Kama kweli Mungu yupo inabidi aniombe msamaha

Duniani tumeletwa ili tumjue, tumpende, tumtumikie na mwisho tufike kwake Mbinguni, ambako tutaishi maisha yetu yote - Milele na milele.
Sasa dunia kama siyo makazi ya kudumu aliiumba ili iweje?? Alishindwa kutiweka huko huko mbinguni automatic?

Sent using unknown device
 
Mwenyezi Mungu ametupa "uhuru kamili" juu ya mambo yetu. Hatuingilii kwa namna iwayo yote, na hii ndio inamfanya awe tofauti.

Ninarudia tena, ninaomba usome vizuri. Alielewa kila kitu, lakini bado alimuumba shetani na kumpa akili na utashi. Kwa maneno mengine, shetani angeweza kubadilisha hatima yake kwa kutumia vema akili na utashi aliopewa katika kufanya maamuzi yake, wala asingekuwa mbaya kama alivyo leo.

Shetani alichagua mwenyewe kuwa na kiburi, na Mwenyezi Mungu hawezi kumlazimisha asiwe na kiburi, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwaminifu kwa ahadi zake na hawezi kujipinga mwenyewe kwa kuingilia maamuzi ambayo alishaamua kutoyaingilia.
 
Nimeshakujibu, aliliona ila bado alimpa shetani nafasi ya kubadilisha "fate" yake. Kitu ambacho shetani alichagua kutokukifanya.
Kwaiyo mungu hakuliona hilo kabla kua hata ukimpa shetani nafasi hatofanya anachokifanya?

Kama aliliona alianzaje kumpa nafasi kama jaribio wakati alisha liona jambo hili kua shetani hawezi kufuata anavyotaka?

Yaani ni sawa na wewe una mtoto wako wa chekechea. Halafu unampango wakumpa mtihani wa mathematics wa form six. Wakati hata kabla ya kumpa ulishajua kua ukimpa mtihani ule huyo mtoto hatofaulu. Sasa inamaana mpaka unampa mtoto mtihani huo je ulikua huna uhakika na maono yako???? unategemea atafanya jambo lipya ambalo lilikua tofauti na maono yako uliyoyaona kabla kua hatofauru??

Sent using unknown device
 
Ndio maana nimekuambia, Mwenyezi Mungu alimpa maarifa yote shetani. Shetani alifanya maamuzi akiwa na taarifa zote muhimu. Kama unajua vizuri historia ya shetani wala usingekuwa na hizi misunderstandings.

Mfano wako wa mtoto upo tofauti na uhalisia. Wewe unachoongelea ni kuwa unampa mtoto mtihani wa mambo ambayo hajui na haujamfundisha, kitu ambacho ni tofauti kwa shetani aliyekuwa anajua kila kitu.

Shida unasoma haraka, sijui hauelewi? Majibu yapo kwenye hizo post zangu hapo juu. Unarudia maswali ambayo nimeshayajibu.

Mimi ninalala, tutaendelea siku nyingine.
 

Kama mungu ametupa uhuru na hauingilii uhuru aliotupatia, imekuaje auingilie uhuru huo kwa kudai kua atatuchoma moto wa jehanamu?

Kiburi ichi cha shetani alikipatia wapi, ikiwa kilakitu kibaya chanzo chake ni shetani je chanzo cha viburi kuasi kililetwa na shetani yupi mpaka kikasababisha huyu shetani kumuasi mungu???

Sasa pamoja na utashi aliopewa shetani kwani mungu hakuliona hili swala kua kwanamna yeyote ile huyu bwana atakuja nisaliti siku za mbeleni??

Hapo utakubaliana na mimi kua mungu hakuweza kujua linalojiri mbeleni, ndio maana alishindwa kumfanya shetani asihasi kwa namna yeyote ile

Sent using unknown device
 
Mkuu naomba niongezee kidogo kuwa kwann Mungu hatutokei kama alivyokuwa anawatokea akina Adam na Eva,Ibrahim, isaka,yakobo,Musa na mitume wake Wengine.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mambo ukiyafikiria kiundani zaidi utaona suala la Mungu kuwepo au kutokuwepo ni changamoto kubwa.. Hebu fikiri Mungu alijua kuwa Adam na Eva watamkosea,na atakaye sababisha ni shetani..kama kweli alikuwa anawawazia mema Adam na Eva kwann asinge deal na shetani (nyoka) ili kuwaweka salama adam na Eva waendelee kuinjoy maisha ya bustanini.? Kibaya zaidi anakuja kumlaani nyoka,adam pamoja na Eva(hii haikuwa solution) zaidi ilitakiwa apambane na kiini cha tatizo na si kupambana na mwanadamu aliyemuumba mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu Ni Mwema
Tena Husamehe Wajinga Wasiojua Watendalo
 


Wewe ndiye unayetakiwa kumuabudu na kumshukuru Mungu kwa sababu kama angetaka angalikuumba funza wa chooni badala ya mtu.

Mungu Kukuumba mtu ni heshima kubwa sana aliyokupatia kwa sababu hiyo ni tiketi ya wewe kwenda "peponi" kwenye maisha ya milele baada ya kufa ambapo viumbe wengine wakifa hiyo inakuwa "the end all" ya maisha yao.

Majanga na madhara yanayomkabili mtu mengine huwa ni yanatokana na ujinga wa mtu mwenyewe mfano mtu anaambiwa kwamba meli hii inauwezo wa kubeba tani 2, mtu anabeba tani 5!!, sasa hapo unataraji nini??, wewe huna akili aliyokupa Mungu ya kujua kitakacho tokea unapozidisha uzito??, kwanini Mungu alaumiwe kwa uzembe wa mtu mwenyewe??!!,.

Juu ya yote kila kitu ni kiumbe chake na sisi sote tumekuja kwa hiyari na matakwa yake basi tuache viburi vya kujiona isije kuchochea hasira yake na akatuangamiza "with agony" tukijua kuwa yeye anafanya analolipenda kama jinsi alivyopenda sisi tuwe watu, hiyo ni heshima kubwa aliyotupa hivyo tutoe shukrani badala ya kulaumu.
 
unanitisha kwene hamna mkuu?
 
Mkuu sioni sababu ya kumshukuru nimshukuru kwa lipi labda?
 
Fact
 
Fact
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…