Hicho ndicho kilichonijia kichwani leo nikiwa natafari mwenendo wa siasa za Tanzania kwa sasa.
Maswali ni je nani atakubali kusimama na ni nani atakubali mwenzake kusimama.
Itakua nipatashika nguo kuchanika ndani ya vyama na nje ya vyama.
SIYO KILA UTAWALA HUTOKA KWA MUNGU.
Kwa nini Mungu aliwaepusha wana wa Israel na mateso ya Farao nchini Misri kama Falme zote zinatoka kwa Mungu? (Mwanzo 12:10-20, Mwanzo: 37-50. na Kutoka: 1-40)
Je nao utawala wa Nebucadnezar wa Babeli ulitoka kwa Mungu? Mbona aliwatumia manabii kuwatoa mikononi mwao na kuwarudisha Jerusalem ? (Ezra: 1-10)
Kwenye agano jipya Yesu mwenyewe amejaribiwa mara tatu na Shetani lakini amekaidi akiwa kwenye mfungo wa siku 40. (Luka 4:1-13). Yesu amekataa kumtii Herode alipomtaka ageuze maji ili iwe mvinyo ili amuachie baada ya Wayahudi kumkamata kabla ya kuhukumiwa na Ponsio Pilato.(Luka 23:7-15)
Hii ina maana kuna tawala dhalimu ambazo zinatoka kwa shetani lazima tuzikatae kwa nguvu zote kama Wakristu. Kinyume cha hapo ni kudhalilisha Ukristu wetu.
Utawala wa Magufuri ulitoka kwa shetani, siyo kwa Mungu wetu aliye hai, na tuliukataa kwa nguvu zote. Magufuri hakuwa na Mungu kabisa katika matendo na fikra zake. Mtawala anayetoka kwa Mungu hawezi kuwa na roho kama ya Magufuri inayotuma kuua Tundu Lissu, kuua Ben Saanane, Azory Gwanda.
Utawala unaotoka kwa Mungu hauwezi kubomoa nyumba za watu wa Kimara- Mbezi bila kuwafidia halafu ukaacha nyumba za Wasukuma wa Mwanza bila kuzibomoa.
Utawala unaotoka kwa Mungu hauwezi kukawafukuza wafanyakazi waliofoji vyeti vya Form IV ili wawe madreva na kumuacha Makonda aliyefoji cheti cha form IV na kuwa Mkuu wa Mkoa. Ndiyo maana ameondolewa pamoja na kuiba uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019 na uchaguzi Mkuu wa 2020. Mungu hazihakiwi