yaani ccm wamefanya tuone kila kitu kinawezekana,kwa ccm mzamivu wa afya anakwenda kusimamia kilimo na mambo yanaharibika hatujui tatizo liko wapi.
upelelezi wa makosa ya jinai,ndio upelelezi wa msingi zaidi kuliko upelelezi mwingine,
ni kama kusema mpelelezi wa makosa ya jinai,anaweza fanya kazi yoyote ya inayohusu kada hiyo,lakini si mpelelezi wa kijeshi kufanya upelelezi wa kiraia,itamlazimu kurudi darasani upya,achia mbali kuwa boss wao.
aina ya upelelezi wa kijeshi(MI)na ule wa idara kama usalama wa taifa,unalenga kuhujumu adui na mshindani wako zaidi,na si kutafuta haki ya mtu mwingine ama ushahidi wa kuwasilisha sehemu nyingine.
kule USA aina hiyo ya upelelezi iko mikononi mwa CIA,lakini upelelezi wa jinai na mambo ya ushahidi uko mikononi mwa FBI na CIDs.
kwa hapa bongo hilo linawezekana kabisa,halafu tutaendelea kufunga novena ili kupokea ufanisi ushuke kama upako.