Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
Tabia ya Mungu au niseme utaratibu wa Mungu ni kwamba ukitenda dhambi lazima ufe, damu imwagike kabisa. zamani hizo wanadamu wakitenda dhambi ilitakiwa wamwage damu walau ya mnyama, kwa niaba ya dhambi ile waliyoitenda. meaning, ukitenda leo utamwaga damu na ile damu inahudu dhambi hiyo tu, haihusu dhambi utakazofanya keshokutwa au mwakani, hizo zitahitaji umwagaji damu wake. waisrael wamekuwa wakimwaga damu za kondoo, mbuzi, ng'ombe, na njiwa kwa namna hiyo kwa ajili ya upatanishi, ama la wao ndio wangekufa. mnyama unayetoa sadaka hiyo ya dhambi alitakiwa awe msafi, asiye na madoadoa wala uchafu wowote.Nawasalimu Salam ya wakati huu.
Kiukweli kabisa Mimi hili suala mpaka kesho sijawahi kulielewa,
Kama tunaambiwa kwamba dhambi zetu yesu alizimaliza msalabani sasa kwanini watu wanalia na kusaga meno kila siku wasamehewe dhambi zao?
Je, kuna makundi ya dhambi zilizosamehewa na ambazo bado ama?
Na kwanini kwenye kutubu lazima waanze kusema nisamehe Mimi mwenye dhambi?
Mwenye kunielewesha karibu sana.
katika Agano Jipya, Mungu akaleta utaratibu mpya, ipatikane Damu ya mtu ambaye hana hatia kabisa yaani hajawahi kutenda dhambi, mtakatifu na msafi, ili afe kama sadaka ya kuchukua dhambi badala ya ng'ombe na mbuzi kuchinjwa kama sadaka. hakuna mwanadamu yeyote wa kawaida ambaye angeiweza hiyo kazi kwasababu wanadamu woote wana asili ya udhaifu wa dhambi, hata wale wanadamu waliopaa mbinguni kama kina Eliya, walishatendaga dhambi. hivyo, Mungu yeye mwenyewe akafanyika mwili (akaingia kwenye mwili wa mwanadamu ili auvae mwili huo kwa kuzaliwa kama mwanadamu), aishi kama mwanadamu, asitende dhambi yeyote, na asiwe na mbegu (sperm) ya mwanadamu ili Damu isiwe ya kibinadamu bali Damu ya Kimungu, aishi maisha ya kibinadamu, ashinde dhambi zote, halafu auawe kama kafara la dhambi za wanadamu wote. huyo ndiye Yesu Kristo aliyezaliwa pale Bethlehem.
kwa kifo chake, ukitenda dhambi, badala ya kuchinja ng'ombe, unatubu kwa kumwamini yeye, unasamehewa bila gharama yeyote nyingine, imani tu. wapo wachungaji manabii wa uongo wamejitokeza siku hizi wanasema kwasababu Yesu alikufa, hatutakiwi kutubu tena na watenda dhambi hawataenda motoni kwasababu Yesu aliichukua dhambi yetu yote. NO, ukitubu leo Yesu anakusamehe dhambi uliyotubu, ukitenda dhambi kesho baada ya kutubu, hiyo mpya haitasamehewa hadi utubu na kuacha, ama la utaenda nayo motono.
kwahiyo, kile kitendo chetu cha kutubu kwa specific dhambi, ni sawa na kwenda zizini na kuchagua mnyama wa kuchinja badala ya dhambi uliyoitenda. Yesu alichinjwa badala yako hivyo ukitubu kwa Jina lake, unasamehewa specific dhambi uliyotubu. hausamehewi zile utakazotenda kesho na keshokutwa, ndio maana kutubu kutakuwepo kila siku, unapaswa kujitakasa kila siku ukijua mwanadamu ana madhaifu kila iitwapo leo.
na sio dhambi tu, Yesu Kristo aliyachukua hata magonjwa yetu, aibu yetu na huzuni zetu. Isaya 52 na 53 inaeleza kwamba, jinsi alivyoishi awali, alikuwa mtu anayedhaniwa ni dhaifu, aliyedharauliwa hadi watu walitema mate wakimwona, alikuwa mtu wa huzuni nyingi mno na masikitiko, Yesu hakuishi maisha ya furaha. kwa kifupi, ili wale watakaomwamini waishi maisha ya furaha, yeye alibeba huzuni/aliishi maisha ya huzuni muda wote na masikitiko, aliposulibiwa aliumizwa mwili kwa mijeledi na kipigo ili kwa kupigwa kwake sisi tupone miili yetu isipate maumivu, hata tukipata anao uwezo kuyaondoa kwasababu aliyashinda na alilipa garama hiyo, alimwaga damu ili kwa Damu yake iwe kafara la dhambi za dunia nzima, meaning, yeyote ulimwenguni akija kwake kumwamini na kutubu, dhambi yake inalipika/inasameheka kwasababu alilipa deni la dhambi yeyote itakayofanywa na wanadamu wowote wale waliokuwepo na walioendelea kuzaliwa, deni lililipwa.
usijichanganye tunaposema Yesu alilipa deni, hii haimaanishi deni lilishalipwa hivyo tufanye tu dhambi hatutaadhibiwa kwasababu alilipa, NO, inamaanisha, ukifanya dhambi, badala ya kugarimia ng'ombe au kondoo, yeye alishamwaga Damu yake badala ya mang'ombe na makondoo, atakusafidha dhambi yako (ile tu unayotubu sio zile za kesho na keshokutwa hizo zitahitaji kutubu kupya).
na hakuna njia nyingine ya kusamehewa dhambi, wanadamu wote wasiopitia njia hii wataenda motoni moja kwa moja, meaning, waislam,wabudha na kadhalika wote imani yao haitawaokoa, ni watu wa motoni.