Kama kweli Yesu aliteseka msalabani kwaajili yetu ili tusamehewe dhambi zetu, sisi tunatubu ili iweje?

Chai

Yesu hakuwahi kuteseka kwa dhambi ya mtu yeyote.
 
Niongeze swali hapo

Ikiwa Mungu ndiye aijuaye kesho ya kila alichokiumba, hakujua kama shetani angekuja kwenda kinyume na matakwa yake asimuumbe? Na kwa nini baada ya kuasi kwa huyo shetani asingemuua ili hiki kiumbe kiitwacho binadamu kisije pata adha naye?
 


Haha
 
Kwa hiyo waliiokolewa ni hawa warumi weusi, wasabato, walokolole au jamii ya akina nabii tito;


View: https://youtu.be/6dcvuGot1UA?si=-u_PsbHH9mWdC4fJ
 
Suala hili hata mimi sijawahi kulielewa kabisa.

Bahati mbaya hata uzi huu na michango yake kibao umeshindwa kutuelimisha tusioelewa zaidi ya vitisho tu. Hii inaonesha hakuna majibu ya kueleweka. Kwenye imani kuna maswali huwa hayana majibu, ndo maana atheists kama Kiranga huwa wanajiondokea na points tatu zao muhimu.
 
Vipi na wale watu walioishi na kufa kabla yesu hajazaliwa. Na wao dhambi zao zimefutwa na yesu msalabani ?
Watahukumiwa kwa dhamira zao. Maana mwanadamu kaumbwa na kitu kinaitwa dhamili inayomshuhudia ndani yake kuwa atendalo ni jema au baya.
 
Ili upate msamaha wa dhambi lazima umkiri Yesu. Ni sawa na kusema kwa kwa nini kupiga kura wakati wagombea wako tayari si mmoja awe rais tu?. Ukisoma Warumi 10:4-12 Kwa maana Kristo ndiye mwisho wa Sheria, ili kila mtu aliye na imani awe na uadilifu. 5 Kwa kuwa Musa anaandika hivi kuhusu uadilifu kupitia Sheria: “Mtu anayefanya mambo hayo ataishi kupitia mambo hayo.” 6 Lakini uadilifu unaotokana na imani husema: “Usiseme moyoni mwako, ‘Ni nani atakayepanda juu mbinguni?’ yaani, kumleta Kristo chini, 7 au, ‘Ni nani atakayeshuka katika shimo?’ yaani, kumleta Kristo juu kutoka kwa wafu.” 8 Lakini linasema nini? “Neno hilo liko karibu nawe, katika kinywa chako na katika moyo wako mwenyewe”; yaani, “neno” la imani, ambalo sisi tunahubiri. 9 Kwa maana ukitangaza waziwazi kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana, na kuwa na imani moyoni mwakokwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokolewa. 10 Kwa sababu kwa moyo mtu huwa na imani ili apate uadilifu, lakini kwa kinywa mtu hufanya tangazo la hadharani ili apate wokovu. 11 Kwa kuwa andiko linasema: “Yeyote anayemwamini hatakata tamaa.” 12 Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki. Kuna Bwana yuleyule juu ya wote, aliye tajiri kwa wote wanaomwitia. 13 Kwa maana “kila mtu anayeliitia jina la Yehova ataokolewa.” 14 Hata hivyo, watawezaje kumwitia ikiwa hawajamwamini? Nao watamwaminije yule ambaye hawajamsikia? Nao watasikiaje bila mtu wa kuhubiri? 15 Nao watahubirije isipokuwa wawewametumwa? Kama ilivyoandikwa: “Jinsi inavyopendeza miguu ya wale wanaotangaza habari njema ya mambo mema!” 16 Hata hivyo, si wote waliotii habari njema. Kwa maana Isaya anasema: “Yehova, ni nani ambaye ameamini jambo alilosikia kutoka kwetu?” 17 Kwa hiyo imani hufuata jambo lililosikiwa. Nalo jambo lililosikiwa ni kupitia neno kumhusu Kristo. 18 Lakin.
 
Ni kweli kuwa Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu baada anguko la Adamu na Hawa katika bustani Edeni. Kabla ya kujaribiwa na Ibilisi au Shetani, Mungu alimpa mwanadamu uwezo wa kuchagua kumpenda na kumtii yaani kuchagua mema na mabaya au uzima na mauti.

Katika kitabu Mwanzo 2,:16-17 Bwana Mungu akamwagiza huyu mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika. Na katika kitabu Kumbukumbu ya Torati 30:19 tunakutana katazo hilo Nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana.

Lakini Mwanzo 3 tunaona mwanadamu akiacha maagizo akamsikiliza Shetani "Ati hivi ndivyo alivyosema Mungu, msile matunda ya miti yote ya Bustani? "(Mwa 3:1). Mwanamke alimwambia Shetani matunda ya miti ya bustanini waweza kula ispokuwa mti ulio katikati ya bustanini wasile. Tunamwona Shetani akiendelea kumwambia Hawa kwamba wasingekufa. Hilo kosa kubwa lilosababisha anguko ya kutoyatii maagizo ya Mungu. Anguko hilo lilisababisha kufukuzwa bustanini na aliaandaa mpango mpya wa kumkomboa mwandamu atoke katika dhambi kwa kusema kwamba uzao wa mwanamke ungemponda Shetani (Mwa 3:15).

Uzao wa mwanamke ni Yesu Kristo aliyezaliwa na Mariamu. Katika Yohana 3:16 tunasoma kwamba Mungu aliupenda Ulimwengu hata akamtoa Mwanae wa pekee. Akasema pia amwaminiye yeye hakumiwi, asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. Kwa hiyo kosa kubwa ambalo wanadamu watahukumiwa nalo ni kuukataa msamaha ambao Mungu ameutoa kwa kupitia Yesu Kristo pale Msalabani.

Njia pekee kwako kwa sasa ni kuubali msamaha huo yaani kuokoka na kumpokea Bwana Yesu ili awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako.
 
Mfalme Daudi pia alimtenda Mwenyezi Mungu dhambi.... Akaungama akasamehewa, Waisrael walimtenda Mwenyezi Mungu dhambi wakatubu wakasamehewa, watu wa Ninawi kipindi cha Yona walisamehewa pia!!!

Swali n kwamba... Kama Mungu akiombwa msamaha anasamehe Yesu kufa kwake msalaban kwaajili ya dhambi inafaida gani ikiwa bado tunaendelea kutubu Kama zamani🤔🤔🤔

Ilitakiwa kwasasa tufanye dhambi free sabb dhambi zetu kishazibeba yeye🚶🚶
 
H
Hilo group bila shaka ni.... Kundalin awakening 😂😂
Nimo humo
 
Bora walau wewe umejua kwamba Yesu alikufa kwa ajikl yetu; wenzako kila kukicha kiguu na njia kwa manabii kununia chumvi, maji na mafuta.
 
Kutubu maana yeke ni kugeuka kutoka dhambi na kujikita kwenye kutenda mema. Ni sawa na kusema kama Yesu amefanyika njia ya kutoka matopeni kwanini tunatoka matopeni.
 
Jifungie mahali peke yako! Muite YESU mwenyewe kwa utulivu muulize hilo swali hakika utapata majibu
 
Wakati Yesu anateswa msalabani alianguka mara tatu na kila alipokuwa akianguka alinyanyuka tena na kuendelea na safari ya mateso. Inatufundisha nini kwa Yesu kuanguka na kunyanyuka mara 3? Tunaanguka kwenye dhambi mara nying na tunapoanguka hatuna budi kutubu na kuwa karibu na Mungu. Hivyo basi pamoja na kwamba yesu alibeba dhambi zetu kwa kuteswa msalabani sisi wanadamu bado tunaanguka kwenye dhambi na tunapoanguka kwenye dhambi yatubidi kutubu. Na huko ndiko kunyanyuka kutoka kwenye dhambi na kutubu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…