Kama kweli Mungu yupo inabidi aniombe msamaha

Kama kweli Mungu yupo inabidi aniombe msamaha

Poleni na majukumu wakuu,. Kama heading inavosema apo kama kweli mungu yupo inabidi aniombe msamaha kwa sababu zifuatazo

Moja: Kama Mungu yupo yupo basi ni wazi kua yeye ndo alopanga maisha ya mwanadam kuanzia kuzaliwa mpaka kufa kwake, hivo basi ata aya magumu ninayopitia ni wazi alipanga yeye iwe hivi aniombe msamaha kwa hili

Mbili:kama kweli yupo basi ni yeye anaeruhusu watu wafe na wengine wazaliwe kwa maana iyo ni yeye ndo aliruhusu ndugu zangu nnaowapenda akiwemo my lovely mother afe, na kwanini aliruhusu afe wakati alijua kua mama angu ndo furaha yangu yeye ndo alienisabaishia hizuni mpaka leo na kwa hili ata aombe msamaha siwezi kumsamehe

Tatu:kwa nini amekua wa kujificha sana au hataki watu wake waujue ukweli kuhusu yeye ina maana mi nnavohangaika kutafuta dini ya kweli yeye hanioni ? aniombe msamaha kwa kweli
Tatizo liko kwako wewe kutumia akili vizuri,Mungu ameshapanga kila jambo,kua ukifanya hivi kutakuwa na matokeo haya,ni sawa na gari,mtengenezaji gari ameshekuwekeq utaratibu gari,lipate service kwa kwa kilomita labda 30,0000,na usipofanya litaharibika,wewe hufanyi,halafu wamlaumu aliyetengeneza gari,itakuwa hutumii akili.
 
Dhambi atende Adam, kuumia niumie then nife mimi. Sema tu ili tuwe na relief ya maisha yajayo, lazima kuwe na impossible thinking kama hivi. Religion and God may not be existing at all, ni mbinu tu za kufanya tuishi kwa matumaini, imagine kama kusingekuwa na imani hizi....
 
Mungu hakukuleta duniani ili ufanikiwe na kuishi kwa furaha.
Amekuleta duniani ili uidhi kua mwaminifu (be faithful).
Uwe Mwaminifu kwa lipi na kwa nani?
Huu ni wizi Mtupu!
 
hakuna Mungu, Huu ni uongo tuliomezeshwa kwa Muda Mrefu!
 
Hata mimi nastahili kusema aniombe msamaha japo siamini kama yupo
 
Kinachonicheleshaga hukusu hizi imani/dini nia pale

Mtu mwenye dini ya kiislam anapomuona kama mtu mwenye dini ya kikristo anapotea, au mtu mwenye dini ya kikristo anapomuona mtu wa dini ya kiislam anapotea.

Lakini akitokea mtu either hana dini au haamini uwepo wa Mungu basi hao wawili wanaungana na kumuona huyo mtu kama anapotea mbaya.
 
Poleni na majukumu wakuu,. Kama heading inavosema apo kama kweli mungu yupo inabidi aniombe msamaha kwa sababu zifuatazo

Moja: Kama Mungu yupo yupo basi ni wazi kua yeye ndo alopanga maisha ya mwanadam kuanzia kuzaliwa mpaka kufa kwake, hivo basi ata aya magumu ninayopitia ni wazi alipanga yeye iwe hivi aniombe msamaha kwa hili

Mbili:kama kweli yupo basi ni yeye anaeruhusu watu wafe na wengine wazaliwe kwa maana iyo ni yeye ndo aliruhusu ndugu zangu nnaowapenda akiwemo my lovely mother afe, na kwanini aliruhusu afe wakati alijua kua mama angu ndo furaha yangu yeye ndo alienisabaishia hizuni mpaka leo na kwa hili ata aombe msamaha siwezi kumsamehe

Tatu:kwa nini amekua wa kujificha sana au hataki watu wake waujue ukweli kuhusu yeye ina maana mi nnavohangaika kutafuta dini ya kweli yeye hanioni ? aniombe msamaha kwa kweli
Umeshiba ugali tu cheza na mambo mengine sio kuhusisha Mungu,yeye sio mtu afananishi wala hajalibiwi kumbuka imeandikwa usilitaje jinalake bure nakuombea tu a kusamehe ujinga wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mungu hata kama yupo hahisiki na umaskii wako ,mkuu pambana uzuri wote tunauhakika mungu hazuii mapambano yetu hata kama hayabariki vipi
 
Mimi nimemmaindi tu kutokana na sifa yake yakujua yaliyo mbeleni kabla hayajatokea. Kwa sifa hii inamaana alijua kua kivuko cha nyerere kitakuja kuzama lakini hakuzuia akaacha ndugu zetu wapoteze maisha wakati alikua na uwezo wa kuzuia.

Kwasifa hii bora tu asiwe anajua yajayo maana haina umuhimu, yaani unajua yajayo halafu huwezi kuyaepusha mabaya ambayo uliyaona kabla hata hayajatokea

Mimi ninamashaka sana na huyu mungu. Vitabu vyake vinatuambia hakuna linaloshindikana mbele zake, lakini tunaona ameshindwa kutokomeza dhambi pamoja na kumdhibiti shetani.

Tunaambiwa ombeni lolote nanyi mtapewa. Lakini tunaona wachungaji bila sadaka zetu hawaendi toilet, inamaana mungu kashindwa kuwasaidia watumishi wake kuwapatia hitaji lao mpaka wategemee sadaka za waumini ambao wamekua wakihangaika usiku na mchana kutafuta ridhiki kwa jasho kwa ajili ya familia zao?

Mungu huyu aliyekua hana masihala na watenda dhambi wakipindi icho, mpka kufikia hatua ya kuangamiza kizazi cha sodoma na gomora kwa moto. Leo hii america na nchi nyingi za ulaya zimehalarisha ndoa za jinsia moja lakini katulia tu bila kuchukua hatua yoyote.

Sent using unknown device

Qur'an 2:
2_286.gif

286. Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia. (Ombeni Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri. 286
 
Poleni na majukumu wakuu,. Kama heading inavosema apo kama kweli mungu yupo inabidi aniombe msamaha kwa sababu zifuatazo

Moja: Kama Mungu yupo yupo basi ni wazi kua yeye ndo alopanga maisha ya mwanadam kuanzia kuzaliwa mpaka kufa kwake, hivo basi ata aya magumu ninayopitia ni wazi alipanga yeye iwe hivi aniombe msamaha kwa hili

Mbili:kama kweli yupo basi ni yeye anaeruhusu watu wafe na wengine wazaliwe kwa maana iyo ni yeye ndo aliruhusu ndugu zangu nnaowapenda akiwemo my lovely mother afe, na kwanini aliruhusu afe wakati alijua kua mama angu ndo furaha yangu yeye ndo alienisabaishia hizuni mpaka leo na kwa hili ata aombe msamaha siwezi kumsamehe

Tatu:kwa nini amekua wa kujificha sana au hataki watu wake waujue ukweli kuhusu yeye ina maana mi nnavohangaika kutafuta dini ya kweli yeye hanioni ? aniombe msamaha kwa kweli
Daaaaah! 😢😢😢
 
Qur'an 2:
2_286.gif

286. Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia. (Ombeni Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri. 286
mungu wako kaisha zingua iweje akuachie msala wewe?

Sent using unknown device
 
Mosi; Mwenyezi Mungu alikuumba wewe, na anajua kila kitu kuhusu wewe ila hajakupangia. Amekupa akili na utashi wa kutambua mema na mabaya na hivyo kufanya maamuzi sahihi.

Ukiona mambo hayaendi ujue huenda hautumii vizuri akili na utashi aliyokujalia. Lakini, kama kuna magumu unapitia, kwa kiasi kikubwa huenda ni matokeo ya dhambi; ukianza na ile ya wazazi wetu wa kwanza, Adam na Eva.

Pili; pole sana kwa kutokwa na mama. Lakini ujue tu kuwa kifo ni safari kutoka maisha ya hapa duniani kwenda maisha ya Milele huko Mbinguni. Hauna haja ya kumlaumu Mwenyezi Mungu kuhusu hilo. Yeye aliyepanga tuzaliwe kimwili, ndiye aliyepanga pia tufe kimwili, japo roho zetu zitaishi milele.

Tatu; Mwenyezi Mungu hajajificha. Amekuambia umtafute, nawe utamuona. Mwenyezi Mungu anajidhirisha kwetu kila siku. Mtafute, nawe utamuona.

Uwe na wakati mwema mkuu.
Hii inakutosha sina haja ya kuandika ingine, zingatia haya sana utafaulu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali ni je maombi yanaweza kubadilisha mawazo ya mungu? Mungu akikuandikia kua hakupi je ukisali kwa kuomba atakupatia hitaji lako?

Sent using unknown device
Kwanza Mungu hajakuandikia kutokukupa, amesema ombeni nanyi mtapewa, sharti ni kuomba, ukiomba nawe utapewa, usipopewa kwa wakati unaotaka wewe subiri, jua bado anakuandalia kitu chako ulichoomba, na Mungu kwa wema wake kitu unachoomba kama hakikufai hakupi, instead atakupa kitu ambacho kinakufaa na unachostahili kwa hili mm ni shahidi kwenye maisha yangu,, Mungu ni mtakatifu ni msafi ikitaka kumwendea nenda kwa usafi jisafishe kwanza ndipo mtaelewana, hata maswali yooote haya mnayoyauliza dhidi ya Mungu, majibu yapoo, kama kweli una nia ya kutaka kujua usimulize mwanadamu muulize Mungu mwenyewe atakupa majibu, ila mara nyingi wanadamu ni wavivu hakuna anaetaka kufikia level ya kuhojiana na Mungu tunataka miteremko,, hatuki kulipa gharama ya usafi unaotakiwa ili uweze kuzungumza na Mungu, Adam used to talk to God ila alipofanya dhambi tu na kuharibu uhusiano wake na Mungu ndo uchafu ukaingia akashindwa kuongea na Mungu tena kama zamani, ukisoma Biblia vizazi vikapita akatokea mtu mwingine akakiitia jina la Mungu kwa maana nyingi ukatafuta uhusiano na Mungu baada ya mda mrefu kuvunjika kwa Adamu, saaasa huyo mtu ukisoma biblia ndo familia hiyo hyo ya kina Ibrahimu (Ibrahimu used to talk to God) ndo hiyo hiyo inakuja Isaka (aslo was talking to God) inakuja Yakobo, Yusuph, Musa, Haruni,Yuda, nakuendelea mpaka inakutana na familia ambayo Yesu akazaliwa humo, Nachotaka kuelezea maswali yooote tunayoulizana hapa Majibu yapo kwa Mungu mwombe yeye na atakupa majibu yake kama unataka kujua zaidi njoo PM nikupe mwongozo, kinyume na hapo mtaishia kumdhihaki Mungu na kujichotea dhambi na laana, nimempenda yule aliyesema Mungu ametupa akili na utashi uko sahihi kabisa na ndio majibu, Neno linasema mpende Bwana Mungu wako kwa roho yako yote, kwa akili zako zote, kwa moyo wako wote na kwa nguvu zako zote, ukisoma 1yohana 5:3 atukupa maana halisi ya kumpenda Mungu anasema "Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu kwamba tuzishike amri zake wala amri zake si nzito"
Je ulishawahi kufatilia haya kwenye maisha yako na bado ukafeli?? Maswali yote haya mnaulizana majibu yake yapo embu jiweke karibu na Mungu uone kama hatokujibu, wengi humu pamoja na mtoa mada hamuamini Kama Mungu yupo ndo maana hayo majibu mnayoyataka sijui muombwe msamaha havitakaa vije vitokeee sababu huyo Mungu wa kuwapa majibu hamuani kama yupo, hapa mnapotosha wale wenye uelewa mdogo nao wataanza kumkufuru Mungu na dhambi utakua juu yenu,

Mungu anasema hivii, katika
Kumbukumbu ka torati 39:19
Nazishuhudia mbingu na nchi Juu yenu hivi leo , kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana, basi chagua uzima ili uwe hai wewe na uzao wako"
Sasa hapa tumia akili yako Mungu aliyokupa kufanya machaguo, ila Mungu tayari kakupa ushauri kipi cha kuchagua hapo, Mungu sio dikteta hakuchagulii amekupa akili uchague mwenyewe, yeye ni Mungu hataki kukulazimu wewe uchague nini, ukitumia akili yako kumchagua yeye ndipo anafurahi na kutukuka, ila akitumia nguvu zake yeye kukulazimisha umchague yeye hapo inakua anajiabudu na kujitukuza kwasabu nguvu zake ndo zimetumika,

Mungu yupo na Mungu ni halisi sio Hadithi,
Kuna watu wamepitia maisha magumu Mara kumi zaidi ya mtoa Mada lakini wanaishi Kwa Furaha sasa Kwa sababu ya kuamini Mungu yupo na ndio kila kitu Kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatu..... Soma maandiko. Yaaan usome biblia kwelikweli ndo utapata nafasi ya kumjua huyu Mungu ninani.
Ukikaa kaaa ovyoovyo nakubakia kupokea mafundisho ya walimu wakidini HAUTAKAA UMJUE MUNGU NI NANI.

1 na 2 .. Mungu aliumba mwanadamu mkamilifu na ambaye hakunuumbia kifo.
Kwa mujibu wa kitabu cha mwanzo, dhambi ilipoingia Duniani, ndipo Mungu akikweka kifo kama Adhabu ya kutenda dhambi.

Nilijua una maswali magumu.,, ila nashaur ukasome Maandiko.
 
Back
Top Bottom