Kama kweli Magufuli aliletwa na Mungu basi uchaguzi wa 2025 utakua ni patashika nguo kuchanika

Mama Samia ndiye Rais na Mwenyekiti wa CCM.
Apende asipende 2025 lazima agombee.
Tutaandamana na kumchukulia Fomu.

Utaratibu wa Chama Mwenyekiti ndiye anayekuwa Rais.
Na alikua makamu wa Rais akaimudu vizuri nafasi yake na sasa ni Rais mtenda haki na nchi inapumua.

Mama Samia anajiamini kupita maelezo. Akikwenda Kenya na kwenda moja kwa moja Hospitalini kumsalimia Tundu Lisu bila kuhofia wauaji ndani ya Chama na serikali yake wanasemaje!
Kwa sasa ndiye mkuu wa nchi.

Naamini Huyu Rais ndiye tuliyepewa na Mungu mana hakuna Mwanadamu aliyewaza kuwa ipo siku Samia angekua Rais . Ni Mungu pekee alijua kuwa atawaletea watanzania Mama mwenye huruma ili aliunganishe Taifa na kuondoa Dhulma.

Nchi imejaa dhulma. Mama ataisafisha nchi. Waliopita waliwaza fedha tu na kudhulumu wananchi kwa kukwapua Mali zote za Umma.
Yani watwala mabilionea ndio waliojiuzia nyumba za serikali kwa bei ya kutupa. Hao hao ndio waliogoma kuwaongezea wafanyakazi madaraja na kutoa ajira. Leo mama Samia ameona dhulma na kero zinazogusa maisha ya watanzania walioishi kwa vitisho na kudhulumiwa na watawala waliobeba hulka za tawala katili za Kifirauni na kirumi za karne zilizorangulia.


Mama Samia Chapa kazi tuko nyuma yako. Mama Samia 2025 na akimaliza muda wake tutamuongezea tena mpaka 2050 Mungu akitaka iwe hivyo .
Mungu ametuletea Mama Mama mtu muungwana na mstarabu na mpenda haki bado tunatamani kuongozwa kishetani na kinyangau kama wanyama.

Watu waovu Mara nyingi wanapenda kutawaliwa kiovu ili wapate nafasi.
Vyeo vya kwenye mabaa na magest awamu hii vimeota mbawa. Mama anaweka watu waadilifu na wenye mapenzi mema kwa Taifa sio watu wabinafsi wanaokwapua Mali za Umma ili wakalale kwenye mabaa na magesti wakati hospitalini hakuna dawa.



Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Nothing last forever.
Ni suala la mda tu
 
Kama kuna Mtu mwenye picha za Ellen Jonson Sirleaf (Raisi wa kwanza wa Mwanamama wa Liberia) atuwekee hapa Raisi wetu avae kilemba kama hicho sio hijabu za kidini.

Tunampenda Raisi wetu ila afuate Katiba na Sheria.
 
Hicho ndicho kilichonijia kichwani leo nikiwa natafakari mwenendo wa siasa za Tanzania kwa sasa.

Maswali ni je nani atakubali kusimama na ni nani atakubali mwenzake kusimama.

Itakua nipatashika nguo kuchanika ndani ya vyama na nje ya vyama.
Wema hauozi na mauti ya mwenye haki Mungu huheshimu.....Naiombea nchi yangu mema, wengine wote tutavuna tulicho na tunacho kipanda tena kwakipimo cha kusukasuka, kujaa na kumwagika...Says Ame the Prophet!
 
Take my word, it won't happen bro..
 
Babu vipi?, mungu mwenyewe alimwiita Nebukednezer mtumishi wangu, , ,
Mungu alimwita mfalme koreshi wa iran, MASIHA, kwasababu ya kuwakomboa wayahudi toka utumwani babel na kuwarudisha caanan[emoji847][emoji847]
Sijamuongelea Cyrus the Great mfalme wa Persian Empire, ila usiseme Iran
 
Mnaikosea sana Biblia !! Siyo kila utawala hutokea kwa Mungu. Yaani Hitler alitoka kwa Mungu kweli? Hapana tuache kumtwisha Mungu UDHALIMU wa binadamu
 
Hicho ndicho kilichonijia kichwani leo nikiwa natafakari mwenendo wa siasa za Tanzania kwa sasa.

Maswali ni je nani atakubali kusimama na ni nani atakubali mwenzake kusimama.

Itakua nipatashika nguo kuchanika ndani ya vyama na nje ya vyama.
UPINZANI ni weak sababu kuna watu si waaminifu - mchana upinzani na usiku ccm
 
Changamoto ni Nani atafikia standards alizoweka Magufuli ndani ya miaka 5.
Maana kwa miaka yote mpaka Rais anamaliza 10yrs anatuambia Kasungura kadogo.
Standards gani kaweka Magufuli? Za uwongo na wizi wa Mali ya umma? Za kujenga Kijijini kwake miundombinu ya kitaifa kwa kutumia Mali ya umma?

Standards za kuua akina Ben Saanane na Azory Gwanda? Standards za kumshambulia mbunge Lissu akiwa Bungeni kwa risasi 16??
 
Kweli standards aliweka JK juu ya EPA, ESCROW, RICHMOND,wafanyakazi hewa.
Kuuawa Mwangosi,Ulimboka kung'olewa meno na kucha bila ganzi.

Mwingine aliyeweka standards ni Mbowe kutafuna ruzuku tangu chama Cha baba mkwe aanze kukisimamia bila hata kujenga ofisi.

Rushwa ya ngono Ubunge wa kuteuliwa.
Kuwa mwenyekiti wa maisha.
 
Anakwambia sumu haionjwi
 
Kama aliletwa na Mungu ndio Mungu huyohuyo amemchukua TUMSHUKURU
 
JK juu ya EPA,
Ni fedha zimeibiwa wakati wa B Mkapa siyo JK

RICHMOND
Hakuna fedha ya Serikali iliyotoka kwenda kampuni ya RICHMOND

Wafanyakazi hewa.
NI mambo ya kusadikika ambayo Magufuli alikuwa ana hisi

Kuuawa Mwangosi,
Wahusika walikamatwa na mkondo wa Sheria uliwahusu

Ulimboka,
Yuko hai at least kuliko Ben Saanane aliyeuliwa na Magufuli
 
Baraghashia si vazi la lazima kwa Muislamu ni urembo tu, Ila hijabu kwa mwanamke wa Muislamu ni lazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…