lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
Sababu mama ni kuwa Katiba mpya ndio Tiba ya matatizo yote ya Tz,kama ilivyoelezwa kwenye rasimu ya Jaji Warioba na mama alikua Mwenyekiti wa Bunge la katiba anajua zaidi yangu faida za katiba mpya.
Ila tatizo lililopo ni CCM kutaka kuendelea kutawala hata kama hawana ridhaa za wananchi, na makada wa CCM wenye ndoto mbalimbali za kugombea nafasi mbalimbali za uongoz wa taifa hili.
CCM na hao makada hawako tayari kwa Katiba mpya kwa sababu za kibinadamu tu,na wala sio kwa maslahi ya Taifa. Hivyo kwa muktadha huo wako tayari kufanya lolote,narudia tena kufanya lolote Ili kukwamisha mpango wa kuleta katiba mpya. Na wako tayari kumfanya mtu yoyote kitu chochote Ili kumzuia asilete katiba mpya. Kwa hali hiyo suala la katiba mpya ni kaa la moto kwa kiongozi yoyote atakae onesha kusudio la kuileta.
Sasa sababu zangu kwa nini asiogope kuruhusu katiba mpya:
Kwa sasa hivi kuna watu ndani ya chama chake wanamawazo mabaya na yeye,wanamfikiria vibaya na inawezekana wakawa wanapanga njama ovu dhidi yake.
Wapo walioanzisha shule ya uongozi na wapo wanaolaumu kukopa,wakati miezi kadhaa tu aliekuwepo alikua anakopa.wapo wengi wa hivi.
Sasa kwa Katiba hii mbovu wakifanikiwa kufanya yao,tutaweza kurudi kulekukue kwa one man show. Na kwa kutumia katiba hii hii mbovu Mama wanaweza kumuweka pabaya.
Kwa sababu tu alikwenda kinyume na baadhi ya mambo ya Bwana yule au genge lake. Hivyo basi Ili kupata Kinga ya hayo,katiba mpya ndio itakua Kinga yake.
Katiba mpya inahitajika na kutamaniwa na vyombo vote vya Ulinzi na Usalama,yaani Jw,polisi,Usalama,magereza nk. Inawafanya wafanye Kazi zao kwa weledi bila kuingiliwa au kutumwa au kushinikizwa na makada. Ikumbukwe hivi vyombo vina wataalamu waliojifunza mambo ya Ulinzi na Usalama na kubobea. Hivyo wanapolazimishwa kutenda mambo fulani kinyume na taaluma zao na wanasiasa au makada inawakera sana.
Katiba inahitajika na Majaji,mahakimu na wanasheria,
Hawa huwa hawapendi kuelekezwa kufanya mambo kinyume na Sheria,
Wanahabari wanaihitaji katiba mpya,Hawa wakikuandika kwa kukulinda utalindwa,
Utawekwa kwenye kumbukumbu kama shujaa wa Taifa.
Katiba mpya inahitajika na wananchi wengi kwa mamilioni wa kila fani,hivyo mama akiruhusu atakua amechagua kuwa upande wa watu wengi,nao watampa Kinga ya hali ya juu mno, nguvu ya uma,maombi na heshima.hakuna mtu atamgusa.
Ukipigania haki utaungwa mkono ndani na nje.
Hapa mama atapata heshima inayoambatana na Ulinzi kutoka ndani na hata Jumuiya ya kimataifa.hakuna atakae jaribu kumfanya kitu.
Viongozi wa dini.
Hapa atakua ana uhakika wa Kinga ya maombi.
Wazee wastaafu watambariki na kumpa heshima. Alieruhusu katiba mpya alikua Kikwete,alieweka mizengwe alikua Mkapa.
Mkapa alikuja kuona umuhimu wa katiba mpya baadae,akatamani angalau tu kwanza waanze kurekebisha Tume ya Uchaguzi lakini ndoto zake zikazimwa na kifo.
Kikwete hana tatizo na katiba,Mzee Ruksa hana tatizo,Jaji Warioba ,Butiku na wazee wengine hawana tatizo na katiba,hivyo Mama atapata Kinga itokanayo na baraka za wazee. Hakuna atakae mfanya kitu.
Mama atakumbukwa kwa miaka nenda miaka rudi,na atatajwa kwa heshima na upendo kuwa aliruhusu jambo ambalo ilikua linaliliwa na makundi ya watu.
Katiba sio hitajio la chadema Katiba ni hitajio la Taifa,ni hitajio la, wakulima, wafanyakazi, dini, vijana, wanawake, wataalamu, wanajeshi, wanausalama, mapolisi, wabunge, madiwani na kila aina ya kada.
Akiruhusu katiba mpya atakua Rais wa pili Tanzania kuheshimika baada ya Nyerere,hivyo atakua ameweka legasi isiyo ya kutafuta.atakumbukwa kama mtu alieleta faraja kwa watanzania.
Mambo ni mengi jamani mama ajilipue tu,aongee kwanza na Mkuu wa Jw,Mkuu Wa TIss na Mkuu wa polisi,awaambie kusudio lake la kujilipua,wampe Ulinzi dhidi ya mahafidhina wa CCm Kisha apulize kipenga.
Baada ya hapo hata akitembea njiani bila mlinzi sisi Raia tutamlinda kila aendapo.