Hii dunia karibia kila mtu ana matatizo makubwa tu,wewe huna ajira wakati kuna boss bank wanauza mali zake kwa kushindwa kulipa mkopo. Wewe huna ajira kuna binti kama wewe yuko ocean road anapambana na cancer ya ziwa na kwao wana uwezo mkubwa tu .
We all suffer in this life na njia bora ya ku-cope sometimes ni kuweka changamoto zako kwenye mzani na kuzifananisha na wengine. Utagundua zako ni Cakewalk kabisa . Wewe bado ni kijana,sio single mama uliesusiwa mtoto/watoto,afya yako ipo njema kabisa,sio yatima,umesoma mpaka chuo kikuu nk. Kwenye maisha yako kuna positives nyingi sana kuliko vimeo, mshukuru Mungu for what he has given you.
Kwenye maisha haya kumbuka kwamba mtaji namba moja ni Mungu,namba 2 ni afya. Ukiwa navyo hivi basi possibilities ni endless. Endelea kumuomba Mungu wako akujalie yale unayo hahitaji,na ukimuomba yeye basi mwachie atende. Usiombe halafu ukaendelea kuyabeba moyoni,Mungu hawezi kukutua mzigo ambao wewe hautaki kusaidiwa kuubeba .
Kama upo Dar au mji wowote jitahidi kutembelea wagonjwa mahospitalini kuanzia wodi za watoto mpaka watu wazima . Itakufungua macho uone jinsi gani umebarikiwa dada,kama ni mkristo basi usiache kukumbuka lile neno la shukuruni kwa kila jambo.
Mwisho kabisa unaweza jaribu kujisafisha kwa chumvi ya mawe (ogea) hata siku 30 huku ukinuia kuondoa negative energy,vifungo vya kichawi nk. Kila la heri 🥂.