Kama kweli Yesu aliteseka msalabani kwaajili yetu ili tusamehewe dhambi zetu, sisi tunatubu ili iweje?

Kama kweli Yesu aliteseka msalabani kwaajili yetu ili tusamehewe dhambi zetu, sisi tunatubu ili iweje?

Hizi story na thread za kuhusu mambo ya Mungu kadri ya ninavyozisoma na kuzitafakari zinanifanya napoteza imani yangu kwa Mungu wangu. Nataka niache kuzisoma ili niendelee kumtukuza kama nilivyofundishwa tangu utotoni.
National kabisa nikiwa nasali nakosa utulivu na kumaanisha sababu ya hizi mada 🤔🤔🤔
Hahahahah, ilinitokea Mimi Kuna magroup Facebook nilifuatilia yanahusu mambo ya kukosoa Mambo ya Mungu nikaamua niondoke nilianza kuhisi kupotea hivi na nikaona kama naanza kuhama reli. Nikablock makundi yote.

Mfano alihoji kwa ukubwa wa Safina aliyotengeneza Nuhu na vitu vilivyoingia ndani ni haiwezekani pamoja na stock ya chakula Chao. Maana Dunia ina Species milioni 6 na, Sasa piga Wawili Wawili na chakula Chao, zingatia Hali ya hewa na habitats zao, je waliishije na walitoshaje humo?

Pia akadai kwamba Kijiografia uMvua haiwei kunyesha ikagharikisha sehemu zote za Ardhi ya Dunia.

Ila ninavyoona Mimi hivi vitu ni Imani na ni unquestionable wewe amini Kisichowezekana kwa Binadamu kwa Mungu Kinawezekana.
 
Nawasalimu Salam ya wakati huu.

Kiukweli kabisa Mimi hili suala mpaka kesho sijawahi kulielewa,

Kama tunaambiwa kwamba dhambi zetu yesu alizimaliza msalabani sasa kwanini watu wanalia na kusaga meno kila siku wasamehewe dhambi zao?

Je, kuna makundi ya dhambi zilizosamehewa na ambazo bado ama?

Na kwanini kwenye kutubu lazima waanze kusema nisamehe Mimi mwenye dhambi?

Mwenye kunielewesha karibu sana.
Hivi tangu dunia hii imeumbwa mafundisho ndivyo yanatuelekeza na watu tunaelewa. Nikuulize wewe ndugu hivi kwamba ndiyo una akili sana kwa dhihaka kwenye imani. Usiandike tu kisa una afya njema na kuona unaweza kila kitu.
 
Hizi story na thread za kuhusu mambo ya Mungu kadri ya ninavyozisoma na kuzitafakari zinanifanya napoteza imani yangu kwa Mungu wangu.

Nataka niache kuzisoma ili niendelee kumtukuza kama nilivyofundishwa tangu utotoni.

National kabisa nikiwa nasali nakosa utulivu na kumaanisha sababu ya hizi mada 🤔🤔🤔
Kabisaa mkuu
 
Nawasalimu Salam ya wakati huu.

Kiukweli kabisa Mimi hili suala mpaka kesho sijawahi kulielewa,

Kama tunaambiwa kwamba dhambi zetu yesu alizimaliza msalabani sasa kwanini watu wanalia na kusaga meno kila siku wasamehewe dhambi zao?

Je, kuna makundi ya dhambi zilizosamehewa na ambazo bado ama?

Na kwanini kwenye kutubu lazima waanze kusema nisamehe Mimi mwenye dhambi?

Mwenye kunielewesha karibu sana.
Jibu sahihi hili hapa
hakufa Wala hakusurubiwa

Quran 4:157
- Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini.
 
.
 
Nawasalimu Salam ya wakati huu.

Kiukweli kabisa Mimi hili suala mpaka kesho sijawahi kulielewa,

Kama tunaambiwa kwamba dhambi zetu yesu alizimaliza msalabani sasa kwanini watu wanalia na kusaga meno kila siku wasamehewe dhambi zao?

Je, kuna makundi ya dhambi zilizosamehewa na ambazo bado ama?

Na kwanini kwenye kutubu lazima waanze kusema nisamehe Mimi mwenye dhambi?

Mwenye kunielewesha karibu sana.
Ni suala la Imani, ukiamini umesamehewa milele na alizichukuwa hizo dhambi basi wewe hauna dhambi na hauna haja ya kutubu, yaani unatubu nini sasa wakati dhambi ziliisha chukuliwa 🤣🤣🤣
Kuna raha sana haya mambo ukiyajua, yani huwezi kupiga kiboya na matapeli kina kiboko ya wachawi
Injili ya Yohana 1:29 siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake akasema,Tazama Mwana kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.
 
Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

Warumi 10:9
 
Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.

Mithali 28:13
 
Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;

Matendo Ya Mitume 3:19
 
Hudhuria vipindi vyote vya mafundisho kanisani utapata majibu yote ya maswali yako.

Kumbuka mafundisho kama hayo hayapatikani kwa urahisi kwenye makanisa yanayouza maji, chumvi, n.k

Kwa sasa unataka ulishwe ugali wakati unastahili upate uji, (mafundisho laini).
[emoji120]
Mpe hayo mafundisho hapa,
Au ni rocket science??
 
Back
Top Bottom