Pole sana dada yangu kwa unayopitia lakini si mpango wa Mungu.
Mimi ninaona una shida ya koroho zaidi na unahitaji msaada wa kiroho.
Kuna watu wana maagano na shietani huku duniani kuharibu watu na kizazi. Huyo mme wa mtu aliyekuharibia usichana wako hapo ndipo matatizo yalianzia na wewe hapo ndipo ulipokosea na inawezekana kabisa alitumia nguvu za giza kukupata bila wewe kuwa na habari. Na hii ni baada ya wewe kutotulia kwa Mungu. Inawezekana huyu mtu amekuwa spiritual husband wako na amekufunga na kila mwanamme utakayempata anaweza kufa au kukuacha bila sababu yoyote na pia usiweze kufanikiwa. Hayo tumeyaona. Baada ya kukuta wewe bikira basi katika ulimwengu wa roho anaweza kuwa amekufunga kabisa na anataka uwe mke wake na inawzekana wewe ni mke wake bila wewe kujua.
Cha kufanya na ushauri wangu ni huu.
Tafuta mtumishi wa Mungu anayeeleweka au kanisa linaloeleweka linalohubiri injili ya kweli ya wokovu ambayo ni kumpokea Yesu Kristo awe Bwana na mwokozi wa maisha yako. Soma Warumi 10:9-12 "Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao . Baada ya hapo utaombewa delverence ili uweze kufunguliwa katika vifungo ulivyo navyo. Yesu alikuja kuwaokoa wenye dhambi. Soma Matayo 11:28. " Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. Pia soma Yohana 10:10 "Mwivi (shetani) haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi (Yesu) nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele".
Mungu alimtuma mwanaye Yesu ili kutuondolea vifungo ambavyo shetani ametufunga tusifanikiwe. Ukimtafuta na ukimwamini hakika utafunguliwa tu. Wengi wamefunguliwa kwa jina hili la Yesu lipitalo majina yote na maisha yao yamebadilika sana.