyo MM ni sukuma gang au mfia meko wanateseka sana kuona mwendazake anavyo funuliwa sasa
 
tusimsingizie Magufuli kwa kila kitu.

Kuna kikundi ama kingenge cha wahuni sijui kinalipwa na nani kutaka kumchafua Magufuli na report ya cag
Tulia wewe! Kama unaona uchungu mfuate huko, mwenzio kakimbia msala.
 
Jibu rahisi... Ninkwamba


: Transparency isingekuruhusu kuoakuwa pesa zote na kwenda kujenga mahospitali....binge lisingekubali.

:Transparency isingekuruhusu ujenge mabarabara kamanlile la kijazi

: Transparency isingekuruhusu uwakataze hela watu wasile ukimbize kwenye miundo mbinu....

Hata hivyo Binafsi nilidhani angekiwa na kikundi anachokiamini awe anashauriana nacho. Ungekiwa ubabe usio na makosa.

Endelea......
 
Hapa ndipo elimu inapaswa kuheshimiwa Assad aliulizwa kama kuna upotevu was T1.5 hadharani ili Rais afukuze watu hadharani nikumbushe jibu alilotoa .Kukurupuka na kauli za wanasiasa hauwezi kupata uhalisia wenzako wako kazini na wewe soma iyo riport ,nikikuuliza Magufuri kafanya ufisadi upi?nipatie jibu,sio kucheza na mdundo unaopita barabarani.
 
Wasalaam

Ama baada ya salam. Ni kiri kwa moyo na kuandika kwa msaada wa madole gumba haya mawili kwamba, tusichofahamu ni kwamba MAGUFULI amefariki, alikua mwema au muovu aliwaonea watu au aliwahurumia haibadilishi ukweli kwamba MAGUFULI amefariki na kuzikwa nyumbani kwao Chato.

Mama Tanzania ni lazima aendelee, ni tuwepo au tusiwepo. Kinachoniumiza ni kwamba "limeibuka kundi la wanaoogelea kufuata muelekeo wa mawimbi wamejisahaulisha hilo"

Mama Samia Suluhu Hassan kazi iliyoko mbele yako ni kubwa na inayohitaji weledi mkubwa pia.
Naokuomba mama yangu anza kuangalia namna gani unaweza kudhibiti team ya watu wanao shambulia Legacy ya Magufuli kwani wakimaliza watakugeukia wewe na mliokuwepo wote na tahamaki Uchaguzi 2025 huu hapa.

Mzee wangu Mwanakijiji wewe ni miongoni Mwa watu waungwana waliobaki katika Dunia hii na Mwenyezi Mungu akuongezee ufahamu.
 
Bunge hatuna, hivi!!
Kunakisa lipi wananchi tukiandamana kwenda kwenye jengo letu pale bungeni ili kuwaondoa wote ili turudi kwenye uchaguzi
 
Bunge hatuna, hivi!!
Kunakisa lipi wananchi tukiandamana kwenda kwenye jengo letu pale bungeni ili kuwaondoa wote ili turudi kwenye uchaguzi
Naunga mkono hoja .Iko haja wanananchi tuwaonyeshe kuwa hatuna imani na bunge lililojaa wanafiki wakiongozwa na spika Ndugai
 
Hivi Katiba hairuhusu Spika kujiuzulu..!??
Hastahili kuwepo pale bungeni hata sekunde..
 
Mtu anaepingana na Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambayo kwa hakika haijaacha shaka yoyote juu ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma; nathubutu kusema kwamba atakuwa sehemu ya ufisadi. Mwanakijiji unapohoji waliopo kwanini walishindwa kuchukua hatua lazima ufahamu kwamba na ujiulize swali kwamba kiongozi mkuu wa serikali aliruhusu kukosolewa? Kwa hiyo mimi sidhani kama serikali inayoendelea inakosa legitimacy as long as imeamua kuwaonyesha watanzania ukweli kwa kumruhusu CAG ''Asimung'unye Maneno'' hii ni hatua ya dhati kabisa; hasa ukizingatia kwamba hatujapata Ripoti yoyote ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali tangu Assad aondolewe kwenye kiti chake.
 
Hao siyo wanyonge , bali ni wajinga na wanstumika kama mtaji wa wanasiasa matapeli.
 
Kama huu ufisadi mrioripoti ni kweli basi hata rais wa sasa anahusika kwa sababu alikuwa sehemu tena muhimu ya serikali wakati yanafanyika haya, kusema sijui hakuwa na kauli sijui nini ni kudanganyana. Kama hakukubaliana nayo angeachia ngazi abaki na heshima yake, kubaki madarakani ilikuwa ni kuunga mkono kila kilichofanyika. Ndugai alikuwa spika wa bunge lenye jukumu la kuisimamia serikali na hakutimiza/hawakutimiza wajibu huo ipasavyo, so nashauri tuanzie kwa kuwaburuza wote hao mahakamani sheria ipite nao. Kuendelea kushabikia wizi wakati walioshiriki wizi huo wapo na tena wanatuongoza mbele mbele katika kushangilia ni unafiki na uzandiki.
so mimi nasimama kuhesabiwa........ KAMA UFISADI HUU WOTE ULIFANYIKA WAKATI SAMIA SULUHU HASSAN AKIWa MAKAMU WA RAIS AWAJBIKE kwa sababu ndiye alikuwa msaidizi namba moja wa rais aliyekuwepo madarakani. Kusema eti kwa sababu aliyekuwa rais hayupo basi na ufisadi Huu tuachane nao ni unafiki na uzandiki wa hali ya juu.
 
Nimesoma lakini sijaelewa unataka kufikisha ujumbe gani.
Amesema hivi wanaosema tumepigwa sana na huu ufisadi wanaouonyesha kila kona walikuwa panoja na JPM MUDA WOTE LEO WAMEGEUKA KAMA.VILE ALIVYOGEUKA JOM KWA JK ni mwendo wa KARMA
 
Kwa hiyo unataka kusema Shirika letu la Ndege lipo vizuri hamna ufusadi wowote wanamsingizia marehemu?

NIDA, Bandari, NSSF kote safi?

Pesa hizo alizokuwa anatembea nazo kwenye gari, anagawa mitaani, zilikuwa zinatoka fungu lipi, kwa idhini ya nani?

Tufahamishe mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…