Kama lengo la chama cha siasa ni kushika madaraka, kwa sasa CCM ndiyo chama chenye mafanikio zaidi Afrika?

Kama lengo la chama cha siasa ni kushika madaraka, kwa sasa CCM ndiyo chama chenye mafanikio zaidi Afrika?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Nimesikia mara nyingi sana viongozi, hasa viongozi wa vyama vya upinzani wakisema kuwa lengo kuu la chama cha siasa ni kushika madaraka. Maana yake chama kikishika madaraka kinakuwa kimetimiza lengo lake kuu. Na kikiyashika kwa muda mrefu zaidi ndivyo kinavyokuwa kimetimiza lengo lake kuu kwa mafanikio zaidi.

Sasa kwa vyama vilivyopo madarakani Afrika Nzima, CCM ndicho chama kilichokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi. Na katika historia nzima ya Afrika ni chama cha pili kwa kutawala muda mrefu. Hilo haliifanyi CCM kuwa chama chenye mafanikio zaidi Afrika? Kitu gani kimefanya CCM ifikie mafanikio hayo? Vyama vingi vya aina yake vimeishapotea siasani. Tena vingine vikiwa na nguvu kubwa sana ya dola nyuma yake lakini vimeanguka. Nini siri ya mafanikio haya makubwa ya CCM?
 
𝐍𝐚 𝐦𝐚𝐟𝐚𝐧𝐢𝐤𝐢𝐨 𝐲𝐞𝐧𝐲𝐞𝐰𝐞 𝐧𝐢 𝐤𝐮𝐭𝐮𝐦𝐢𝐚 𝐧𝐠𝐮𝐯𝐮 𝐲𝐚 𝐯𝐲𝐨𝐦𝐛𝐨 𝐯𝐲𝐚 𝐮𝐬𝐚𝐥𝐚𝐦𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐡𝐢𝐧𝐝𝐢 𝐤𝐢𝐥𝐚 𝐜𝐡𝐚𝐠𝐮𝐳𝐢 .
 
Uongozi bora siasa na umoja ndani ya chama kubwa makofii tafadhali pwah pwah pwah.......
 
Back
Top Bottom