Kama kweli unamchukia Hayati Magufuli fanya haya utuachie tunaompenda

Kama kweli unamchukia Hayati Magufuli fanya haya utuachie tunaompenda

Usipite na gari lako Kijazi interchange.

Kwa wanao toka Mbezi kuelekea kariakoo na Posta pitia njia ya Goba au maji chumvi.

Fanya hivyo boss utakua na amani.

Tuache kudharau viongozi wetu tusitukane tuwaheshimu wote.

Kama unaona unakereka na uongozi wa kiongozi yeyote jenga hoja njoo na data kuliko kutukana viongozi njoo na data.

Humpendi lakini bado unajilazimisha kupita kwenye daraja alilosimamia. Huoni kama unajiumiza.
View attachment 3019558
Mkuu kwani alijenga kwa hela yake??? Ilitumika ni kodi yetu, Ala! Wewe vipi?? usitupangie!! Kaanike mahindi huko kwenye uwanja wa ndege Chato!!!

Usilolijua ni kuwa watanzania wengi hawakumchukia yeye binafsi isipokuwa matendo yake ya kikatili Mkuu!!!

Wewe ndiye unayeleta mahaba mbuzi hapa!! Unafiki mtupu!!! Kama vipi kazikwe naye in zito's words!!!
 
Alijenga kwa pesa zetu!
Kwa Tanzania Rais/kiongozi akitumia pesa zetu kwenye maendeleo hiyo ni big step ni bahati kubwa sana
kwasababu wengi wao wanatumia pesa zetu kunenepesha matumbo yao tu!
Mkuu wengi wao akina nani??? Wataje kwa ushahidi ulioona wakinenepesha matumbo yao kwa mshahara wako?!!!

Unapanua mdomo hapa kama kiboko apigaye miayo asubuhi!!!

Kwani Magufuli alikuta nchi hii pori na machaka!! Kwenda huko na unafiki wako!!
 
Leo mtasema yote mnatuletea unafiki hapa. Sijawai kupewa pesa na mtu wala rushwa.
Linapokuja swala la kuusema ukweli lazima tuseme.
Kama humpendi kwanini unapita kwenye daraja alilosimamia huoni kama unaumiza moyo wako.
 
Magufuli ndio alijenga kwa pesa zake ??

Yaani kijana mdogo na msomi umeamua kuwa Lumumba buku 7??

NAMEUBUNGO INTERCHANGE
LENGTH (km)
SIGNING DATE22/02/2017
CONTRACT SUM (Bil)177.42
CONTRACTORCCECC
CONSULTANTDASAN
FINANCIERWORLD BANK
STAGEDesign

Yaani achilia mbali Magufuli mnayemsifia hata sio watanzania waliojenga!

🙋‍♂️✍️📝👍👌👏👊🤝🙏🔊🎁🛡️
 
Shida nini mkuu siku hizi reasoning yako ina plummet? Ni sawa na kusema kwakuwa Nyerere alipinga wakoloni basi akavunje Reli ya kati, akavunje UDSM, akavunje bandari n.k? Ubaya wa JPM ni leadership style sio barabara.

Kwani Mandela kipindi anakataa makaburu hawakuwa wamejenga barabara nchi nzima? Very poor reasoning.

JPM anapingwa kwa udikteta wake kama ambavyo Hitler licha ya maendeleo makubwa aliyowaachia ujerumani, anakumbukwa kwa udikteta wake.
🙋‍♂️✍️📝👍👌👏👊🤝🙏🎁🛡️
 
Kuwa kiongozi imara mwenye mawazo chanya kwa taifa lako hilo ni jambo kubwa sana. Magufuli hapo ndio alikonga nyoyo za Watanzania wengi, na wengi wameona thamani yake baada ya kuondoka, na asilimia kubwa huwa iko hivyo.

Fedha alizo tumia ni za Watanzania kwa ujumla tena nilimsikia akisema fedha zote za mradi huo zimetoka kwa watanzania bila ya kukopa ata shilingi mia moja. Kwahiyo unaona kabisa alisimamia vizuri kuweza kuleta mambo chanya kwenye taifa letu.
Mkuu si ungesoma hiyo document hapo kabla ya kuhoroja hapa!!! Kwani hapo world bank hela yake ni ya sadaka!!!
 
Jiwe ndiyo mtu wa hovyo kuliko wote waliowahi kupewa madaraka ya urais nchi hii:-
1. Alikuwa mporaji, mtekaji, muuaji na mpiga watu risasi.
2. Aliunda kundi la watu wasiojulikana lililokuwa linaua na kuteka watu.
3. Alikuwa muuaji wa uchumi wa nchi kwani alikuwa anapigana kufa kupona ili kuua sekta binafsi
4. Hivyo vidaraja unavyoviita flyover ni ushubwada tu ukilinganisha na mauaji ya watu
5. Alikuwa hapendi demokrasia. Alizima internet siku ya uchaguzi, aliwachukia wapinzani na upinzani na akawafukuza nchini wapinzani. Mshenzi sana yule.

Usinichoshe yanatosha kwa sasa
🙋‍♂️✍️📝👍👌👏👊🤝🙏🎁🛡️
 
"Na Mimi nataka niseme Watanzania mtanikumbuka na mtanikumbuka kwa mazuri na si kwa mabaya kwasababu nimesacrifice maisha yangu kwa wananchi masikini"
Mkuu kama kweli alikuwa na anawapenda masikini hela ya vitambulisho vya machinga masikini wa Mungu alikula ya nini??? Jizi tu lilikuwa!!! Fisadi la kizilankende!!!
 
Kuwa kiongozi imara mwenye mawazo chanya kwa taifa lako hilo ni jambo kubwa sana. Magufuli hapo ndio alikonga nyoyo za Watanzania wengi, na wengi wameona thamani yake baada ya kuondoka, na asilimia kubwa huwa iko hivyo.

Fedha alizo tumia ni za Watanzania kwa ujumla tena nilimsikia akisema fedha zote za mradi huo zimetoka kwa watanzania bila ya kukopa ata shilingi mia moja. Kwahiyo unaona kabisa alisimamia vizuri kuweza kuleta mambo chanya kwenye taifa letu.
🤔🤔🤔
 
Kwahiyo kipindi tunamkejeli kuwa JK alikua fisadi je hakuwa amejenga barabara nchi nzima, hakuwa amejenga terminal 3? Hakuwa ameleta umeme wa gesi au hakuwa amesambaza maji ya ziwa Victoria? Hakuwa amejenga UDOM na mloganzila?

Ubaya wa uongozi hauna uhusiano na miundombinu uliyojenga. Leadership is software rather than hardware
🙋‍♂️✍️📝👍👌👏👊🤝🙏🎁🛡️
 
Watu kama nyie ndio matatizo ya hili Taifa..., Hakuna Mradi wa JPM wala Samia kwahio yoyote aliyefanya vitu kwa Kodi zetu ni kwamba aliwajibika wala hakuna sababu ya kumsifia na anayelaumu analaumu kwa mapungufu aliyofanya sababu ni haki yake kama mlipa Kodi....

Kwahio muda wa kusifia tungekuwa tunautumia kulaumu wasiofanya huenda wangefanya..., By the way sikubaliani na wanaopambana na marehemu wakati kinachoendelea sasa kinawapita....
👏👏👏🛡️
 
Aliyejenga mlima Kilimanjaro, aliyechimba bahari ya Hindi, aliyechimba ziwa Victoria, nyasa na Tanganyika, na kuyakabidhi Kwa wanadamu wa TANGANYIKA, awekwe kundi gani? Acha kusujudia binaadamu, Magufuli hana tofauti yeyote Ile nawewe.
🙋‍♂️✍️📝👍👌👊🤝👏🙏🎁🛡️
 
Nipo nafanya jogging Kijazi Interchange juu kabisa
Mkuu safi sana!!!
 
Usipite na gari lako Kijazi interchange.

Kwa wanao toka Mbezi kuelekea kariakoo na Posta pitia njia ya Goba au maji chumvi.

Fanya hivyo boss utakua na amani.

Tuache kudharau viongozi wetu tusitukane tuwaheshimu wote.

Kama unaona unakereka na uongozi wa kiongozi yeyote jenga hoja njoo na data kuliko kutukana viongozi njoo na data.

Humpendi lakini bado unajilazimisha kupita kwenye daraja alilosimamia. Huoni kama unajiumiza.
View attachment 3019558
Alijenga kwa fedha zake? Acha kulazimisha mambo kama unampenda shauri Yako mfuate
 
Back
Top Bottom