Kama kuna yeyote anaeweza kunipa faida za kutokuoa au kutokuolewa ajitokeze

Kama kuna yeyote anaeweza kunipa faida za kutokuoa au kutokuolewa ajitokeze

Kutooa Faida yake nyingine ni Ubinafsi.

Mali ulizochuma ni zako tena hata mkiachana hamna haja ya kugawana.

Freedom unaweza fanya chochote

Hasara za kutooa/kuolewa.

Sometimes wengine hawafanikiwi mpk waoe. Ndoa sometimes ni baraka na inaleta mafanikio.
Vilevile ndoa sometimes inaleta mikosi
 
Kwa lugha nyingine unatafuta hasara za kuoa na kuolewa....
 
Hoja nimeshaipinga tayari, sababu kiuhalisia hakuongelea juu ya faida bali mtazamo wake katika upande mmoja, hali ya kuwa si sahihi na akili inakataa.
Huo mtazamo wake alouongelea ni kuhusu nini?
 
Mbona nyingi tu...

Inamaanisha unajua faida za kuoa/kuolewa, sasa kinyume chake ndo faida za kutooa/kutoolewa
 
Maisha ni kuchagua,Mimi napenda kuishi maisha huru,nahis nisipooa nitaishi kwa amani sana na kwa starehe,Kuna zile unakutana na manzi mzuriiiiiiiiiiiiii afu anakushobokea mwenyew,ukiwa hujaoa unapitia fasta ila ukiwa umeoa unaanza kumuwazia mkeo,mi kuoa mpaka niwe na miaka 45
 
Ombi langu toka kwako ni kuwa naomba unipe faida za kuto kuoa na kutokuolewa.
Faida za ndoa nikikupa Kama una mwenza pasua kichwa hazina umuhimu zaidi utaona ni Mambo ya kufikirika.
 
Faida za ndoa nikikupa Kama una mwenza pasua kichwa hazina umuhimu zaidi utaona ni Mambo ya kufikirika.
Haya ni matokeo kama yalivyo matokeo mengine, ila ndoa haina hasara zaidi ya faida.

Ama kuhusu kutokuoa ay kuolewa hakuna faida abadani kuanzia mwanzo wake kati yake mpaka mwisho wake.

Ndiyo maana sisi Wislamu mkishindwana ule mlango wa dharura (Talaka) unatumika,lengo na shabaha ni kupata faida tu.
 
Hakika ni maumivu kila kukicha
Kwanini ? Mbona wake zangu wana furahia sana kuolewa na mimi ?

Itakuwa basi wake zangu ni watu wa ajabu sababu wanamvumilia Zurri. Leo nawapelekea zawadi ya hongera.
 
kuoa kunaweza kupelekea mahusiano yako na rafiki zako wa jinsiia tofauti kuwa na risk, watu waliooa au kuolewa kwa asilimia kubwa wame-loose interest katika maisha ya kijamii baada ya kufunga ndoa. simu za nyakati za usiku kutoka kwa marafiki zako hutazipata, wala mialiko ya party au dinner ambayo kwa asilimia kubwa itakuhitaji upate ruhusa kutoka kwa mweza ili aridhi

kwa tafiti za wanandoa zinaonesha kua watu hupoteza rafiki wa karibu pindi tu watapofunga ndoa

Ndoa inaweza kusababisha tabia hatari ya kumtegemea mtu mmoja kwa kila hitaji
ukiwa mwanandoa unaingia kwenye dhana ya mwili mmoja, bahati mbaya dhana hiyo haiishii hapo tu bali hufifisha ujasiri na kuimarisha uzembe wa kumtegemea mwana ndoa wako kwa kila kitu.

imagine mwanandoa wako unamtegemea yeye kuanzia ngono, company, mtunza fedha, mpanga bajeti, mshauri wako karibia kila kitu. jambo la kustaajabisha ni kwamba hii dhana huonekanna ni jambo zuri na romantic na ndio maana ni kawaida sana hata wasanii kuimba "youre my everything" kama dogo janja alivyoimba kisha baada ya kuoa siku kadhaa kupita akatemana na uwoya wakati ndiye kila kitu chake

watu waliooa mwisho wao hauwi na furaha kama ilivyo kua awali wakiwa single, kwa statistic za wanasaikolojia maana nyingi
Ngoja nikujibu kwa ufupi wenye kukidhi haja. Wake zetu wana akili sana, huwa wanagomba wanapo kuona unapoteza muda mwingi na marafiki kwenye hamna,hakuna mwanamke ambaye ana akili timamu, akishajua uko na watu makini na mnafanya mambo ya msingi akawa sababu ya wewe kupoteza marafiki zako. Wake zetu huwa wanachukizwa na sisi wanapo ona badala ya kurudi nyumbani tunaishia kwenye vijiwe na kupiga soga. Huu ni uzezeta.

Automatically maisha unayo ishi kabla hujaoa lazima yabadilike baada ya kuoa. Sababu sisi ndiyo walinzi kwa wake zetu na watoto zetu, kwanza lazima turudi mapema nyumbani kwa ajili ya kusikiliza kesi mbali mbali toka kwa wake zetu juu ya watoto zetu au mfano wao.

Kadhalika ni uzwa uzwa una mke na familia unachelewa kurudi nyumbani kijinga jinga tu kisa marafiki, wewe utakuwa hujui vipaumbele.

Mpaka muda huu muda sijapewa faida ya kutokuoa wala kuolewa.
 
Very simple

Hasara:

Ukioa au kuolewa unajifunga, kuna baadhi ya mambo hutotakiwa kuyafanya au kua nayo tena, ili ndoa yako i survive kuna vitu utalazimika kuviacha pia, mfano kuna mtu kaongelea huko juu kua ,,
  • Itabidi uachane na baadhi ya marafiki
  • Itabidi ubadilishe life style yako
-Ukioa ni agano unajifunga kwa wakristu. hutakiwi kua na mwanamke mwingine wala totoz the same thing kwa wanawake pia.
-Lazima ubadilishe aina ya uvaaji tofauti na kabla ujaoa
-Pia kwa mwanamke anakua na majukumu mengi ambayo yatamnyima uhuru wake, mfano akitaka kwenda sehemu lazima amuage mumewe, kurudi nyumbani pia lazima arudi within a specific time, tofauti na wanaume, kifupi wanawake wanakua under control.

Faida ya kuoa au kuolewa

- faida ni kua na familia,
-heshima kwa jamii inayokuzunguka
-kuna baadhi ya kazi kupata mpaka uwe umeoa au umeolewa

Faida za kutokuoa au kuolewa

Unakua huru na mambo yako, huna haja ya ku m please mtu au kuomba ruhusa ya mtu ili tu kufanya jambo lolote.

Unakua huru kuishi aina yoyote ya maisha unayoyataka, ukitaka kua muhuni, mlevi, mdangaji yote sawa tu no one care

Hasara
  • kitu kikubwa hapa ni uzinzi tu
  • kutoaminika na jamii yako inayokuzunguka, wapo watakao kuona muhuni, malaya, hanisi, lesbian upande wa wanawake n.k
-
 
Ngoja nikujibu kwa ufupi wenye kukidhi haja. Wake zetu wana akili sana, huwa wanagomba wanapo kuona unapoteza muda mwingi na marafiki kwenye hamna,hakuna mwanamke ambaye ana akili timamu, akishajua uko na watu makini na mnafanya mambo ya msingi akawa sababu ya wewe kupoteza marafiki zako. Wake zetu huwa wanachukizwa na sisi wanapo ona badala ya kurudi nyumbani tunaishia kwenye vijiwe na kupiga soga. Huu ni uzezeta.

Automatically maisha unayo ishi kabla hujaoa lazima yabadilike baada ya kuoa. Sababu sisi ndiyo walinzi kwa wake zetu na watoto zetu, kwanza lazima turudi mapema nyumbani kwa ajili ya kusikiliza kesi mbali mbali toka kwa wake zetu juu ya watoto zetu au mfano wao.

Kadhalika ni uzwa uzwa una mke na familia unachelewa kurudi nyumbani kijinga jinga tu kisa marafiki, wewe utakuwa hujui vipaumbele.

Mpaka muda huu muda sijapewa faida ya kutokuoa wala kuolewa.
Umemjibu vizuri mkuu lakini hao marafiki lakini huwezi kua nao kila sehemu, mfano unakuta wewe mwanaume una interest za viti tofauti tofauti kama

Mpira: hapa unaweza kukuta una urafiki mkubwa sana na mtu kwa sababu tu ya mpira labda mnashabikia timu moja, na kweli mkawa marafiki sana,, katika nyanja hii asimilia kubwa ya urafiki wenu utakua unahusu mambo ya mpira na vitu vingine vyenye kuelekea huko

Halafu mke wako akupangie kua achana na huyo rafiki yako kisa tu urafiki wenu haujengi kwa maana ya maono ya kutengeneza pesa n.k ,, huoni kama hapo pia ni kukosa uhuru?
 
Hatari ya Kupata ngoma. Maana condom haitumiki.
 
Mpira: hapa unaweza kukuta una urafiki mkubwa sana na mtu kwa sababu tu ya mpira labda mnashabikia timu moja, na kweli mkawa marafiki sana,, katika nyanja hii asimilia kubwa ya urafiki wenu utakua unahusu mambo ya mpira na vitu vingine vyenye kuelekea huko

Halafu mke wako akupangie kua achana na huyo rafiki yako kisa tu urafiki wenu haujengi kwa maana ya maono ya kutengeneza pesa n.k ,, huoni kama hapo pia ni kukosa uhuru?
Swali la msingi ni kuwa je unapata faida gani unapo shabikia mpira na kupoteza muda katika mpira ? Jibu la haraka na usahihi ni kuwa hakuna faida unayopata ukishabikia mpira na kuangalia mpira zaidi ya kupoteza muda na hela.

Maana yake ni wajibu wako kumsikiliza mkeo katika hilo, sababu halina faida na wewe.

Uhuru usiyo na mipaka ni utumwa wa kujitakia. Hapo hakunyimi uhuru bali anakusaidia juu ya kuachana na vitu vya kipuuzi.
 
Mpira ni burudani, mpira ni kama burudani zingine mfano mziki, kutazama movie na kuendelea.

Naomba nikuulize, wewe burudani yako ni ipi?
 
Back
Top Bottom