Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Ukisoma mitandao ya kijamii hasa twitter utafikiri kweli hii nchi imeibiwa kila kitu na hakuna kitu kimeachwa, kumbe sio kweli.

Watu wanajifanya kushangaa ATCL kupata hasara, hivi mtu mwenye akili timamu unaweza kushangaa atcl kupata hasara? By the way, ni shirika gani la serikali linalopata faida? Lipi? Mashirika yote ni hasara kila mwaka kuanzia Tanesco, TPDC, TTCL, ATCL, NHC na mengine yote, kwa nini shida iwe kwa ATCL?

Halafu watu wanataka kusema Magufuli ange eliminate rushwa ama wizi wa mali za umma 100%, hilo jambo halipo Duniani. Duniani kote, kuanzia China ambapo kosa la rushwa unaweza kuuwawa ama Marekani ambapo mifumo iko strong bado watu wanaiba na kula rushwa, tusimsingizie Magufuli kwa kila kitu.

Kuna kikundi ama kingenge cha wahuni sijui kinalipwa na nani kutaka kumchafua Magufuli na report ya cag
Umeandika utopolo mtupu. Ila sio kosa lako itakuwa shule za kata hizi na vyuo vya kata huko ndio ulikolelewa; ndio maana huwezi kukuta mtoto wa kiongozi anasoma shule za kata wala vyuo vya kata.
Yaani Tanesco ndio ya kupata hasara [emoji23][emoji23] halafu unashangaa kwamba Atcl isipate hasara Daaah

We kiazi kweli
 
Naiona sababu kubwa baadhi ya nchi ambazo raia wanaamua kuandamana na wengine wanaamua kwenda msituni.

Yaaaani serikali na uchafu wooooiiiite huu kwa mjibu wa wao wenyewe lakini bado chama kiko madarakani na serikali yake yooooote iko madarakani?

Na mbaya zaidi kinataka kiendeleee kuwa madarakani.

Hapa kwa mbaaaaaaaali jeshi letu nalo ambalo tuliamini ni safi baadhi vitengo vyetu vinatumika kupitisha ufisadi?


Baaasi ki ukweli wanyonge tulipewa nafasi na sisi ya kupata ka ridhiki maeneo wanayotamani kutufulumusha asee tujiandaeni kuwapisha wenye magari aseeee.




Wapinzani nao badala kuandaa mazingira ya kutupokea, mnaanza na nyie tena kusherekea
ANZA WEWE BABAYE ACHA KULAUMU WENZIO
 
Sidhani kama huu CAG ni mkweli.Yani kaaamua kwa makusudi kununulika Kuiua CCM na Tanzania .ni aibu kwa kweli.Tunarudi nyuma kwa kasi ya ajabu.
Kama Mwanakijiji alivyosema kuna kitu kinaundwa.Ajabu Spika hajui kinachoundwa.in short CCM is finished ,Tanzania is finished.
 
Anachojaribu kusema ni hiki

Kama Magufuli alikuwa nduli, fashisti na fisadi basi alikuwa mzuri. Mtu Fisadi anakwapua pesa halafu anapeleka umeme kila kijiji na Elimu bure nchi nzima na zahanati nchi nzima na miradi ya barabara nk hadi vichochoroni. Mistendi kibao hadi mingine inaitwa stendi ya Ndugai hilo fisadi na fashisti na nduli wananchi tunalikubali sababu lilikuwa linakwapua na kuwapelekea wanyonge miradi kibao.

Lingebaki liendelee kufisadi na kupelekea wanyonge

Haya tunasubiri msio nduli na mafashisti na msio mafisadi tuone kama spidi ya maendeleo kwa wanyonge ya hilo nduli,fashisti na fisadi tuone kama spidi hiyo mtaiweza.Tuone nani zaidi kati ya nduli fashisti na Fisadi Papa Magufuli na ambao sio nani zaidi .Wanyonge ndio watakuwa mahakimu kwa hili
Kwamba JK hakufanya kitu?
 
Upinzani uko kwenye damu yangu; ila sasa hivi naona kama umepotea maana sijui ni nani amebakia upinzani kweli. Labda tuunde upya kabisa... maana upinzani umekubali jukumu lisilo lao...
upinzani haukupotea bali ulipotezwa kimabavu na wengi tukashangilia....Mtu mmoja alitumia maguvu yake isivyo halali kuusambaratisha upinzani ili asipigiwe kelele anapofanya mambo yake...huo ndio ukweli mchungu ambao wengi hamtaki kuusema lakini inakera saaana..

Tunapomuita Ndungai mnafiki bali na wengi wetu tujue pia ni wanafiki, wakati maovu yanaendelea na watu wanaumizwa kwa sababu ya misimamo yao wengine mliwakebehi na kuwabatiza majina kedekede....mitandao ilivyominywa na watu kufungwa midomo wengine mkasema wapinzani hawana akili oooh fulani jembe...nk

Inasikitisha saana, tuseme tu nyekundu ni nyekundu tuache ushabiki..
 
Dhani hujamwelewa Mwanakijiji rudia Tena kusoma,
Mm nimejaribu kumwelewa kidogo anachosema,Kama huo ufisadi umetokea kweli na aliyekufa ni mmoja na waliokuwa wanamsaidia wote wapo Kuna haha gani ya kuwa na serikali iliyokuwa inatudanganya? Ni muhimu wote wajiuzuru na kufanya uchaguzi upya.
KIUKWELI NAISIKITIKIA TANZANIA YANGU NA WANANCHI.
WANASIASA RISASI NI ADHABU PEKEE KAMA CHINA

Magufuli alikuwa waziri kwa miaka mingapi kabla ya kuwa Raisi? Mbona hakujuuzulu kwa ufisadi uliofanyika akiwa waziri na badala yake akasubiri awe Raisi na kuanza kushambulia ufisadi uliopita huku akificha kwa mtutu wa bunduki ufisadi wa serikali ambayo yeye ni Raisi.
 
Unaandika mithili ya layman. Kwani kuwa mpinzani lazima ujinasibishe na wapinzani unaowaita wamepotea?

Wewe binafsi ume compromise nafsi yako kwakua wengine wamepotea? Really?

Hivi misimamo na ideology za mtu huwa kwa wengine au wewe binafsi?

Kwahiyo huko nyuma ulifanya upinzani kwakua wengine walifanya?

Au kauli na matendo yako yanadhihirisha ulifanya mambo kwa chuki binafsi, chuki za kimaslahi, kikanda, kidini na kirangi? Seriously mtu mwenye upinzani wa Moyoni unaweza sema nilishindwa fanya upinzani maana sikumjua mpinzani wa kweli?

Seriously mtu wa kariba yako ulikuja kuwa simply brainwashed na siasa za watu aina ya akina Magufuli really?
Hakuna kitu hapo menyimwa ufahamu kwa sababu ya mahaba kwa huyo mungu mtu wenu,

Mbona kuna miradi mikubwa na mingi ilifanywa wakati wa kikwete au kwavile mlikuwa haipigiwi debe kama ilivyo kuwa inapigiwa debe kwa mungu mtu wenu? Na ukifanya analysis kikwete katekeleza miradi mingi mikubwa sana awamu yake kuliko huyo kibwetere wenu ila tu hayakuwa matangazo na sifa kama ilivyo kwa huyo mungu mtu wenu

Tatizo huyo mungu mtu wenu alitaka hata akijamba tu dunia nzima asikie na umsifie na ndio hapo mlipo hadaika wale wote wenye akili ndogo mnao danganyika kirahisi

Nina hakika wewe kama ni mwanamke basi jamaa watakuwa wanajisevia sana na kama ni mwanaume sijui hata nisemeje.
 
Humjui huyu jamaa, pitia maandishi yake ya nyuma sana utaelewa kwamba jamaa yuko vizuri sana kichwani, ila baada ya ku-side na Magu hana article anayotumia akili siku hizi.

He was so objective by then.
Leo kaandika vizuri sana mkuu.Soma tena utamuelewa.
 
Nimesoma lakini sijaelewa unataka kufikisha ujumbe gani.
Soma tena mkuu, utaelewa. Mi nimesoma mara 1 tu na nimemuelewa mzee mwanakijiji. Anajaribu kusema, kama mwendazake alifanya ufisadi ilihali kafanya vitu vinavyo onekana hadi sasa na tena aliokua anafanya nao ndio hao hao leo wanashiriki kumkosoa then sisi kama wananchi tuna sababu gani ya kuwaamini kina Majaliwa, Ndugai na hata mama? Si wote walikua team moja? Ndicho anacho jaribu kutwambia wasomaji wake
 
Hii nchi imejaa mashetani. JPM alitufungua akili na kutupa ujasiri sisi wanyonge. Tunawasubiri tu, ngoja tuone
 
Deni la Taifa limekuwa kwa Trillion 18 katika kipindi chake cha miaka 5 tu. Tulikuwa tunaambiwa hiyo miradi inajengwa kwa pesa zetu za ndani!
Na. M. M. Mwanakijiji

Ufisadi uliofanyika wakati wa miaka mitano ya Rais Magufuli tunaambiwa ni mkubwa sana. Kwamba, mabilioni ya fedha yameliwa na wajanja na kuwa fedha hizi zimeliwa na watu walioteuliwa na kusimamiwa na Rais Magufuli. Kwa haraka haraka - kama kawaida naona siku hizi - wakosoaji wa Rais Magufuli (na hapa nawazungumzia wale wa kisiasa) wameruka ruka kwa shangwe wakisema "si tuliwaambia!". Na kinachosikitisha kidogo ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wamejitambulisha kuwa ni wapinzani nao wamerukia kwa furaha tu na hata hawajui ni kitu gani wanaandaliwa. Sijui ni nani anayewalengesha hawa lakini kilichofanyika na kinachoandaliwa labda ni cha kutisha zaidi kuliko kilichotokea. Kuna mtu aliuliza (jamaa yangu Philemon Michael) wakati msiba ulipotangazwa maswali ambayo sidhani kama kuna mtu atakuja kuyauliza hadharani au kutaka kuyajibu yaeleweke. Na kuna mtu aliuliza tena wakati CAG amewasilisha Bungeni ripoti yake kwamba je hii ndio ile ile ripoti ambayo kama JPM angekuwa hai angekabidhiwa? Sijui jibu lake... Kama ni ile ile inawezekana hakukuwa na jinsi ripoti hii ingekutana na JPM meza moja... Kama ni nyingine... Magufuli alikuwa sahihi mara ya 1.

Hii miaka mitano tumeshuhudia miradi mikubwa ya kila namna na hata tukajisikia kuwa kuna kifu kinafanyika... lakini leo tunaambiwa lote ni changa la macho. Hizo hospitali hakuna zilizojengwa, hakuna masoko, hakuna vituo vya mabasi, hakuna shule zilizofanyiwa matengenezo makubwa, hakuna hiki wala kile na hata ndege tulizoambiwa zilinunuliwa kwa fedha taslimu kumbe hazikununuliwa... yaani, hata hii SGR na Bwawa la Umeme la Nyerere yote ni geresha tu! Kwamba kote huku watu walikuwa wanakula tu na tunachokiona hakipo na kama hili ni kweli basi Magufuli alikuwa sahihi mara 2.

Lakini kingine ni kuwa baadhi ya watu ambao waliteuliwa na Magufuli, walifanya naye kazi, na waliimba "maendeleo" "maendeleo" na hata kusifia kuwa tumeachiwa "urithi" kumbe si kweli; tumeachiwa madeni na ufisadi. Na kwa vile hakuna anayejitokeza kuwa na ujasiri wa kutetea walichokifanya kwa sababu kuna mtu anaitwa "Mwendazake" ameende na utetezi wake kumbe watu wamelia bure. Leo wengine (kina Ndugai) wanageuka wazi wazi; kumbe walikuwa wanaunga mkono uongo; walikuwa wanashangilia ulaghai, na walikuwa wanaficha ufidadi.. hapa watanyoshewa kidole wote kuanzia aliyekuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri wote (na wengi wamerudi au kuhamishwa) na kwa kweli inawezekana wabunge wote walioweza kuingia wakisimama nyuma ya Magufuli. Kama hili ni kweli kwamba ufisadi umetokea wakati watu wale wale ambao leo wanatufunulia ufisadi huo walikuwepo basi Magufuli alikuwa sahihi mara ya 3.

Swali kubwa ni usahihi gani ambao ninauzungumzia? Mwenye kusoma na aelewe. Kama kinachodaiwa na kushangiliwa leo ni kweli basi nchi haina kitu kingine cha kufanya bali kurudi kwenye uchaguzi mkuu mapema zaidi (labda Oktoba mwaka huu) kusafisha uchafu huu; ili wananchi wasisubiri kupigwa tena miaka mitano ijayo... Kama kina Majaliwa na wenzake wote hawakubaliani na assessment hii ya kuwa wamekuwa ni serikali ya kifisadi basi Waziri Mkuu aongoze kujiuzulu mara moja ili kumpa Rais nafasi kweli ya kuunda serikali anayoitaka ambamo ndani yake asirudi HATA MMOJA ALIYEKUWA NDANI YA SERIKALI YA MAGUFULI. Ndio maana ya KUWAJIBIKA KWA PAMOJA.

Wakitaka kuendelea bila kuwajibika ni lazima kuna kitu kingine kinaandaliwa. Ajenda ya Magufuli haijafa, haitakufa na kwa hakina haitoachwa ife. Maana, kama ufisadi huu umefanyika kwa kiasi hiki basi inawezekana Magufuli alikuwa ni genius aliyepindukia. Yaani, kama ufisadi kama huu ungefanyika wakati wa Mkapa au JK hii nchi ingekuwa mbali sana!
 
Back
Top Bottom