Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Hebu tuondolee UPUMBAVU wako! Eti ajenda ya Magufuli haijafa!!! Tangu 2016 kila ripoti ta CAG ilikuwa imejaa madudu ya kutisha na hakuchukua hatua zozote zile zaidi ya yeye na Ndugai kuja na mkakati wa kumfukuza CAG Assad kwa kusema ukweli kabisa kwamba Bunge ni dhaifu. Una akili sawa sawa wewe? Magufuli kakwapua hazina 2.7 trillions ndani ya miaka miwili tu ya mwanzo na kugomea uchunguzi huru. Toa ujinga wako!!!!
NAKAZIA mkuu
 
Mbona hawakuhoji akiwa hai. Bunge si ni taasisi huru inayojitegemea kuisimamia serikali. Waache akili ya mbuni
Bunge halikuwa huru chini ya huyu dictator. Kwanza alilizima likawa linajdili gizani kinyume na sheria. Cag asingesoma hiyo riport tungesomewa nyingine ya kumpamba tu. Hakutaka kabisa kukosolewa. Aliyedieiki kumkosoa aliuawa au kupigwa risasi au kupoteza kabisa Kama akina mdude, lisu, Ben saa nane b.k.

Hivyo hatukuwa na rais tulikuwa na shetwani
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ufisadi uliofanyika wakati wa miaka mitano ya Rais Magufuli tunaambiwa ni mkubwa sana. Kwamba, mabilioni ya fedha yameliwa na wajanja na kuwa fedha hizi zimeliwa na watu walioteuliwa na kusimamiwa na Rais Magufuli. Kwa haraka haraka - kama kawaida naona siku hizi - wakosoaji wa Rais Magufuli (na hapa nawazungumzia wale wa kisiasa) wameruka ruka kwa shangwe wakisema "si tuliwaambia!". Na kinachosikitisha kidogo ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wamejitambulisha kuwa ni wapinzani nao wamerukia kwa furaha tu na hata hawajui ni kitu gani wanaandaliwa. Sijui ni nani anayewalengesha hawa lakini kilichofanyika na kinachoandaliwa labda ni cha kutisha zaidi kuliko kilichotokea. Kuna mtu aliuliza (jamaa yangu Philemon Michael) wakati msiba ulipotangazwa maswali ambayo sidhani kama kuna mtu atakuja kuyauliza hadharani au kutaka kuyajibu yaeleweke. Na kuna mtu aliuliza tena wakati CAG amewasilisha Bungeni ripoti yake kwamba je hii ndio ile ile ripoti ambayo kama JPM angekuwa hai angekabidhiwa? Sijui jibu lake... Kama ni ile ile inawezekana hakukuwa na jinsi ripoti hii ingekutana na JPM meza moja... Kama ni nyingine... Magufuli alikuwa sahihi mara ya 1.

Hii miaka mitano tumeshuhudia miradi mikubwa ya kila namna na hata tukajisikia kuwa kuna kifu kinafanyika... lakini leo tunaambiwa lote ni changa la macho. Hizo hospitali hakuna zilizojengwa, hakuna masoko, hakuna vituo vya mabasi, hakuna shule zilizofanyiwa matengenezo makubwa, hakuna hiki wala kile na hata ndege tulizoambiwa zilinunuliwa kwa fedha taslimu kumbe hazikununuliwa... yaani, hata hii SGR na Bwawa la Umeme la Nyerere yote ni geresha tu! Kwamba kote huku watu walikuwa wanakula tu na tunachokiona hakipo na kama hili ni kweli basi Magufuli alikuwa sahihi mara 2.

Lakini kingine ni kuwa baadhi ya watu ambao waliteuliwa na Magufuli, walifanya naye kazi, na waliimba "maendeleo" "maendeleo" na hata kusifia kuwa tumeachiwa "urithi" kumbe si kweli; tumeachiwa madeni na ufisadi. Na kwa vile hakuna anayejitokeza kuwa na ujasiri wa kutetea walichokifanya kwa sababu kuna mtu anaitwa "Mwendazake" ameende na utetezi wake kumbe watu wamelia bure. Leo wengine (kina Ndugai) wanageuka wazi wazi; kumbe walikuwa wanaunga mkono uongo; walikuwa wanashangilia ulaghai, na walikuwa wanaficha ufidadi.. hapa watanyoshewa kidole wote kuanzia aliyekuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri wote (na wengi wamerudi au kuhamishwa) na kwa kweli inawezekana wabunge wote walioweza kuingia wakisimama nyuma ya Magufuli. Kama hili ni kweli kwamba ufisadi umetokea wakati watu wale wale ambao leo wanatufunulia ufisadi huo walikuwepo basi Magufuli alikuwa sahihi mara ya 3.

Swali kubwa ni usahihi gani ambao ninauzungumzia? Mwenye kusoma na aelewe. Kama kinachodaiwa na kushangiliwa leo ni kweli basi nchi haina kitu kingine cha kufanya bali kurudi kwenye uchaguzi mkuu mapema zaidi (labda Oktoba mwaka huu) kusafisha uchafu huu; ili wananchi wasisubiri kupigwa tena miaka mitano ijayo... Kama kina Majaliwa na wenzake wote hawakubaliani na assessment hii ya kuwa wamekuwa ni serikali ya kifisadi basi Waziri Mkuu aongoze kujiuzulu mara moja ili kumpa Rais nafasi kweli ya kuunda serikali anayoitaka ambamo ndani yake asirudi HATA MMOJA ALIYEKUWA NDANI YA SERIKALI YA MAGUFULI. Ndio maana ya KUWAJIBIKA KWA PAMOJA.

Wakitaka kuendelea bila kuwajibika ni lazima kuna kitu kingine kinaandaliwa. Ajenda ya Magufuli haijafa, haitakufa na kwa hakina haitoachwa ife. Maana, kama ufisadi huu umefanyika kwa kiasi hiki basi inawezekana Magufuli alikuwa ni genius aliyepindukia. Yaani, kama ufisadi kama huu ungefanyika wakati wa Mkapa au JK hii nchi ingekuwa mbali sana!
Unevurugwa ukavurugika. Kweli wewe ni shabiki kindakindaki wa huyu mtu, huoni wala husikii.
Naona huamini kabisa macho yako kwa unayoyasikia kuhusu huyu kiongozi wa Malaika.

Kuna aliyeelewa huyu Mataga alichoandika?
 
Mag
Ukisoma mitandao ya kijamii hasa twitter utafikiri kweli hii nchi imeibiwa kila kitu na hakuna kitu kimeachwa, kumbe sio kweli.

Watu wanajifanya kushangaa ATCL kupata hasara, hivi mtu mwenye akili timamu unaweza kushangaa atcl kupata hasara? By the way, ni shirika gani la serikali linalopata faida? Lipi? Mashirika yote ni hasara kila mwaka kuanzia Tanesco, TPDC, TTCL, ATCL, NHC na mengine yote, kwa nini shida iwe kwa ATCL?

Halafu watu wanataka kusema Magufuli ange eliminate rushwa ama wizi wa mali za umma 100%, hilo jambo halipo Duniani. Duniani kote, kuanzia China ambapo kosa la rushwa unaweza kuuwawa ama Marekani ambapo mifumo iko strong bado watu wanaiba na kula rushwa, tusimsingizie Magufuli kwa kila kitu.

Kuna kikundi ama kingenge cha wahuni sijui kinalipwa na nani kutaka kumchafua Magufuli na report ya cag
magufuli hasafishiki. Kwa kuzuia uwazi serikalini , yeye ndiye icon wa ufisadi nchi hii.
 
Mwanakijiji,
Zamani kuna watu walikuwa wanaitwa Nyumbu, mie nilikuwa sijui, sasa ndiyo nimeamini humu Nyumbu ni hawa wafuasi wa wapinzani, sometimes na wapinzani wenyewe. Kwanza wana attack individual, wanasahau kuwa system ndiyo mbovu. Angalia wamesahau kabisa kuwa Kikwete ndiyo alikuwa mtesaji wao kile kipindi cha awamu ya nne, sasa kawa JPM. Hawajui hao wote ni system ambayo ipo na CCM, na itakuwepo wakati wote.

Pili baada ya kifo cha JPM wanaongea mengi sana, ok I am independent, sikupenda JPM his part of human rights, lakini kwa kazi zake ni nani kama yeye? Sasa angalia Nyumbu wamebadirishiwa "narrative" na hiyo hiyo system kuwa JPM alikuwa fisadi sasa wanaamini na kushangilia ati mnaona? Ukweli upo pale pale CCM na system iliyopo ndivyo ilivyo. Angalia huyu mama Samia, mimi naona ni mama wa Mipasho tu, alikuwa na magufuli pamoja yeye ni VP atajitengaje na yale aliyoyafanya magufuli?? Or let say, JPM was sleeping with the Devil? Unam-support mtu kwa maneno kumbe moyoni sivyo? What I am seeing ni kuwa huyu Mama wa Mipasho na JK were very patient, the Vultures, are Patient Birds. Na kweli sasa wanabadirisha "Narrative" sasa Nyumbu wanashangilia. Hawajui kuwa muda si mrefu watalia.

Halafu kuna Group la tatu, hawa watendaji waliokuwa na JPM, wachumia tumbo. Hawa lazima waonyeshe mwelekeo wao maana lazima wajue watakula wapi. Kama tunavyoona Ngugai, kabadirika ghafla, CAG kabadirika ghafla, HK kabadirika ghafla, Nape katoa makucha, they must show where they are.

"The way the coockie crumbles" JPM itakuwa ndvyo alifikiria alipoona kifo kinakuja, we only live once!!
Unless kama unasema walipaswa kujiuzulu iwapo kama hawakuwa wanakubaliana naye on various issues, vinginevyo mwendazake alikuwa anashaurika?
Japo mwendazake anaweza kuwa alikuwa na nia safi lakini kwa ile modality ya one man show basi mengi yalipita humo kwa humo...
 
Mwandishi ni kama vile hutaki kuamini kuwa Magufuli alikuwa fisadi namba moja wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Ripoti rasmi za kiuchunguzi wa pesa (CAG) za sasa zinaonyesha hivyo. Ni upigaji mtupu.

Kwanini ushangae hilo sasa wakati wakosoaji wa Magufuli walikuwa wakiyasema hayo kwa miaka mitano yote?

Ni akina nani waliohoji upotezi wa Trilioni 1.5 zilizotajwa na Professor Assad?
Kwanini Professor Assad alifukuzwa kimizengwe?

Kwanini vyombo vya habari vilizibwa midomo?

Kwanini wapinzani walipotezwa, kununuliwa, kuteswa na kuuwawa?

Kwanini wapinzani walinyimwa fursa ya kufanya siasa, kushika ikulu, kuingia bungeni, kutawala serikali za mitaa au mabaraza ya halmashauri ?

Kwanini genge la Magufuli lilikuwa likiratibu utawala wa Magufuli udumu milele?

Kwanini tender zote za miradi mikubwa ziwe siri ya Magufuli na ikulu tu?

Kwanini genge la Magufuli lilitaka kupindisha mambo kwa gharama yoyote ili kukamata kiti cha urais hata baada ya Magufuli kuwa mahututi/kufariki dunia?

Ukweli unaweza kuchelewa kujionyesha, lakini muda utaufunua ukweli wote. Muda umefika sasa kwa utawala wote wa Magufuli kupimwa upya. Tusiogope kusema ukweli hata kama ukweli huo utatufedhehesha baadhi yetu.
Madhani hujamwelewa Mwanakijiji rudia Tena kusoma,
Mm nimejaribu kumwelewa kidogo anachosema,Kama huo ufisadi umetokea kweli na aliyekufa ni mmoja na waliokuwa wanamsaidia wote wapo Kuna haja gani ya kuwa na serikali iliyokuwa inatudanganya? Ni muhimu wote wajiuzuru na kufanya uchaguzi upya.
KIUKWELI NAISIKITIKIA TANZANIA YANGU NA WANANCHI.
WANASIASA RISASI NI ADHABU PEKEE KAMA CHINA
 
Kwa Magufuli bus terminal nakubaliana na CAG, iko karkbu sana na barabara. Hilo kwa mtu ambae unaona mbali lazima utaliona tu.

Sijui kwa nini watanzania tunapenda kujenga karibu na barabara. Ile stend iko karibu sana na barabara.

Stend kubwa kama ile ilipaswa kuwa angalau 2 km nje ya barabara.
Uko sahihi..
 
Ajabu sana sana! Kila mtu ameufyata! Kama mtu mmoja ndiye aliyefanya haya ambayo hakuna wa kutetea wakati walituaminisha kwa takwimu basi hao watu hawafai kutumikia serikali yoyote.

Yapo maswali mengi sana ambayo CCM lazima wajibu na kuwajibika! Spika Ndugai hahitaji hata mjadala kwa aibu aliyobeba. Nafikiri JPM anaweza kuwa ameifikisha CCM pazuri kuwajibika kuliko wakati wowote!
 
Subiri kidogo, miradi yote tunayoiona itasimama, ndipo utajua tofauti kati ukweli na uongo. Kati ya Rais na mwimba taarabu.

Awamu zote za marais waislam nchi hii huyumba sana. Subiri tu ujionee.
Unaweza kuwa upo sahihi lakini kumbe unaendeshwa kwa chuki na udini.
Komenti zako zinaukakasi japo unachozungumza ni kile unachoamini.
 
Wapigaji wamerudi kwa kasi ili mambo yao yaende kazi ni moja kuua legacy yote ya mwendazake alafu waanze kupiga kama ilivyoada
Numbers don't lie....You can't eat the cake and have it.

Habari za usubuhi.
 
Umeandika kitu hapa, ninavyofahamu madudu ya ofisi za huko serikalini huwa yapo kila awamu, japo sasa tunaaminishwa yamezidi kwa awamu iliyopita, ningedhani pia kwa uelewa wangu wapinzani sasa waje na solution nini cha kufanya ili kuepuka hiyo situation mbele ya safari, badala yake naona wapinzani wameungana na lile kundi jingine la CCM kumshambulia mwendazake, hapa mwenye akili timamu lazima ujiulize, hawa wapinzani wa sampuli hii lengo lao ni nini hasa?

Wamejisahau wanamshangilia huyu mama tokea aingie ikulu, hata madudu yake yaliyotokea hivi karibuni bado hawajayaona, wao ni kushangilia tu kwa hali hii kwanini tusiendelee kutawaliwa na CCM miaka yote? hii ni kwasababu watu wameacha kufuata akili zao wanafuata za viongozi wao wa mitandaoni ndio maana.

CCM ni wale wale, kulindana kuko pale pale lakini watu wanashangilia tu kwa ufupi wa kumbukumbu zao, baada ya siku kadhaa akili zitawarudia waanze kulia tena, just a matter of time.
Wee acha upuuzi tatzo ww unaangalia hawa wapinzani wa mtandaoni ndo unadai wapinzani eti wanamshangilia Samia,Nani alikuambia wapinzani wanamshangilia Samia umetumia kigezo kuconlude et wapinzani wameungana na majiz ccm kumshangilia Samia,Tundu Lissu kila siku anampiga spana huyu Samia huoni?wapi umeona Mh Mbowe,Mnyika nk wanamsifia Rais Samia? Tofautisha wakina Mshana Jr, salary slip,Mmawia nk na chama cha upinzani
 
Tanzania viongozi ni majizi kuliko Nchi nyingi za Afrika Zuma anashinda mahakamani kwa pesa ambazo walioba Tanzania wapi nje harafu anatokea mwanakijiji anataka kupotosha report rasmi ya ukaguzi wa fedha nilichogundua pia Elimu zetu ni za hovyo mno mno kama unaona live Prof anaenda na ndege ya serikali kununua Novida huko na bado anaendelea kuwa kiongozi hawa wakina mwanakijiji wapo wengi siwashangai na sintokuja kuwashangaa ndio madhara ya mifumo mibovu ya Elimu kuanzia chini...
 
SGR, Rufiji Dam ni picha tu zile....[emoji1787]

CAG kaamua kishabiki kusema bila aibu akiwa na watendaji wale wale....akitaka kujikomba kwa mama kumbe anachotwa akili!

wa kujiuzulu sio PM tu hata Rais!!!!

Hakuna namna watamzima kirais JPM, he is here to stay with us for long long time
Ripoti za CAG zinaandaliwa muda mrefu, huu utani wa hadi kusema stendi ya Mbezi italeta foleni ni ukaguzi wa muda mrefu? Inawezekana yapo mengi sana ya kuhoji!

Lakini ajabu kuliko yote JPM alikuwa Rais, wako wapi wasaidizi wake watuambie walikuwa wanafanya kazi gani? Hii ripoti tunataka majibu ya kina ama kila mtu awajibike! Hatuwezi kuishi kwa propaganda na janja janja.
 
Ukisoma mitandao ya kijamii hasa twitter utafikiri kweli hii nchi imeibiwa kila kitu na hakuna kitu kimeachwa, kumbe sio kweli.

Watu wanajifanya kushangaa ATCL kupata hasara, hivi mtu mwenye akili timamu unaweza kushangaa atcl kupata hasara? By the way, ni shirika gani la serikali linalopata faida? Lipi? Mashirika yote ni hasara kila mwaka kuanzia Tanesco, TPDC, TTCL, ATCL, NHC na mengine yote, kwa nini shida iwe kwa ATCL?

Halafu watu wanataka kusema Magufuli ange eliminate rushwa ama wizi wa mali za umma 100%, hilo jambo halipo Duniani. Duniani kote, kuanzia China ambapo kosa la rushwa unaweza kuuwawa ama Marekani ambapo mifumo iko strong bado watu wanaiba na kula rushwa, tusimsingizie Magufuli kwa kila kitu.

Kuna kikundi ama kingenge cha wahuni sijui kinalipwa na nani kutaka kumchafua Magufuli na report ya cag
Ama kweli!!! Leo mnahalalisha wizi kuwa ni kawaida duniani kote!!
 
Back
Top Bottom