Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Kila baada ya uchaguzi mkuu imekuwa ni jambo la kawaida kusikia wapinzani wa wakilalamika kuwa wameibiwa kura. Jambo ambalo W anaCCM huwa wanakanusha. Lakini hiki kilio cha wizi wa kura ni cha muda mrefu.
Mwaka 1995 mtifuano mkali kati ya mgombea uraisa wa NCCR Mageuzi na CCM ulisababisha watu wengi kuamini kuwa huenda matokeo yalichakachuliwa. Maana ushindani ulikuwa mkali sana. Na kwa kulinganisha ushindani kipindi cha kampeni na matokeo ndio hapo watu huamini kuwa matokeo yalichakachuliwa.
Lakini nini hasa suruhu ya hili tatizo?
Kwa nini wapinzani na chama tawala wasikubaliane kufanya mabadiliko ya katiba kuwe na kipengele kinachoruhusu matokeo ya urais kuhojiwa?
Kwa nini tusiwe na mahakama ya juu itayokuwa na mamlaka kusikiliza malalamiko ya wizi wa kura au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi?
Huu ndio wakati wa wadau wote wa demokrasia kuhakikisha kero kama hizi zinafutika. Tusisubiri 2025 kusikia kilio kinachojirudia kila uchaguzi ukifanyika.