Kama Kuna msaada wa kiimani ama kisaikolojia naomba tafadhari kabla sijachanganyikiwa

Asilimia 80 ya jf members ni majobless so mkuu usiwaze haupo peke yako ni vyenye hatusemi endelea kukaza.
 
Pole kwa hayo yaliyokuta!
Jambo la Kwanza usikate Tamaa wakati Mungu yupo! Mungu hajakutupa kwa namna yo yote hata kama umefanya dhambi ya uasherati hata kutoa mimba! Shetani asikudanganye kwamba Mungu amekuacha! Mpinge na kumkataa kabisa.Rudi mbele za BWANA mwambie umekosa! Yeye bila shaka atakusamehe,(Isaya1:18) na (ufunuo2:15)
2.Pili,usiweke matumaini yako kwa wanadamu kuwa ukiolewa ndiyo utakuwa umetoka kimaisha! Kwa kizazi hiki hakuna ndoa za maana,ndoa za sasa hivi ni za kuoana leo kesho zinavunjika.
Mwachie Mungu akuongoze kumpata mme bora. Usitumie akili zako kutafuta Mme.
Tatu,usiweke mawazo yote kwenye Ajira za kuajiriwa kiasi cha Shetani kukufanya usitafakari milango mingine ya kutafuta fedha! Ndiyo kusema usione haya kwa sababu ya Usomi kufanya kazi hata za kuuza Mchicha,maandazi au nini!
Nne,Usisikilize maneno ya Shetani kuwa sijui una nuksi,sijui ulitamkiwa maneno mabaya na watu,sijui una mikosi,nk ukiona hivyo Shetani anapanga kukuelekeza kwa Waganga wa Kienyeji na kule atakumalizia kabisa!
HUJACHELEWA BADO!
 
katika yote uliyoandika sijaona mpango kazi wa kuwekana sawa na Mungu wako, yeye ni chanzo cha kila kitu kwako, he can restore anything you lost, tafuta ibada, shiriki ibada, fanya maombi, jichanganye na waliofanikiwa, kama upo dar......twende kwa Pastor Tony ijumaa kwa mkesha.
utanielewa badae
 
Naweza kukusaidia kulipa kisasi kwa huyo mamako wa kambo kwa manyanyaso uliyopitia. Atakufa kifo cha kawaida tu hakuna atakaye jua wala kukuhisi vibaya. Kama upo serious nicheki

Aisee hata dunia ivae sket siwezi kulipiza kisasi kwa mtu yoyote unajua ni kwanini, Mungu ndie anaenilipizia kisasi yule mama alikuwa hataki Mimi nisome kabisa ilikuwa hadi anachoma nguo na madaftari ya shule naweza kaa miezi 6 sijaenda shule,, unaona Mungu alivyo mkuu sana mimi nimesoma kuliko watoto wake….

So achana na maswala ya kuua Watu Sina hilo wazo wala simlaani kwa chochote isitoshe mzee wangu alichangia hapo… kama alishindwa kumdhibiti mke wake juu ya matendo yake basi wa kulaumiwa ni yeye
 
Kuweni na busara jmn tusijazane imani potofu.. Kuna mtu Kaniambia Mimi ndio nimemuua mchumba angu kwasababu nina jini mahaba… naomba mniambie hapa dalili za mtu mwenye jini mahaba… maana mimi hata mambo ya ngono sio kipaumbele kwangu naweza date na nisiitaji sex wala sijawahi kuota ndoto za mapenzi… huo unabii nimeukataa
 
Hujarogwa bali umejawa na woga, wasiwasi na kukata tamaa...

Kazi si lazima kuajiriwa, unaweza kujiajiri pia...

Maisha yako yasiendeshwe na maneno ya watu bali ishi ukitimiza ndoto zako, naona umeanza kumention mtu ambaye pengine hata yeye ana matatizo kukuzidi...

Achana na habari za mahusiano kwa sasa hadi utapoimarika kiuchumi na kifikra, kumbuka una makovu kwenye mahusiano tayari...

Mwisho, rejelea ibada na ufanye toba...
 
Uko mkoa gani kwanza, tuanzie hapo.

Halafu unaonekana kichwa chako kiko resi sana, yani it seems haujasettle kabisa kiakili.

Ndiyo maana hata kazini unafukuzwa bila mpangilio, hiyo yote ni kwa sababu wanakuona hauko sawa, yani mtu akikutazama anaona kabisa something somewhere is wrong with you..
 
Wewe si umetoa mimba umeua mtoto? Sasa unavyoambiwa ni laana unabisha nini? Unasema sex siyo kipaumbele chako nahuku umesimulia hapo kuwa ulikuwa na wanaume watatu, mmoja kujuana nae siku ya graduation akakulala siku hiyo hiyo? Unapewa ushauri uwaone wachungaji wakuombee unakaza kichwa, sasa Baki hapo hapo.
 

Umeelewa nilichoandika au unaweka makasiriko tu.. Laana nani amenipa?? Kama wazazi wangu hawezi kunipa laana.. Mungu nae ana mambo mengi ya kufanyaa hatoitoi laana kwa mwanadamu… nyie manabii wauongo mje mniambie nina laana ili mninunulishe mafuta ya upako na michango ya sadaka… shindwaa Hakuna laana katika maisha yangu wala kizazi changu
 
Asante kwa kushiriki hadithi yako kwa uwazi na uaminifu. Maisha yako yamekuwa na changamoto nyingi, na ni kawaida kuhisi kuchanganyikiwa au hata kuamini kuwa unakumbwa na laana au karma kutokana na matukio ya nyuma. Hata hivyo, nataka nikupe mtazamo wa uhalisia na kukusaidia kuelewa kuwa bado kuna tumaini na nafasi ya kubadilisha maisha yako.

Kuhusu Maisha Yako ya Zamani

1. Uhusiano na Mama Yako: Ni kweli mama yako alifanya maamuzi ambayo kwa wakati huo yalionekana sahihi kwake, hata kama hayakuwa mazuri kwako. Hata hivyo, kumbuka kuwa wazazi pia ni binadamu na wana mapungufu yao. Inaweza kusaidia kujaribu kumsamehe na kuelekeza nguvu zako katika kujenga maisha yako.


2. Mimba na Abortion: Hisia zako za hatia ni za kawaida, hasa kama unajiona kuwa ulifanya kosa. Lakini maisha ni safari ya kujifunza, na hakuna mtu asiyekosea. Mwanaume aliyekupenda alikuwepo kwa wakati huo na alikusaidia kwa namna yake. Jikubali kuwa ulimfanya uamuzi huo kwa mazingira ya wakati huo.

Kuhusu Hali Yako ya Sasa

1. Kazi na Mahusiano:

Maisha yana vipindi vya kupanda na kushuka. Kukosa kazi au kuona mahusiano hayafanikiwi mara moja haina maana kwamba umeandikiwa maisha ya kutofanikiwa.

Inaweza kuwa kuna maeneo unahitaji kuboresha, kama vile ujuzi mpya wa kazi, kujituma zaidi au hata kujaribu sekta tofauti za kazi. Pia, mahusiano mazuri huja kwa wakati sahihi; usijilaumu.

Jihadhari na maneno hasi ya wengine. Mara nyingi watu huonyesha udhaifu wao kwa kukukosoa.

2. Maneno ya Mama au Wengine:

Si kweli kwamba laana au maneno mabaya ya mtu mwingine yanaweza kukufanya ushindwe maisha. Unaweza kuvunja mzunguko huu wa mawazo kwa kujikubali na kuendelea mbele.

Jaribu kumsamehe mama yako kwa semi zake; anaweza asiwe anamaanisha mabaya lakini anahofia kuhusu hali yako.

3. Kijana Anayeonekana Kukuvutia:

Ikiwa kweli unahisi kuna hisia kwa upande wako, zungumza naye kwa upole na uelezee unavyohisi. Usikubali kubaki kwenye hali ya kutokujua, kwani hilo linaweza kukwaza zaidi kisaikolojia.
Hatua za Kuchukua

1. Kibinafsi:

Tafuta msaada wa kiroho kutoka kwa mshauri wa kiroho au hata kasisi ikiwa uko tayari kurudi kanisani. Maombi yanaweza kusaidia kupunguza mzigo wa kihisia.

Tafuta njia za kujitunza: Fanya mazoezi, soma vitabu vya kujijenga kisaikolojia, na tafuta watu wanaoleta amani kwako.

2. Kazi:

Hakikisha wasifu wako uko vizuri, na jaribu kujifunza ujuzi mpya unaoendana na mahitaji ya soko. Tafuta mashirika au watu wanaoweza kukusaidia kuimarika kitaaluma.

Endelea kuomba kazi na kuwa tayari kwa kazi yoyote halali inayojitokeza. Matokeo yanahitaji uvumilivu.
3. Kisaikolojia:
Mtafute mshauri wa kisaikolojia ikiwa una nafasi. Mtu wa taaluma hiyo anaweza kukusaidia kushughulikia hisia za hatia, huzuni, na kukosa mwelekeo.

Kuwa na shukrani kwa hatua ndogo unazopiga kila siku. Shukrani hufungua milango ya baraka zaidi

Mwisho

Haya ni maisha yako, na bado una nafasi kubwa ya kuyabadilisha. Changamoto na maumivu ya nyuma hayapaswi kuwa kifungo cha maisha yako ya baadaye. Tafuta msaada kwa watu unaowaamini na uamini kuwa maisha yanaweza kuwa mazuri tena. Naamini kuwa unaweza kufanikisha hili.
 
Huu ni ushauri mzuri sana. Mungu akubariki.
 
Acha ubishi, soma kutoka sura ya 20 mstari wa 5, kama wazazi wako walifanya makosa, laana inahamia hadi kizazi Cha nne, na hiyo laana ya kuua mtoto asiye na hatia, itaendelea kutafuna mpaka vitukuu vyako, unaua mtoto halafu utegemee Mungu akuache hivi hivi? halafu Mimi siyo nabii, na siyo lazima ufuate ushauri wangu, kama hutaki kutibu na kumrudia Mungu, akili zako zitakupeleka kwa waganga, huko ndo utaongeza laana zingine kwasababu ni madhabahu iliyo kinyume.

Watu wanakuuliza umesomea nini ili wakupe connection za kazi husemi, wanakuuliza unaishi mkoa gani wakuelekeze hata kwa wataalamu wa saikolojia husemi, na heading yako inaeleza inahitaji msaada wa kiroho au wa saikolojia, unapewa msaada unakaza kichwa.
 
Kama Kuna mtu ana ushauri wa kiroho na wa kimwili anipe hapa nitoke kwenye hiki kifungo
Nimejaribu kuelezea story ya nyuma ili mwenye kutoa ushaurii aweze ku relate hizo dots maybe kuna sehemu nilipolegeza nikaanguka
Nina cousin wangu ana same scenario,
Ana akili sana nakumbuka yy ndo alikuwa anatufundisha hesabu tukiwa O-level yaani anakusanya group of 10-20 people anatufubdisha. O level nakumbuka alipiga Div 1 ya point 9 hv, 4rm6 akachaguliwa Mazengo by then, kbl ya kwenda Mazengo ile likizo ya kusubiri matokeo ya 4rm4 aliokoka kbs akiwa home coz muda mwingi alikuwa analelewa kwetu so alifuata maneno mazuri ya kuokoka kutoka kwa wazazi wangu, mm niliwaambia washua kuwa naomba nisiokoe kwa kufuata mkumbo, Mungu atanipa njia yale hii atakapoona imefaa... mwenzangu akaokoka akawa anapendwa sn na washua mm nikawa kama kikwazo hawanifagilii kivileeee, lkn ndo hvy watafanyeje ndo mwanao....siku za kwenda mazengo zikafika cousin akaenda Dodoma kwa ajili ya kuanza shule Mazengo, hiyo siku ilikuwa J1 so alipitia kwa Auntie area C kwa ajili ya kuvuta punzi kesho yake aelekee shule.

Jamaa katika check check akafungua friji akakutana na tusker bariiiiid, Shetani akamshinda nguvu akavuta tusker akigida ulokole wake ukaishia hapo (akamkana Mungu wake)

Amesoma vzr kbs lkn wakati wanajiandaa na mtihani wa 4rm6 akawa kama anapata wenge yaani anasema akiingia darasani anasikia harufu isiyovumilika na anachukia kukaa darasani.

Siku 2 kbl ya mtihani akapotea, alikuja kupatikana wiki mbili wakat mtihani ukiwa tayar umekwisha hvyo hakufanya mtihani. Kutoka hapo maisha ya cousin yakaharibika kbs hadi ninapozungumza hivi jamaa ni mtu wa kufundisha vi-tuition hv na shule ambapo anafundisha kwa siku chache wakitaka cheti ndo wanakuwa wamemfukuza coz hana doc reliable ambayo inaweza kumbeba.

Ninachotaka kukueleza ni kwamba, ulimjaribu Mungu wako, ukawa upande wake ghafla ukamdhihaki same as my cousin, jambo pekee ambalo unaeza fanya sasa ni kumrejea Mungu na kusali sana kwa maana ya kurejea Mungu katika maana halisi. Hy nduo njia pekee naamini mtarejea kukaa sawa.

Lkn pia itasaidia kama kuna yyt aliyepo katikati. (Adui wa mtu ni mtu)
 
Naweza kukusaidia kulipa kisasi kwa huyo mamako wa kambo kwa manyanyaso uliyopitia. Atakufa kifo cha kawaida tu hakuna atakaye jua wala kukuhisi vibaya. Kama upo serious nicheki
Khaa aisee jaman tumefikia huku?
 
Umeshauri vizuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…