Swali ni je maombi yanaweza kubadilisha mawazo ya mungu? Mungu akikuandikia kua hakupi je ukisali kwa kuomba atakupatia hitaji lako?
Sent using
unknown device
Kwanza Mungu hajakuandikia kutokukupa, amesema ombeni nanyi mtapewa, sharti ni kuomba, ukiomba nawe utapewa, usipopewa kwa wakati unaotaka wewe subiri, jua bado anakuandalia kitu chako ulichoomba, na Mungu kwa wema wake kitu unachoomba kama hakikufai hakupi, instead atakupa kitu ambacho kinakufaa na unachostahili kwa hili mm ni shahidi kwenye maisha yangu,, Mungu ni mtakatifu ni msafi ikitaka kumwendea nenda kwa usafi jisafishe kwanza ndipo mtaelewana, hata maswali yooote haya mnayoyauliza dhidi ya Mungu, majibu yapoo, kama kweli una nia ya kutaka kujua usimulize mwanadamu muulize Mungu mwenyewe atakupa majibu, ila mara nyingi wanadamu ni wavivu hakuna anaetaka kufikia level ya kuhojiana na Mungu tunataka miteremko,, hatuki kulipa gharama ya usafi unaotakiwa ili uweze kuzungumza na Mungu, Adam used to talk to God ila alipofanya dhambi tu na kuharibu uhusiano wake na Mungu ndo uchafu ukaingia akashindwa kuongea na Mungu tena kama zamani, ukisoma Biblia vizazi vikapita akatokea mtu mwingine akakiitia jina la Mungu kwa maana nyingi ukatafuta uhusiano na Mungu baada ya mda mrefu kuvunjika kwa Adamu, saaasa huyo mtu ukisoma biblia ndo familia hiyo hyo ya kina Ibrahimu (Ibrahimu used to talk to God) ndo hiyo hiyo inakuja Isaka (aslo was talking to God) inakuja Yakobo, Yusuph, Musa, Haruni,Yuda, nakuendelea mpaka inakutana na familia ambayo Yesu akazaliwa humo, Nachotaka kuelezea maswali yooote tunayoulizana hapa Majibu yapo kwa Mungu mwombe yeye na atakupa majibu yake kama unataka kujua zaidi njoo PM nikupe mwongozo, kinyume na hapo mtaishia kumdhihaki Mungu na kujichotea dhambi na laana, nimempenda yule aliyesema Mungu ametupa akili na utashi uko sahihi kabisa na ndio majibu, Neno linasema mpende Bwana Mungu wako kwa roho yako yote, kwa akili zako zote, kwa moyo wako wote na kwa nguvu zako zote, ukisoma 1yohana 5:3 atukupa maana halisi ya kumpenda Mungu anasema "Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu kwamba tuzishike amri zake wala amri zake si nzito"
Je ulishawahi kufatilia haya kwenye maisha yako na bado ukafeli?? Maswali yote haya mnaulizana majibu yake yapo embu jiweke karibu na Mungu uone kama hatokujibu, wengi humu pamoja na mtoa mada hamuamini Kama Mungu yupo ndo maana hayo majibu mnayoyataka sijui muombwe msamaha havitakaa vije vitokeee sababu huyo Mungu wa kuwapa majibu hamuani kama yupo, hapa mnapotosha wale wenye uelewa mdogo nao wataanza kumkufuru Mungu na dhambi utakua juu yenu,
Mungu anasema hivii, katika
Kumbukumbu ka torati 39:19
Nazishuhudia mbingu na nchi Juu yenu hivi leo , kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana, basi chagua uzima ili uwe hai wewe na uzao wako"
Sasa hapa tumia akili yako Mungu aliyokupa kufanya machaguo, ila Mungu tayari kakupa ushauri kipi cha kuchagua hapo, Mungu sio dikteta hakuchagulii amekupa akili uchague mwenyewe, yeye ni Mungu hataki kukulazimu wewe uchague nini, ukitumia akili yako kumchagua yeye ndipo anafurahi na kutukuka, ila akitumia nguvu zake yeye kukulazimisha umchague yeye hapo inakua anajiabudu na kujitukuza kwasabu nguvu zake ndo zimetumika,
Mungu yupo na Mungu ni halisi sio Hadithi,
Kuna watu wamepitia maisha magumu Mara kumi zaidi ya mtoa Mada lakini wanaishi Kwa Furaha sasa Kwa sababu ya kuamini Mungu yupo na ndio kila kitu Kwao.
Sent using
Jamii Forums mobile app