Tume huru ya uchaguzi bila katiba mpya ni sawa na kuziba mashimo ya panya kwa mikate!
Maana Tanzania uchaguzi ni mfumo sio tume tu.Nguvu ya Rais na wateule wake, polisi, TISS, Jeshi, Tume, Tamisemi na wengineo lazima viangaliwe kwa pamoja kupitia katiba mpya kwa sababu vyote hivi huwa vinahusika na chaguzi zetu.
Hiki kinachoitwa ni Tume huru ya uchaguzi ni changa la macho kwa wajinga ambao ndiyo wengi kwenye hii nchi.
ACT wazalendo ambao ndiyo vinara wa kudai tume huru ya uchaguzi badala ya katiba mpya ni chama pandikizi cha CCM kwa ajili ya kuvuruga maslahi mapana ya demokrasia kwenye nchi hii kwa maslahi ya kuhakikisha kuwa CCM inaendelea kutawala.
View attachment 2159445