Kama kweli Yesu aliteseka msalabani kwaajili yetu ili tusamehewe dhambi zetu, sisi tunatubu ili iweje?

Kama kweli Yesu aliteseka msalabani kwaajili yetu ili tusamehewe dhambi zetu, sisi tunatubu ili iweje?

Nawasalimu Salam ya wakati huu.

Kiukweli kabisa Mimi hili suala mpaka kesho sijawahi kulielewa,

Kama tunaambiwa kwamba dhambi zetu yesu alizimaliza msalabani sasa kwanini watu wanalia na kusaga meno kila siku wasamehewe dhambi zao?

Je, kuna makundi ya dhambi zilizosamehewa na ambazo bado ama?

Na kwanini kwenye kutubu lazima waanze kusema nisamehe Mimi mwenye dhambi?

Mwenye kunielewesha karibu sana.
Chai

Yesu hakuwahi kuteseka kwa dhambi ya mtu yeyote.
 
Niongeze swali hapo

Ikiwa Mungu ndiye aijuaye kesho ya kila alichokiumba, hakujua kama shetani angekuja kwenda kinyume na matakwa yake asimuumbe? Na kwa nini baada ya kuasi kwa huyo shetani asingemuua ili hiki kiumbe kiitwacho binadamu kisije pata adha naye?
 
Niongeze swali hapo

Ikiwa Mungu ndiye aijuaye kesho ya kila alichokiumba, hakujua kama shetani angekuja kwenda kinyume na matakwa yake asimuumbe? Na kwa nini baada ya kuasi kwa huyo shetani asingemuua ili hiki kiumbe kiitwacho binadamu kisije pata adha naye?


Haha
 
Nawasalimu Salam ya wakati huu.

Kiukweli kabisa Mimi hili suala mpaka kesho sijawahi kulielewa,

Kama tunaambiwa kwamba dhambi zetu yesu alizimaliza msalabani sasa kwanini watu wanalia na kusaga meno kila siku wasamehewe dhambi zao?

Je, kuna makundi ya dhambi zilizosamehewa na ambazo bado ama?

Na kwanini kwenye kutubu lazima waanze kusema nisamehe Mimi mwenye dhambi?

Mwenye kunielewesha karibu sana.
Kwa hiyo waliiokolewa ni hawa warumi weusi, wasabato, walokolole au jamii ya akina nabii tito;


View: https://youtu.be/6dcvuGot1UA?si=-u_PsbHH9mWdC4fJ
 
Nawasalimu Salam ya wakati huu.

Kiukweli kabisa Mimi hili suala mpaka kesho sijawahi kulielewa,

Kama tunaambiwa kwamba dhambi zetu yesu alizimaliza msalabani sasa kwanini watu wanalia na kusaga meno kila siku wasamehewe dhambi zao?

Je, kuna makundi ya dhambi zilizosamehewa na ambazo bado ama?

Na kwanini kwenye kutubu lazima waanze kusema nisamehe Mimi mwenye dhambi?

Mwenye kunielewesha karibu sana.
Suala hili hata mimi sijawahi kulielewa kabisa.

Bahati mbaya hata uzi huu na michango yake kibao umeshindwa kutuelimisha tusioelewa zaidi ya vitisho tu. Hii inaonesha hakuna majibu ya kueleweka. Kwenye imani kuna maswali huwa hayana majibu, ndo maana atheists kama Kiranga huwa wanajiondokea na points tatu zao muhimu.
 
Vipi na wale watu walioishi na kufa kabla yesu hajazaliwa. Na wao dhambi zao zimefutwa na yesu msalabani ?
Watahukumiwa kwa dhamira zao. Maana mwanadamu kaumbwa na kitu kinaitwa dhamili inayomshuhudia ndani yake kuwa atendalo ni jema au baya.
 
Suala hili hata mimi sijawahi kulielewa kabisa.

Bahati mbaya hata uzi huu na michango yake kibao umeshindwa kutuelimisha tusioelewa zaidi ya vitisho tu. Hii inaonesha hakuna majibu ya kueleweka. Kwenye imani kuna maswali huwa hayana majibu, ndo maana atheists kama Kiranga huwa wanajiondokea na points tatu zao muhi
Ili upate msamaha wa dhambi lazima umkiri Yesu. Ni sawa na kusema kwa kwa nini kupiga kura wakati wagombea wako tayari si mmoja awe rais tu?. Ukisoma Warumi 10:4-12 Kwa maana Kristo ndiye mwisho wa Sheria, ili kila mtu aliye na imani awe na uadilifu. 5 Kwa kuwa Musa anaandika hivi kuhusu uadilifu kupitia Sheria: “Mtu anayefanya mambo hayo ataishi kupitia mambo hayo.” 6 Lakini uadilifu unaotokana na imani husema: “Usiseme moyoni mwako, ‘Ni nani atakayepanda juu mbinguni?’ yaani, kumleta Kristo chini, 7 au, ‘Ni nani atakayeshuka katika shimo?’ yaani, kumleta Kristo juu kutoka kwa wafu.” 8 Lakini linasema nini? “Neno hilo liko karibu nawe, katika kinywa chako na katika moyo wako mwenyewe”; yaani, “neno” la imani, ambalo sisi tunahubiri. 9 Kwa maana ukitangaza waziwazi kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana, na kuwa na imani moyoni mwakokwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokolewa. 10 Kwa sababu kwa moyo mtu huwa na imani ili apate uadilifu, lakini kwa kinywa mtu hufanya tangazo la hadharani ili apate wokovu. 11 Kwa kuwa andiko linasema: “Yeyote anayemwamini hatakata tamaa.” 12 Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki. Kuna Bwana yuleyule juu ya wote, aliye tajiri kwa wote wanaomwitia. 13 Kwa maana “kila mtu anayeliitia jina la Yehova ataokolewa.” 14 Hata hivyo, watawezaje kumwitia ikiwa hawajamwamini? Nao watamwaminije yule ambaye hawajamsikia? Nao watasikiaje bila mtu wa kuhubiri? 15 Nao watahubirije isipokuwa wawewametumwa? Kama ilivyoandikwa: “Jinsi inavyopendeza miguu ya wale wanaotangaza habari njema ya mambo mema!” 16 Hata hivyo, si wote waliotii habari njema. Kwa maana Isaya anasema: “Yehova, ni nani ambaye ameamini jambo alilosikia kutoka kwetu?” 17 Kwa hiyo imani hufuata jambo lililosikiwa. Nalo jambo lililosikiwa ni kupitia neno kumhusu Kristo. 18 Lakin.
 
Ni kweli kuwa Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu baada anguko la Adamu na Hawa katika bustani Edeni. Kabla ya kujaribiwa na Ibilisi au Shetani, Mungu alimpa mwanadamu uwezo wa kuchagua kumpenda na kumtii yaani kuchagua mema na mabaya au uzima na mauti.

Katika kitabu Mwanzo 2,:16-17 Bwana Mungu akamwagiza huyu mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika. Na katika kitabu Kumbukumbu ya Torati 30:19 tunakutana katazo hilo Nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana.

Lakini Mwanzo 3 tunaona mwanadamu akiacha maagizo akamsikiliza Shetani "Ati hivi ndivyo alivyosema Mungu, msile matunda ya miti yote ya Bustani? "(Mwa 3:1). Mwanamke alimwambia Shetani matunda ya miti ya bustanini waweza kula ispokuwa mti ulio katikati ya bustanini wasile. Tunamwona Shetani akiendelea kumwambia Hawa kwamba wasingekufa. Hilo kosa kubwa lilosababisha anguko ya kutoyatii maagizo ya Mungu. Anguko hilo lilisababisha kufukuzwa bustanini na aliaandaa mpango mpya wa kumkomboa mwandamu atoke katika dhambi kwa kusema kwamba uzao wa mwanamke ungemponda Shetani (Mwa 3:15).

Uzao wa mwanamke ni Yesu Kristo aliyezaliwa na Mariamu. Katika Yohana 3:16 tunasoma kwamba Mungu aliupenda Ulimwengu hata akamtoa Mwanae wa pekee. Akasema pia amwaminiye yeye hakumiwi, asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. Kwa hiyo kosa kubwa ambalo wanadamu watahukumiwa nalo ni kuukataa msamaha ambao Mungu ameutoa kwa kupitia Yesu Kristo pale Msalabani.

Njia pekee kwako kwa sasa ni kuubali msamaha huo yaani kuokoka na kumpokea Bwana Yesu ili awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako.
 
Umaana na umuhimu wa kuungama na kutubu dhambi zetu umetokana na ukweli huo haswa kwamba Kristu alikufa msalabani.

Bila tukio la Kalvari, hata mwanadamu angelia machozi na kujigaragaza majivuni akiyaomboleza maovu yake, bado angeonekana mwenye hatia ileile mbele ya Mungu.

Hii ndiyo kusema kwamba Yesu alikufa ili kutununulia muda na uwezekano mwingine wa kutubu na kufanyika upya watoto watiifu wa Mungu.

Na haya yote hayatokei kwa juhudi zetu tu, bali nguvu za Mungu hushirikiana na nafsi yenye utashi ili kumwongoza hatua kwa hatua kutoka kwenye umateka na mitego ya Ibilisi hadi kwenye jukwaa la uhuru na uzima wa milele.

Msalabani Kalvari ndipo mahali makhususi ambapo mwanadamu anaweza kutambua lengo kamili la uumbaji na thamani yake kwa kuzingatia umbali ambao Mungu yuko radhi kwenda ili kumrejesha Kwake.
Mfalme Daudi pia alimtenda Mwenyezi Mungu dhambi.... Akaungama akasamehewa, Waisrael walimtenda Mwenyezi Mungu dhambi wakatubu wakasamehewa, watu wa Ninawi kipindi cha Yona walisamehewa pia!!!

Swali n kwamba... Kama Mungu akiombwa msamaha anasamehe Yesu kufa kwake msalaban kwaajili ya dhambi inafaida gani ikiwa bado tunaendelea kutubu Kama zamani🤔🤔🤔

Ilitakiwa kwasasa tufanye dhambi free sabb dhambi zetu kishazibeba yeye🚶🚶
 
H
Hahahahah, ilinitokea Mimi Kuna magroup Facebook nilifuatilia yanahusu mambo ya kukosoa Mambo ya Mungu nikaamua niondoke nilianza kuhisi kupotea hivi na nikaona kama naanza kuhama reli. Nikablock makundi yote.

Mfano alihoji kwa ukubwa wa Safina aliyotengeneza Nuhu na vitu vilivyoingia ndani ni haiwezekani pamoja na stock ya chakula Chao. Maana Dunia ina Species milioni 6 na, Sasa piga Wawili Wawili na chakula Chao, zingatia Hali ya hewa na habitats zao, je waliishije na walitoshaje humo?

Pia akadai kwamba Kijiografia uMvua haiwei kunyesha ikagharikisha sehemu zote za Ardhi ya Dunia.

Ila ninavyoona Mimi hivi vitu ni Imani na ni unquestionable wewe amini Kisichowezekana kwa Binadamu kwa Mungu Kinawezekana.
Hilo group bila shaka ni.... Kundalin awakening 😂😂
Nimo humo
 
Bora walau wewe umejua kwamba Yesu alikufa kwa ajikl yetu; wenzako kila kukicha kiguu na njia kwa manabii kununia chumvi, maji na mafuta.
 
Nawasalimu Salam ya wakati huu.

Kiukweli kabisa Mimi hili suala mpaka kesho sijawahi kulielewa,

Kama tunaambiwa kwamba dhambi zetu yesu alizimaliza msalabani sasa kwanini watu wanalia na kusaga meno kila siku wasamehewe dhambi zao?

Je, kuna makundi ya dhambi zilizosamehewa na ambazo bado ama?

Na kwanini kwenye kutubu lazima waanze kusema nisamehe Mimi mwenye dhambi?

Mwenye kunielewesha karibu sana.
Kutubu maana yeke ni kugeuka kutoka dhambi na kujikita kwenye kutenda mema. Ni sawa na kusema kama Yesu amefanyika njia ya kutoka matopeni kwanini tunatoka matopeni.
 
Jifungie mahali peke yako! Muite YESU mwenyewe kwa utulivu muulize hilo swali hakika utapata majibu
 
Hudhuria vipindi vyote vya mafundisho kanisani utapata majibu yote ya maswali yako.

Kumbuka mafundisho kama hayo hayapatikani kwa urahisi kwenye makanisa yanayouza maji, chumvi, n.k

Kwa sasa unataka ulishwe ugali wakati unastahili upate uji, (mafundisho laini).
[emoji120]
Wakati Yesu anateswa msalabani alianguka mara tatu na kila alipokuwa akianguka alinyanyuka tena na kuendelea na safari ya mateso. Inatufundisha nini kwa Yesu kuanguka na kunyanyuka mara 3? Tunaanguka kwenye dhambi mara nying na tunapoanguka hatuna budi kutubu na kuwa karibu na Mungu. Hivyo basi pamoja na kwamba yesu alibeba dhambi zetu kwa kuteswa msalabani sisi wanadamu bado tunaanguka kwenye dhambi na tunapoanguka kwenye dhambi yatubidi kutubu. Na huko ndiko kunyanyuka kutoka kwenye dhambi na kutubu.
 
Back
Top Bottom