Kama kweli mnajiamini mguseni Mtanganyika Dr. Emanuel Nchimbi

Kama kweli mnajiamini mguseni Mtanganyika Dr. Emanuel Nchimbi

Hakuna kitu kitaiua CCM haraka kama Utanganyika vs Uzanzibari. Na hapa ndipo panaogopwa zaidi na Samia.
Hili silielewi, mkuu 'Fazil', la Samia kuogopa "u-Tanganyika na u-Zanzibar'.

Sioni kigezo chochote kinachohusiana na jambo hilo kinachomhusu Samia mwenyewe moja kwa moja.

Ungefafanua zaidi huenda nami ningeelewa unachomaanisha hapa.

Kawaua waTanganyika huyu kwa maelfu, kwa kuwatumia waTanganyika hao hao, na sasa ni waTanganyika kama akina Asha-Rose na akina Wasira, Kambamaganda, Nchemba na wengine wengi wanaomsifu kufanya "kazi ya kutukuka" kwa mauaji hayo!

Huenda unayo maana yako nyingine ya "...kuua CCM haraka..." ambayo mimi bado sijaitilia maanani.
 
Acheni kuingia kwenye mitego ya CCM, watu wameuwawa October 29 na huyu Nchimbi akiwa katika kubariki mauaji hayo .
huyo nchimbi angetoa kichwa tu na yeye angeliwa juu juu, wale wazanzibar walikuwa hawatanii
 
Siwezi kukubali kuona Watanganyika wananyanyaswa au kuuliwa hata kama ni itikadi tofauti.
Kuhusu hili mkuu 'figga' sina tofauti yoyote nawe.
Kama upo karibu na Nchimbi, mshauri ajiweke mbali na watu wanaofanya haya tusiyokubaliana nayo wewe na mimi.
Huo utakuwa ushauri mzuri sana kwake Nchimbi..
 
Mnachezewa kisiasa tu 😀 Nyote mmeamini YUDA anaezungumziwa ni Nchimbi, mkiulizwa sababu ni ipi hamna, basi tu mnapenda kujitengezea furaha. Hivi mna akili kweli? Umekaa hapo unamshadidia kiongozi ambae yumo katika serikali ambayo wewe huitambui na unaiita ya haramu, anakula mshahara kupitia serikali hio hio.
 
View attachment 3600265

Salaam Wakuu,

Naomba Dr. Emanuel Nchimbi mumuache afanye kazi.

Msimuingize kwenye ugomvi wenu na Ufisadi wenu..

Ameishi kwa heshima kwa kuheshimu wakubwa na Wadogo..

Uroho wenu wa madaraka usiwafanye mumchafue kisa yeye anawalazimisha kutenda mema.

Watanganyika tuko nya yake, na tumeona figisu zenu zimeanza..

Dr. Emanuel Nchimbi nakutia moyo.
Kaa kimya kama kawaida yako.

Hii Nchi ni ya Wananchi si mali ya mtu mmoja..

Wanaotumwa kukushambulia, wameshindwa kabla ya kuanza..

Fanya kazi zako kwa mjibu wa katiba, usishiriki maovu.

Baada ya kufanya mliyofannya kwa Balozi Humprey Polepole mnafikiri mtaweza fanya kwa Nchimbi pakalike? Jaribuni
Hii karat inavyochezwa wee huwezi jua iko hivi.
Huyu jamaa kaambiwa ajitenge fulani kama vile kasaliti ili kurudisha watanzania pamoja upepi uelekee kwake mama asahahulike mabaya yake maana ji muhulq wake wa mwisho akistaafu hamna shida .kazi iliopo ji kuhakikisha anafanya kazi kama hafungamani na mama ili kufanikisha jambo fulani maana watanzania mpaka sasa ccm haijui itaanzia wapi 2030 kazi itakua ngumu mno
 
Ntashangaaa sana kama kuna Mpumbavu yeyote anae ona kuna kiongozi wa ccm alieko madarakani leo hiii yupo upande wa wananchi...yani kama ni kulogwa watanzania tumelogwa mlogo wa enzi za Nyerere.

Unaanzaje mtetea mtu alieko madarakani leo hiiiii..unaaanzajeee?

Nani yupo pale alipo kwa haki au kwa matakwa ya wananchi NANIiii...

Yote ni yale yaleeee Hebu KAZENU na tambueni nini mnakitaka
 
Nchi keshawahi kukemea mauaji yaliyofanywa na bosi wake?
Nnimetafuta hotuba zake za kukemea mauaji nimekuta wamezifuta.. Hotuba zake anakemea maovu sijui nani anaziondoa mtandaoni
Screenshot_20260603_200700_TikTok.jpg
 
Watanganyika wanadanyika kirahisi sana,tatizo sio mtu ni mfumo, mkihisi yupo nanyi karaghabao
 
View attachment 3600265

Salaam Wakuu,

Naomba Dr. Emanuel Nchimbi mumuache afanye kazi. Kwanza udaktari wake wa kusomea so aheshimiwe.

Msimuingize kwenye ugomvi wenu na Ufisadi wenu..

Ameishi kwa heshima kwa kuheshimu wakubwa na Wadogo..

Uroho wenu wa madaraka usiwafanye mumchafue kisa yeye anawalazimisha kutenda mema.

Watanganyika tuko naye bega kwa bega, na tumeona figisu zenu zimeanza..

Dr. Emanuel Nchimbi nakutia moyo. Kaa kimya kama kawaida yako.

Hii Nchi ni ya Wananchi si mali ya mtu mmoja..

Wanaotumwa kukushambulia, wameshindwa kabla ya kuanza..

Fanya kazi zako kwa mjibu wa katiba, usishiriki maovu.

Baada ya kufanya mliyofanya kwa Balozi Humprey Polepole mnafikiri mtaweza fanya kwa Nchimbi pakalike? Vita ya maji maji itapigwa mara ya pili. Jaribuni
Kama Polepole amesahaulika, Magufuli amesahaulika, na makumi kadhaa ya watu nao wamelala mauti na yeye tutasahau tu wakiamua na MUNGU akaruhusu
 
Acheni vigeugeu chadema, kama hamuwataki ccm, iwe ccm wote sio mnapick and choose, ccm wote ni walewale...
Kazi ya Chadema ni kutafuta haki popote pale inapodhulumiwa iwe CCM, chaumma nk. Siyo kwa ajili mtu ni adui yako ndio utake adhulumiwe. Pole mlio na mawazo finyu
 
Back
Top Bottom