Kama kweli unamchukia Hayati Magufuli fanya haya utuachie tunaompenda

Kama kweli unamchukia Hayati Magufuli fanya haya utuachie tunaompenda

Nililia muda wote tangu alipotangazwa amefariki mpaka kuzikwa kwake, na hata leo ninaporudia kuangalia matukio ya msiba wake, wale wajeda na kina mama, wazee kwa vijana walivyokuwa wakishindwa kujizuia, huwa inanitoa machozi

Nilimkubali sana yule mzee, na hakika yangu, haijatokea kiongozi niliyewahi kumkubali na sijui kama atatokea tena kama yule mzee

Ila Mungu ni mwema, asikie kilio cha wote wanaonyanyasika na mabwanyeye ya CCM
Mkuu pole sana, shida ulikuwa unafurahia maumivu ya wengine, ikawa zamu yako kuonja machungu yao!!! Mtafute ndugai mnaweza kufarijiana!!

Na sasa Somo limeeleweka, hakosei mtu hapa!!! Mwendo ni huu wa kizimkazi!!
 
Uliponunua bidhaa , shilingi kadhaa zilienda kufidia deni la huo mradi hivyo upo sawa kujivunia uliposimama ni kodi yako ila sio kutuletea hadithi za asiyempenda Magufuli asipite hapo.
🙋‍♂️✍️📝👍👌👊🤝👏🙏🛡️
 
Hao uliowaamini kwa pesa zako walifanya nini
Mkuu unaona interchange ya Ubungo ndio kitu cha maana pekee yake kufanywa kwa miaka 60!! Ama kweli ulikula matangopori ya mwenzake ukashiba!!
 
Alijenga kwa pesa zetu!
Kwa Tanzania Rais/kiongozi akitumia pesa zetu kwenye maendeleo hiyo ni big step ni bahati kubwa sana
kwasababu wengi wao wanatumia pesa zetu kunenepesha matumbo yao tu!
Kama sasa hiv.
Toka tumeskia watajenga Flyover Mwenge na morocco ni lini
Pesa zinakopwa lakin Miradi haianzi
 
Kuwa kiongozi imara mwenye mawazo chanya kwa taifa lako hilo ni jambo kubwa sana. Magufuli hapo ndio alikonga nyoyo za Watanzania wengi, na wengi wameona thamani yake baada ya kuondoka, na asilimia kubwa huwa iko hivyo.

Fedha alizo tumia ni za Watanzania kwa ujumla tena nilimsikia akisema fedha zote za mradi huo zimetoka kwa watanzania bila ya kukopa ata shilingi mia moja. Kwahiyo unaona kabisa alisimamia vizuri kuweza kuleta mambo chanya kwenye taifa letu.
Umeisoma hii komenti chini hapa au umeiruka kwa kuwa imeandikwa kwa lugha ngeni huilewi?

Magufuli ndio alijenga kwa pesa zake ??

Yaani kijana mdogo na msomi umeamua kuwa Lumumba buku 7??


NAMEUBUNGO INTERCHANGE
LENGTH (km)
SIGNING DATE22/02/2017
CONTRACT SUM (Bil)177.42
CONTRACTORCCECC
CONSULTANTDASAN
FINANCIERWORLD BANK
STAGEDesign




Yaani achilia mbali Magufuli mnayemsifia hata sio watanzania waliojenga!

 
kodi gani unayolipa wewe mbona hizo kodi hazikufanya kitu awamu nyingine fikiri kabla hapo wewe mwenyewe unajua yule kichwa na hata sasa hakuna kiongozi anatajwa sana kama yeye sababu ziko wazi hata mkulima kule kijijijni anamlilia JPM kwanini tafuta jibu hapa kazi tuu.
Mkuu una uhakika kodi haikuwahi kufanya chochote awamu zote ila ilimsubiri Mwendazake ndio ikafanya kazi!!

Mkuu umefikia hatua hii ya ufikiri??? Kuna jambo haliko sawa sawa kwako!!
 
Typical JPM follower, unashindwa kusoma unabaki kujibu kwa hisia.

Nilichosema ni kwamba Wajerumani walifanya maendeleo makubwa sana hapa ila tuliwapinga sio sababu ya miundombinu ila UONGOZI.

Same to Hitler, aliikuta nchi ni maskini kuliko most Ulaya ila ikageuka kuwa top 5 economy ndani ya miaka 5 pekee!! Ila je waliompinga Hitler ni sababu ya mafanikio yake kiuchumi au sababu ya udikteta?

Mfano wa mwisho, Makaburu Afrika kusini waliifanya Sauzi hadi iwe ina vinu vya nuclear na uchumi ulikua juu kuliko alipopewa mtu mweusi. Swali ni je kama issue ni miundombinu pekee kulikua na sababu gani Mandela kumpinga Kaburu?

Uongozi ni zaidi ya miundombinu. Hata JK licha ya kuitwa fisadi ila alijenga miundombinu ikiwemo mwendokasi, lami mikoa yote, umeme wa gesi, mlonganzila , Udom n.k ila bado tulimpinga
🙋‍♂️✍️📝👊🤝👏👌👍🙏🎁💐🗼🎖️🏆👑🔊🎧🎶🎵
 
Wanasiasa uchwara? Mbona alikumbatia mafisadi yaliyotajwa na ripoti ya makinikia? Vipi ripoti ya Bashiru kuhusu majizi wa mali za CCM kuna aliyekamatwa hadi leo?

JPM alijua kuwachota nyie wajinga tu.

Alafu ulivyo mpumbavu unasema wapinzani hawana faida cha ajabu huyo JPM wenu alikua anawapa wapinzani ubunge wakihamia CCM. Bila kusahau mawaziri na manaibu waziri 7 katika utawala wake walikua wametoka directly Chadema.

Kama hawafai kwanini aliwapa uwaziri walipohamia CCM? embicile
Mkuu watu walipumbazwa wakapumbazika. Tuwaelimishe taratibu wataelewa tu!!!
 
Ndiyo aliwasimamia vizuri na hela zilitumika vizuri kufanya kazi.angalia sasa hivi kila waziri ni wapigaji na miradi zinadoda na watu wanapiga hela ovyoovyo alafu mnacheka tu.Magufuli alikuwa msimamizi mzuri sana
Mkuu kilicho muondoa Kangi Lugola uwaziri ni nini??? Sio ufisadi, kilikuwa kipindi gani, acha uongo wako!! Peleka mahaba yako huko chato kaburini Pake, kwa katili mwenzio!!
 
Wajinga kama nyie na wenye vyeti feki na mafisadi lazima muone hivyo mkiambiwa wekeni evidence ya hela iliyoibiwa hamuwezi.aliwabana sana mafisadi na wapenda Magendo ndo maana mambo yalikuwa yanaenda.
Mkuu acha kuruka mada, tulia hakuna mwenye vyeti Feki hapa.

Magufuli mwenyewe unayemhusudu alikuwa na cheti cha PhD Feki.

Tuliza mshono usirukeruke kama bisibisi Mkuu, jibu hoja hii.

Je, Magufuli kajenga interchange ya Ubungo kwa hela yake yaani mshahara wake au kwa mkopo wa world bank????
 
Hiyo miundombinu sio mali ya magufuli. Imejengwa na kodi za watanzania. Yeye kuwa rais haifanyi hizo ziwe mali yake, halihalalishi ukatili uliotendeka yeye akiwa kiranja mkuu na akafumbia macho, na wala sio kigezo cha kupendwa. Kumbuka akiwa kwenye hiyo ajira ya urais tulimlipa mshahara, na hakuna chochote alichofanya kinaweza kuwa hisani. Yeye mwenyewe hakuwa na upendo. Pia tofautisha kati ya kutukana na kuelezea tabia/ubinadamu wa magufuli.
Mkuu Nziiri jr, umesummarize kwa weledi sana. Umeeleweka vizuri sana. Big up Mkuu!!!
 
Hiyo miundombinu sio mali ya magufuli. Imejengwa na kodi za watanzania. Yeye kuwa rais haifanyi hizo ziwe mali yake, halihalalishi ukatili uliotendeka yeye akiwa kiranja mkuu na akafumbia macho, na wala sio kigezo cha kupendwa. Kumbuka akiwa kwenye hiyo ajira ya urais tulimlipa mshahara, na hakuna chochote alichofanya kinaweza kuwa hisani. Yeye mwenyewe hakuwa na upendo. Pia tofautisha kati ya kutukana na kuelezea tabia/ubinadamu wa magufuli.
🙋‍♂️✍️📝👊🤝👏👌👍🙏🎁💐🗼🛡️
 
Binafisi huwa naamini ni heri ufanye jambo hata kama hautalifanya kwa usahihi kuliko kutokulifanya kabisa...kikubwa na cha muhimu uwe umeonesha nia ya dhati kabisa kwenye jambo hilo.

Magufuli alivyofichua sakata la Makinikia na madudu mengine mengi yaliyokuwa yakiendelea kwenye sekta mbali mbali za uma kama watumishi hewa,mishaara hewa,ukwepaji kodi n.k wengi tulimuona ni shujaa haijalishi hata kama alikabiliana na mambo hayo kwa namna ambayo sio sahihi, ila kitendo tu cha yeye kuonesha uthubutu inamfanya kuwa kuwa kipekee.
Mkuu kila Rais alifanya udhubutu kwa utashi, wakati, mazingira yake na hali ya uchumi ya wakati huo.

Magufuli alitumia polisi iliyoletwa na Nyerere, Alitumia ma land cruiser yaliyoletwa na Mwinyi, Alitumia TRA, Takukuru na Tume ya madawa ya kulevya zilizoletwa na mkapa!!!

Hakuna Rais ambaye hakupiga vita rushwa, madawa ya kulevya, uzembe au vihiyo kazini, wote walipambana kwa nyakati zao.

Huwezi kutumia kainterchange uchwara kamoja kudiscredit kazi nzuri na za msingi za Marais wote 4 waliopita!!!

Huu ni upunguani wa kiwango kisicho mithilika Mkuu!
 
Magufuli ni kama maji,
Usipoyanywa utayaoga !
Alama zake ni nyingi sana Nchini 🙏
Mkuu ni kweli alama zake za maumivu zimetamalaki kote nchi, sio tu kwa wanafunzi, hata wastaafu, walimu, watumishi wa umma, wakulima, wafanyabiashara, wapinzani, wawekezaji!!! Sijui kama ulimaanisha alama hizi za maumivu au???
 
Back
Top Bottom