Kama kweli tunahitaji kufanyia marekebisho Katiba Mpya, tuanze na tume Huru ya Uchaguzi na kupunguza madaraka ya Rais

Uko sahihi. Tume ya uchaguzi ni mojawapo la zao la katiba.
 
Nchi za kifalme ni tofauti na nchi za kidemokrasia
Sisi tulichagua kuwa nchi ya kidemokrasia ni lazima tufanye kwa vitendo na demokrasia ni kusikiliza na kufanyia kazi matakwa ya wananchi sio kupigania matumbo ya viongozi.

Ofisi ya Chadema inahusikaje na katiba mpya?
Kwani hujui ccm walijenga ofisi zao kwa kodi za wananchi, kuna mwanaccm ameshawahi kuchanga mkajenga ofisi?
Zile ni kodi zetu mmekwapua.

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Yaani katiba nzima mnawaza madaraka ya Rais kama vile ndio yanakwamisha maendeleo ya nchi hii kuna nchi nyingi tu madaraka ya Rais ni makubwa na bado nchi inasonga mbele na pia Rais anaheshimu anaheshimu katiba na vyombo vyake
Madaraka ya rais yanakwamisha maendeleo sana tena sana

Kwanza Rais ana kinga
Hii inamfanya kuwa Mungu mtu yani leo hii hata rais angeua mtu hadharani huna cha kumfanya anaweza kuamua kufanya ufisadi awezavyo na hamuwezi kumuuliza wala kumshtaki kokote
Hii inahamasisha ufisadi lakini pia inampumbaza mtu hawezi kusikiliza yeyote

Pili Rais anateua majaji wa mahakana
Huku ni kuingilia uhuru wa mahakama na kumfanya jaji amtumikie aliyemteua sio wanachi

Tatu rais anateuawabunge (10)
Anateua mawaziri
Anateua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mkurugeznzi halafu anakwenda kugombea
Anateua wakurugenzi amabao ndio wasimamizi wa uchaguzi
Anateua wakuu wa vyombo vya usalama
Anateua wakuu wa wilaya na mikoa

Ni punguani pekee hataweza kuona athari za kiuchumi siasa, kijamii za kumpa madaraka yote haya mtu mmoja halafu bado mnampa na kinga ya kutoshtakiwa.


Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Hili umelijua baada. Ya kuona Raise ni Mama au ni nn?
 
Nimepitia Katiba ya mwaka 2005, binafsi ninaona kama vile hili swala la kurekebisha katiba ni dogo sana kuliko linavyokuzwa na wanasiasa wa upinzani; wamekalia kuwa wanamlalamikia rais ila swala hili limo mikononi mwa wabunge. Kinachotakiwa kwa mujibu wa katiba hiyo ni kwa mbunge yeyote kutumia aya ya 98 ya katiba hiyo kuleta mswada wa kubadilisha katiba ama kwa kutambulisha rasimu iliyotolewa na tume ya Warioba kama katiba kamili ya Jamhuhuri ya Muungano wa Tanzania, au kwa kuandika muswada wake binafsi wa kubadilisha baadhi ya vifungu vya katiba. Bunge linapiga kura, iwapo 2/3 ya wabunge (super majority) watakubaliana na mswada huo basi, mswada utapelekwa kwa Rais, ambaye akishasaini, basi Katiba mypa inaanza. Hakuna mbunge yeyote aliyewahi kutumia kifungu hicho, lakini utakuta wanamlalamikia rais tu.

Hata Lisu mwenyewe kabla hajashambuliwa maisha yake hakuwahi kutumia kifungu hicho cha kaatiba. Rais hana mamlaka ya kubadili katiba, ni bunge tu linaloweza kufanya hivyo. Lawama zitapelekwa kwa raistu iwapo bunge limepitisha mswada, lakini Rais amektaa kuusaini. Ningekuwa mbunge ningeunganisha mswada huo na bajeti ya serikali kiasi kuwa rais asipousaini basi serikali pia inakosa hela.

Lile bunge maalum la katiba halikuwa na mamlaka ya kikatiba kujadilina kubadili katiba kwani katiba hiyo haina kifungu chochote kinachohalalisha uwepo wa bunge maalum la katiba, kile kikao kilikuwa haramu na kilipoteza hela za walipa kodi bure. Ilitakiwa rasimu ijadiliwe na Bunge lililopo kikatiba, na bunge hilo linaweza kufanya hivyo wakati wowote, siyo lazima kuwe na tume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…