Kama Kuna msaada wa kiimani ama kisaikolojia naomba tafadhari kabla sijachanganyikiwa

Nampendamilele Soma hapa tena na tena na tena na tena na tena. Kuna neno la msaada. Fanyia kazi Uendelee na Safari ya utafutaji
 
Dhambi ya mauaji (abortion) inakutafuna, na ikumbukwe kuwa mwenye kiumbe alikubali na alikuwa na future na wewe, tamaa za maisha mazuri ya bila jasho zinakuangusha katika dhambi ya uzinifu, mrudie Mungu wako kabla ya umauti kukufika
 
njoo dm tushauriane kwanza pole sana kwa yaliyo kukuta hapo chamsingi omba toba kingine usijihisi unagundu wekazana kumuomba MUNGU ,ILI ufanikiwe lazima utake risk uhame mbali na hapo ulikozoeleka vinginevyo mda utaenda huna la maana na wazazi macho yote kwako maana wanaona mtu akisoma tayari ashatoboa maisha,anza kuuza hata mihogo ,uji n.k
 
Wanawake mkiwa kwenye peak ya raha kuna tabia mbovu mnakua nazo na vilevile mkiwa na shida mnakua na tabia mbofu ambazo inakua ngumu kusaidika labda kwa mtu anaeelewa hali kama hiyo..

Kwa story nyingi kama yako, ninyi hata mkipata mtu na huyo mtu akakupenda mnaanza kuleta usumbufu wa ndoa ndoa na kufatiliana na wivu wa kipumbavu mwisho unakimbiwa...

Mkipata kazi bado mnakua na kisirani, majibu yenu kwa wateja/waajiri/wafanyakazi wenzenu yanakua ya hovyo mwisho mnaishia pabaya tena.

Kama ni kuharibu maisha basi mara nyingi maamuzi yetu ndio yanatuharibia, maisha uliyopitia ni ya kawaida kwa wanawake wengi tu.
Usijitahidi kulaumu watu kwa matatizo yako, jitahidi kujua makosa yako kwanza na uyakubali.

Achana kwanza na mawazo ya kulogwa sijui nuksi, kwa story ni wewe na maamuzi yako tu hamna uchawi hapo.
 
Wakati ulikuwa na unatoka na Mume wa mtu,ulikuwa na mchumba,at the same time ukabeba mimba ya kijana mwingine.
Wanawake.
Halafu anasema kalogwa, na katoa mimba pia.

Ni maamuzi yake ndo yana tatizo, ajitahidi kufikiri kabla ya kutenda.

Afocus na maisha yake na sio kuolewa. Akiwa na chake atanawiri na wanaume atawapata tu.

Atateseka sana ikiwa atakua mtaka ndoa ndoa ndoa.
 
Wewe ni mtoto wa kanisani vivyo hivyo mafanikio yako yako kanisani.
 
Una shahada gani?
 
Nakushauri umrudie Mungu wako tubu na uokoke kweli kweli na kumbe ulikuwa mlokole mzuri nakupongeza usijaribu kuacha kwenda kanisani maana watakumalizia endelea kwenda kanisani
 
Huyo mama yako na hao ambao hawakuwa upande wako wakashinikiza hadi ukafanya abortion ndio shida ilipoanzia, na watu kama hao ndio wanasababisha walokole waonekane ni wanafki, matendo yenu na ulokole ni vitu viwili tofauti kabisa.

Binafsi naona ndio chanzo cha hayo yote yanayoendelea kwako na yataendelea kukugharimu mpaka pale utakapoomba toba ya kweli.

Huwezi kufurahi kwa kuumiza watu wengine, hujui ni maumivu gani aliyapitia huyo mwanaume aliekupa mimba ukaitoa, bado kuna nafsi ya kiumbe ulichokizulumu haki ya kuishi, kwa namna hiyo unadhani itakuwa rahisi kupata kila unachokitaka/kipenda na kikadumu?
Natamani niandike zaidi ila ngoja niishie hapa ila kumbuka kutubu na ikiwezekana mtafute yule ulietoa mimba yake na umuombe msamaha kwa sababu hakukataa. Pole sana mkuu
 
Kila mtu ana historia yake, ukisikia ya mwingine utajiona wewe ni malaika relax.
 
Hii dunia karibia kila mtu ana matatizo makubwa tu,wewe huna ajira wakati kuna boss bank wanauza mali zake kwa kushindwa kulipa mkopo. Wewe huna ajira kuna binti kama wewe yuko ocean road anapambana na cancer ya ziwa na kwao wana uwezo mkubwa tu .

We all suffer in this life na njia bora ya ku-cope sometimes ni kuweka changamoto zako kwenye mzani na kuzifananisha na wengine. Utagundua zako ni Cakewalk kabisa . Wewe bado ni kijana,sio single mama uliesusiwa mtoto/watoto,afya yako ipo njema kabisa,sio yatima,umesoma mpaka chuo kikuu nk. Kwenye maisha yako kuna positives nyingi sana kuliko vimeo, mshukuru Mungu for what he has given you.

Kwenye maisha haya kumbuka kwamba mtaji namba moja ni Mungu,namba 2 ni afya. Ukiwa navyo hivi basi possibilities ni endless. Endelea kumuomba Mungu wako akujalie yale unayo hahitaji,na ukimuomba yeye basi mwachie atende. Usiombe halafu ukaendelea kuyabeba moyoni,Mungu hawezi kukutua mzigo ambao wewe hautaki kusaidiwa kuubeba .

Kama upo Dar au mji wowote jitahidi kutembelea wagonjwa mahospitalini kuanzia wodi za watoto mpaka watu wazima . Itakufungua macho uone jinsi gani umebarikiwa dada,kama ni mkristo basi usiache kukumbuka lile neno la shukuruni kwa kila jambo.

Mwisho kabisa unaweza jaribu kujisafisha kwa chumvi ya mawe (ogea) hata siku 30 huku ukinuia kuondoa negative energy,vifungo vya kichawi nk. Kila la heri 🥂.
 
Solution yako imejificha hapa chini

A. Mchungaji muadilifu
B. Ostadh muadilifu
C. Mganga machachali😋
D. Ujitie ujuaji tatzo lizidi kuwa kubwa.... Maana kwa huo umri wako na tumebakiza mwak mmoja uwe na 26🤔🤐

Fanya chaguo sahihi kulingana na utashi wako tukupe namba,

Note: wanawake hamkawii kuzeeka, fanya juu chin 27 isikukute hvyo🚶🚶
 
Kwani ulisomea nini chuo?
 
Nampendamilele

Kwanza pole sana.

Pili, endelea kuufundisha moyo wako kuzoea nyakati ngumu na nzuri.. mara nyingi nyakati nzuri hazidumu.

Tatu; Nenda kanisani, tafuta kanisa wanako Sali kwa utulivu bila naguvu. Muombe mola kimya kimya. Hii mambo ya kwenda kuombewa upate mme yataendelea Kulipa sononona, maana waombezi no wengi kuliko majibu.

Nne.. badili makazi, Anza upya kwa umakini zaidi. Omba mzazi akupe support ukajitafute. Usiogope.. ukifeli utarudi nyumbani. Kutembea ni kizuri.
 
You need a powerful medicine called PRAYERS it will cure you and give you a good and new beginnings with happiness and prosperity
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…