Kama kuna yeyote anaeweza kunipa faida za kutokuoa au kutokuolewa ajitokeze

Kama kuna yeyote anaeweza kunipa faida za kutokuoa au kutokuolewa ajitokeze

Sisi waswahili tunasema uungwana ni vitendo na salamu kwa aliye mbali na wewe ni nusu ya kuonana. Nawasalimu kwa maamkizi yetu wote watoto na wavyele.

Anuani ya mada yangu iko wazi na yenye kueleweka. Mwenye kujua ajitokeze atupe faida za kutokuoa na kutokuolewa.

Ahsanteni sana.
kutooa ni unakua huru
 
Mpira ni burudani, mpira ni kama burudani zingine mfano mziki, kutazama movie na kuendelea.

Naomba nikuulize, wewe burudani yako ni ipi?
Labda hatujui mambo yenye faida,japo ambalo halina faida katika afya ya akili yaki, mwili na mali yako halina faida kiuhalisia.

Muziki ni burudani lakini hauna faida, kama ulivyo mpira na mfano wake.

Mimi burudani yangu ni kula chakula kizuri ninachi kipenda na cha halali.
 
FAIDA ZA KUTOKUOA
1.Kutokuwa na mwanamke wa kumgharamia mavazi na maurembo
2.Kutokuwa na mzigo wa familia ya kutunza na kusomesha
3.Kuwa na urahisi wa kuishi gheto (single room) kwa muda mrefu bila kusukumwa kujenga haraka
4.Kutokuwa na sress kununiwa au kutukanwa na mkeo
5.Kutokuwa na mtu wa kukubughudhi hata usipokuwa na chochote mfukoni

HASARA ZAKE
1.Utakuwa unaongezeka umri lakini huongezeki hekima na busara, waweza jikuta unatongoza na kufanya mapenzi hata na kabinti ka darasa nne.
2.Utaikosa heshima ya kimungu ya kuitwa BABA kwani katika familia watoto humuona baba ni kama MUNGU!
3.Wawezajikuta katika visanga na misukosuko ya kutembea na wake za watu au jirani zako
4.Hata ungelikuwa na umri gani, kuishi bila mke ni ngumu kujishauri katika baadhi ya mambo muhimu ya maendeleo, kama vile kununua au kujenga nyumba yako mwenyewe
5.Sehemu kubwa ya jasho lako utawekeza kwa hasara na unaweza usiwe na mwisho mzuri wa maisha yako kwani kukosa watoto maana yake hutokuwa na msaada uzeeni pale utakapohitaji msaada wa wenye nguvu na uwezo kwa wakati huo wewe hata kutoka nje kuota jua unahtaji mtu wa kukokota.

Kwa upande wa wanawake nafkiri faida na hasara zinashabihiana japo kuna variation flani
 
Mkuu wasiooa watarukaruka humu kwenye uzi lakini ukweli ni kwamba khasara wanayopata ni kubwa kuliko faida(khasara >faida) .Wanaishi maisha ya wasiwasi,khofu na kutojiamini.Ni kundi lililojaa khasira na jazba muda wote kisa wanakosa UPENDO.
 
Faida ya kutoolewa Ni kutofua minguo ya mtu mzima mwenye mikono yake.
 
Maisha ni kuchagua,Mimi napenda kuishi maisha huru,nahis nisipooa nitaishi kwa amani sana na kwa starehe,Kuna zile unakutana na manzi mzuriiiiiiiiiiiiii afu anakushobokea mwenyew,ukiwa hujaoa unapitia fasta ila ukiwa umeoa unaanza kumuwazia mkeo,mi kuoa mpaka niwe na miaka 45
Unamiaka mingapi sahizi?
 
Sio uhuru ni utumwa huo
 
Ha haaaa haaaa eti Mungu,we jamaa WeWe mbona umeongea Kama umekatwa kichwa?
Kwa hiyo unamfulia mmeo huku umenuna,au ndo hata kumfulia kwenyewe humfulii? manake wanawake wa humu mh!
 
Ha haaaa haaaa eti Mungu,we jamaa WeWe mbona umeongea Kama umekatwa kichwa?
Kwa hiyo unamfulia mmeo huku umenuna,au ndo hata kumfulia kwenyewe humfulii? manake wanawake wa humu mh!
 
Nafua huku nimenuna!nguo avae Nani kufua afue Nani!
Hahahahaaa,najaribu kuvuta hisia jinsi unavyokua pindi umebeba nguo za mmeo kwenda kuzifua napata picha matata sana.
Wifi yako huku anapofua zangu anachukua fulana/shati suruali yangu anazivaa anafua zingine akimaliza ndio anavaa kanga kumalizia zile azozivaa.
MKIPENDANA hata huko peponi hamtaona haja ya kwenda
 
Wacha weeeeeeee,hivi nyie huwa mnakutana sayari hii hi au Mars?!Mimi Kuna wiki ambazo akizingua sifui kabisa namuacha atambue uwepo wangu,asubuhi Sasa anahaha kutafuta boxer na soksi,mimi Niko busy naimba kapambio kangu ka Mungu yu mwema,mchana utasikia nimekumiss!kanimiss au kamiss soksi na boxer?
 
Back
Top Bottom