Kama Kuna msaada wa kiimani ama kisaikolojia naomba tafadhari kabla sijachanganyikiwa

Matatizo yanaanzia kwenye Abortion.

Hilo jambo usilione dogo... Ni kubwa sana.
Ndo tunamwambia ila anajaza kichwa, na Mungu anasamehe hata waliotoa mimba tano sembuse yeye mimba moja? Tatizo anajiona hafai kabisa nahuku ana nafasi ya kusamehewa na Mungu, basi we mwache aende kwa waganga ma wachawi
 
Hauhitaji ushauri wa kiroho,na wala huna mkosi wowote na wala hujarogwa,ila ni mentality yako inahitaji paradign shift,amua wewe mwenyewe nini cha kufanya na amua mwenyewe ni mume yupi unayemtaka ndipo umtafute wala haitachukua mwezi utampata mchumba
 
Ndo tunamwambia ila anajaza kichwa, na Mungu anasamehe hata waliotoa mimba tano sembuse yeye mimba moja? Tatizo anajiona hafai kabisa nahuku ana nafasi ya kusamehewa na Mungu, basi we mwache aende kwa waganga ma wachawi

Toba ni ya aina gani nifanye… maana ilo jambo nilishalifanyia toba Mbele za Mungu tena kwa maombi ya kufunga wiki nzima na naendelea kuomba toba kila napopata muda wa kuomba…
 
Tuliza akili, fikiria kuhusu uhusiano na watu wanaokuzunguka ujue nini ufanye nann usifanye, nini uongee na nini usiongee. Usijipe laana za kufikirika, jifunze kuwa mtu wa kawaida kama watu wengine zungumza Kwa kujiamini, usimpe mtu mwanya wa kumfanya abashiri maovu yako uliyoyafanya kwani itakupotezea mvuto. Kumbuka kila mtu ana maovu yake ila tofauti yako na wengine ni kwamba wewe huwez kuficha guilty. Kuna wengine ma shoga, wachawi, wauwaji, majambazi lakini hawapungukiwi na bahati nzuri na fursa tamu tamu. Jifunze ukomavu, haujarogwa Wala hauna laana
 
Mkakutana siku moja, akakutongoza siku moja, akakushenyenta siku moja, ukabeba mimba siku hiyo hiyo moja, ukaitoa hiyo hiyo mimba moja... Sijui nataka niseme nini?
Basi sawa.
 
Pole sana dada yangu kwa unayopitia lakini si mpango wa Mungu.

Mimi ninaona una shida ya koroho zaidi na unahitaji msaada wa kiroho.
Kuna watu wana maagano na shietani huku duniani kuharibu watu na kizazi. Huyo mme wa mtu aliyekuharibia usichana wako hapo ndipo matatizo yalianzia na wewe hapo ndipo ulipokosea na inawezekana kabisa alitumia nguvu za giza kukupata bila wewe kuwa na habari. Na hii ni baada ya wewe kutotulia kwa Mungu. Inawezekana huyu mtu amekuwa spiritual husband wako na amekufunga na kila mwanamme utakayempata anaweza kufa au kukuacha bila sababu yoyote na pia usiweze kufanikiwa. Hayo tumeyaona. Baada ya kukuta wewe bikira basi katika ulimwengu wa roho anaweza kuwa amekufunga kabisa na anataka uwe mke wake na inawzekana wewe ni mke wake bila wewe kujua.

Cha kufanya na ushauri wangu ni huu.
Tafuta mtumishi wa Mungu anayeeleweka au kanisa linaloeleweka linalohubiri injili ya kweli ya wokovu ambayo ni kumpokea Yesu Kristo awe Bwana na mwokozi wa maisha yako. Soma Warumi 10:9-12 "Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao . Baada ya hapo utaombewa delverence ili uweze kufunguliwa katika vifungo ulivyo navyo. Yesu alikuja kuwaokoa wenye dhambi. Soma Matayo 11:28. " Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. Pia soma Yohana 10:10 "Mwivi (shetani) haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi (Yesu) nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele".
Mungu alimtuma mwanaye Yesu ili kutuondolea vifungo ambavyo shetani ametufunga tusifanikiwe. Ukimtafuta na ukimwamini hakika utafunguliwa tu. Wengi wamefunguliwa kwa jina hili la Yesu lipitalo majina yote na maisha yao yamebadilika sana.
 
Toba ni ya aina gani nifanye… maana ilo jambo nilishalifanyia toba Mbele za Mungu tena kwa maombi ya kufunga wiki nzima na naendelea kuomba toba kila napopata muda wa kuomba…
Basi msaada wa kisaikolojia ndo utakufaa
 
Mkakutana siku moja, akakutongoza siku moja, akakushenyenta siku moja, ukabeba mimba siku hiyo hiyo moja, ukaitoa hiyo hiyo mimba moja... Sijui nataka niseme nini?
Basi sawa.

Duuh umetulia ukasoma kweli nimesema nilijuana nae ndani ya wiki moja na mimba ni baada ya wiki Tatu … tuliza kichwa
 
Dada pole sana ....najaribu kuwa kwenye kiatu chako ....ila pole tu hapo kwenye kukataliwa kazi sijui kusimamishwa utakuwa umetupiwa ka kitu au umepuliziwa muone sheikh au unetupiwa roho ya kukataliwa tyr
 
Una negative energy nyingi sana umezikumbatia. Focus kwenye mazuri yaliyowahi kutokea kwenye maisha yako na yaliyo mbele yako. Kilichopita kimepita huwezi kubadilisha. Ila kilocho mbele yako ndicho unaweza kukibadilisha. Kaa humo.
 
Mlokole kweli wewe, mara uwe wa kiume mara uwe binti wa miaka 25.

Hauko siriaz
 
Uko tayari nikupeleje kwa bibi yangu Runzewe akajupige chale
 
Umeua, the reactive force will devastate you and kill all your endeavors. Accept the consequences.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…