Kama kweli Mungu yupo inabidi aniombe msamaha

Kama kweli Mungu yupo inabidi aniombe msamaha

Wew usiwe kichwa panzi

Upo mji tumeandaliwa, mji mzur huko mbinguni, watu wa Mungu utawakuta huko.

Wew uliye dunian sasa ishi ukiomba na wew uje ufike huko.

Maisha ya duniani hapa ni kibarua tu.

Ila kama ukifa na dhambi zako duu my dear utachomwa moto kuchomwa....
Kufa sio kitu kibaya, ubaya wengi wanao kufa wanaacha mapengo kilofa kutokana na kuwa hawakutimiza wajbu wao dunian ipasavyo, ndio maana wengi wanao achwa wanakaa kulalama.
Mimi nimemmaindi tu kutokana na sifa yake yakujua yaliyo mbeleni kabla hayajatokea. Kwa sifa hii inamaana alijua kua kivuko cha nyerere kitakuja kuzama lakini hakuzuia akaacha ndugu zetu wapoteze maisha wakati alikua na uwezo wa kuzuia.

Kwasifa hii bora tu asiwe anajua yajayo maana haina umuhimu, yaani unajua yajayo halafu huwezi kuyaepusha mabaya ambayo uliyaona kabla hata hayajatokea

Mimi ninamashaka sana na huyu mungu. Vitabu vyake vinatuambia hakuna linaloshindikana mbele zake, lakini tunaona ameshindwa kutokomeza dhambi pamoja na kumdhibiti shetani.

Tunaambiwa ombeni lolote nanyi mtapewa. Lakini tunaona wachungaji bila sadaka zetu hawaendi toilet, inamaana mungu kashindwa kuwasaidia watumishi wake kuwapatia hitaji lao mpaka wategemee sadaka za waumini ambao wamekua wakihangaika usiku na mchana kutafuta ridhiki kwa jasho kwa ajili ya familia zao?

Mungu huyu aliyekua hana masihala na watenda dhambi wakipindi icho, mpka kufikia hatua ya kuangamiza kizazi cha sodoma na gomora kwa moto. Leo hii america na nchi nyingi za ulaya zimehalarisha ndoa za jinsia moja lakini katulia tu bila kuchukua hatua yoyote.

Sent using unknown device

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.
Binadamu sisi sio wakamilifu,
Kwanini alituumba tuwa hatuna ukamilifu? Hii pia nilawana anayo stahili kupewa

2.
Mungu hakukuleta duniani ili ufanikiwe na kuishi kwa furaha.
Amekuleta duniani ili uidhi kua mwaminifu (be faithful)
kama hakutaka tuwe na furaha, kwanini anajiita mungu mwenye upendo wote wakati ametunyima furaha?

3.
Ukitaka Mungu awe upande wako kwanza achana na dhambi na kutenda haki
Hakikadhalika naye mungu akitaka tusitende dhambi angetuumba tukiwa kamilifu, kisicho kamilifu hakiwezi kutenda yaliyo mema tu. Bali kilicho kamilifu hakiwezi kua na kasoro hivyo hakiwezi kufanya maovu yoyote yale.

4. Nikupe somo kidogo kulingana na maandiko ya neno la Mungu....
"...hatuwezi kuishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu..."
kama hatuwezi kuishi kwa njia zetu binafsi mpaka mungu aamue kipi kifanyike na kipi kisifanyike, hapo hata haipaswi kuomba msamaha wowote ukimkosea maana yote hayo ni mapenzi yake hayajatokea kwa bahati mbaya bali ni mpango wake kua yatokee.

Neno la Mungu ni lipi..?? Utaniuliza mbona sijawai kusikia Mungu akinisemesha..
Biblia takatifu ndio maneno peke ya Mungu kwako wew mwanadamu.
Pia Mungu usema nasi kupitia maono.

Kujua yote hayo soma Biblia yako...
Utajua yote yakupasayo kufanya, na utajua kanisa lipi linafundidha na kushiriki ibada kamilifu sawa na maandiko.

"Kumcha bwana ndio chanzo cha maarida"

Chimbuko langu mm ni Mlutheri.

Sent using Jamii Forums mobile app

Swali ni je maombi yanaweza kubadilisha mawazo ya mungu? Mungu akikuandikia kua hakupi je ukisali kwa kuomba atakupa hitaji lako?

Sent using unknown device
 
Wew usiwe kichwa panzi

Upo mji tumeandaliwa, mji mzur huko mbinguni, watu wa Mungu utawakuta huko.

Wew uliye dunian sasa ishi ukiomba na wew uje ufike huko.

Maisha ya duniani hapa ni kibarua tu.

Ila kama ukifa na dhambi zako duu my dear utachomwa moto kuchomwa....
Kufa sio kitu kibaya, ubaya wengi wanao kufa wanaacha mapengo kilofa kutokana na kuwa hawakutimiza wajbu wao dunian ipasavyo, ndio maana wengi wanao achwa wanakaa kulalama.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama maisha ya hapa duniani ni kibarua tu. Mungu aliumba dunia kwa ajili ya nini?

Kwanini nichomwe moto wakati kosa ni lake kaniumba nikiwa sijakamilika?

Sent using unknown device
 
Binadamu mnapenda mitelemko sana, hiyo roho kemea kabisa,
Kuna kitu kibaya kimepandikizwa ndani yako...

Nijibu hili swali kwanza, ndio ntajua kweli unashida ya kutaka kukua au la,

Kwa mafikirio yako
Wew unadhani Mungu kakuleta dunian uje ufanye nn????????
Kwanini alituumba tuwa hatuna ukamilifu? Hii pia nilawana anayo stahili kupewa

kama hakutaka tuwe na furaha, kwanini anajiita mungu mwenye upendo wote wakati ametunyima furaha?

Hakikadhalika naye mungu akitaka tusitende dhambi angetuumba tukiwa kamilifu, kisicho kamilifu hakiwezi kutenda yaliyo mema tu. Bali kilicho kamilifu hakiwezi kua na kasoro hivyo hakiwezi kufanya maovu yoyote yale.

kama hatuwezi kuishi kwa njia zetu binafsi mpaka mungu aamue kipi kifanyike na kipi kisifanyike, hapo hata haipaswi kuomba msamaha wowote ukimkosea maana yote hayo ni mapenzi yake hayajatokea kwa bahati mbaya bali ni mpango wake kua yatokee.

Swali ni je maombi yanaweza kubadilisha mawazo ya mungu? Mungu akikuandikia kua hakupi je ukisali kwa kuomba atakupa hitaji lako?

Sent using unknown device

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa sikubaliani na upoyoyo wa eti kuna maisha ya milele Mbinguni so duniani tumeletwa kufanya nn?
Mosi; Mwenyezi Mungu alikuumba wewe, na anajua kila kitu kuhusu wewe ila hajakupangia. Amekupa akili na utashi wa kutambua mema na mabaya na hivyo kufanya maamuzi sahihi.

Ukiona mambo hayaendi ujue huenda hautumii vizuri akili na utashi aliyokujalia. Lakini, kama kuna magumu unapitia, kwa kiasi kikubwa huenda ni matokeo ya dhambi; ukianza na ile ya wazazi wetu wa kwanza, Adam na Eva.

Pili; pole sana kwa kutokwa na mama. Lakini ujue tu kuwa kifo ni safari kutoka maisha ya hapa duniani kwenda maisha ya Milele huko Mbinguni. Hauna haja ya kumlaumu Mwenyezi Mungu kuhusu hilo. Yeye aliyepanga tuzaliwe kimwili, ndiye aliyepanga pia tufe kimwili, japo roho zetu zitaishi milele.

Tatu; Mwenyezi Mungu hajajificha. Amekuambia umtafute, nawe utamuona. Mwenyezi Mungu anajidhirisha kwetu kila siku. Mtafute, nawe utamuona.

Uwe na wakati mwema mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasema anajibu maombi lakini kwa maombi yote yale karibu nchi nzima kumuombea ruge apone lakin bado kadanja...huyu mungu changa la macho tumepigwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Angekuwepo asingeruhusu ujinga huu wa kumuacha ruge afe kizembe, halafu awaache al shabaab na boko haram waendelee kuua watu wasio na hatia

Sent using unknown device
 
Poleni na majukumu wakuu,. Kama heading inavosema apo kama kweli mungu yupo inabidi aniombe msamaha kwa sababu zifuatazo

Moja: Kama Mungu yupo yupo basi ni wazi kua yeye ndo alopanga maisha ya mwanadam kuanzia kuzaliwa mpaka kufa kwake, hivo basi ata aya magumu ninayopitia ni wazi alipanga yeye iwe hivi aniombe msamaha kwa hili

Mbili:kama kweli yupo basi ni yeye anaeruhusu watu wafe na wengine wazaliwe kwa maana iyo ni yeye ndo aliruhusu ndugu zangu nnaowapenda akiwemo my lovely mother afe, na kwanini aliruhusu afe wakati alijua kua mama angu ndo furaha yangu yeye ndo alienisabaishia hizuni mpaka leo na kwa hili ata aombe msamaha siwezi kumsamehe

Tatu:kwa nini amekua wa kujificha sana au hataki watu wake waujue ukweli kuhusu yeye ina maana mi nnavohangaika kutafuta dini ya kweli yeye hanioni ? aniombe msamaha kwa kweli

Sawa. Usiku huu anahihitaji roho yako.
 
Binadamu mnapenda mitelemko sana, hiyo roho kemea kabisa,
Kuna kitu kibaya kimepandikizwa ndani yako...

Nijibu hili swali kwanza, ndio ntajua kweli unashida ya kutaka kukua au la,

Kwa mafikirio yako
Wew unadhani Mungu kakuleta dunian uje ufanye nn????????

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiniambia nitumie mafikirio kukujibu ntakuambia mungu hayupo

Ukifikiria kwa makini utaona habari hizi za mungu ni uzushi, angekuwepo angehakikisha kila mtu anakua na afya njema pasipo kuugua gonjwa lolote kwasababu yeye ni mungu muweza wa yote, mjuzi wa kila kitu, mwenye nguvu zote kusingekua na sababu yoyote kuruhusu mambo mabaya kwa watu wake

Sent using unknown device
 
Taja msimamo wako mm sijakuomba unitolee maelezo.

Rudia tena, unaamini Mungu yupo au hayupo???

Na kama yupo unadhani kakuleta dunian uje ufanye nn?????

Swali ni je maombi yanaweza kubadilisha mawazo ya mungu? Mungu akikuandikia kua hakupi je ukisali kwa kuomba atakupatia hitaji lako?

Sent using unknown device
 
Na leo alijua utakuja kuandika uzi utakaokera baadhi ya watu. Dah sipati picha nao wakataka awaombe msamaha kwa kukuacha uione leo ili wao wakereke.

Think twice mkuu

VIIXCCCL GrandLodge,ARUSHA
 
Back
Top Bottom