Kama Kocha Mzawa mwenye Akili Tanzania nzima Mecky Mexime Kaichambua Simba SC vizuri hivi Wewe ni Kibushuti gani umpinge?

Kama Kocha Mzawa mwenye Akili Tanzania nzima Mecky Mexime Kaichambua Simba SC vizuri hivi Wewe ni Kibushuti gani umpinge?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
"Nilishatabiri mapema tu kuwa Simba SC inacheza Fainali ya Shirikisho. Na hata hiyo Jumapili nakuhakikishia Simba SC anaenda Kumfunga Orlando Pirates FC na kwenda Nusu Fainali ya Shirikisho. Simba SC ina Wachezaji wakubwa, wazuri, wanaofika na wanaweza Kukimbizana.

"Nimewaona Orlando Pirates FC ni wepesi mno na nilimshangaa sana yule Kocha wao akilalamika wakati Mimi kama Kocha ile Penati ya Simba SC ilikuwa ni ya halali kabisa.

"Kitu pekee tu ambacho nawaonya Simba SC ni kuwa makini mipira ya Set Pieces na Kona kwani kwa maeneo haya wako vizuri ila Kwingineko ni wa Kawaida na kama Wachezaji wa Simba SC wakijitambua, wakicheza maradufu na walivyocheza Kwa Mkapa nakuhakikishia Simba SC anavuka na kuingia Nusu Fainali na sina Shaka katika hili," amesema Kocha Makini, Mwerevu na Fundi wa Mpira Tanzania nzima na Kocha Mkuu wa Cambiasso Sports Academy Mecky Maxime.

Taarifa: Sports Extra Clouds FM leo.
 
Sidhani Kama mexime ameongea maneno mengine ninayoyaona apo Kama ''Simba lazima icheze nusu fainali" "Simba Ina wachezaji wakubwa wanaokimbizana" "Orlando ni wepesi sana" Nafikiri kuna maneno umemlisha sababu kwa mtu mwenye akili timamu awezi akasimama akasema orlando ni wepesi, eti simba lazima acheze fainali usilishe watu maneno wewe acha upuuzi wako
 
Ni kweli lkn amesema endapo wachezaji watacheza maradufu zaidi ya walivyocheza hapa!!!so wachezaji wa makolo fc wanabidi wapambane jasho na damu ili kuwatoa maharamia wa orlando pale soweto
 
Ni maoni yake, na kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake. Inawezekana ameamua kuyaongea hayo ili kuwapa morali wachezaji kuona inawezekana kupata matokeo huko huko kwao. Lakini kiuhalisia timu ambayo inacheza kwa Mkapa halafu wanaruhusu goli moja tu, maaana hiyo timu sio nyepesi wako vizuri kwenye ufundi na mbinu. Huu ndio uwanja ambao Simba imewavunisha magoli mengi mno. Kwanzia msimu wa 2019. Timu ambazo zimeweza kuzuia kipigo cha mbwa mwizi zina hesabika.
 
Haiwezi fika fainali na wala haiwezi pita hii atua waliofikia labda wakiacha kununua mechi za Ligi kuu
Timu bado inawanunua mechi za Geita gold,Biashara United Pamba
 
Angetoa maoni tofauti na hayo angeitwa shoga siku hizi ukiwa na maoni tofauti unaitwa shoga , amejua kucheza na akili zao
 
Mexime alifukuzwa Kagera sugar baada ya kutaka kuishusha, haaminiki
 
Katafutatafuta maneno hahahaaaa
Ningewaona mna Akili kama nanyi ambayo mnamdhihaki na kujifanya mnajua Kiingereza haya Maelezo yenu yasingekuwa kwa Kiswahili hiki kama ambavyo mnakiandika. Mmejaa Chuki, Wivu, Uswahili na Upumbavu utokanao na Umasikini wenu na Stress za Maisha magumu yanayowakabili.

Cc: Arovera
 
dah yaani tanzania nzima kocha mwenye akili ni huyo mtajwa ? hahahahaha
 
Badala ya kuwashauri kwenye technique capacity mnawasifia ati wako vizuri...ngoja wapokee kichapo cha mbwa koko ndiyo mtajua hamjui.
Kwani Wenye Akili Wameongezeka Hapo Yanga Zaidi ya Wawili?
 
Back
Top Bottom