LGE2024 Kama lile ndio Daftari la kujiandikisha kupiga kura, Professor Assad yuko Sahihi kuwa hatapiga kura

LGE2024 Kama lile ndio Daftari la kujiandikisha kupiga kura, Professor Assad yuko Sahihi kuwa hatapiga kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mwenyewe nilienda jumapili nilishangaa sana.
Niliwauliza vitu gani nahitaji kuwa navyo iliniweze kujiandikisha, nikaambiwa huhitajiki chochote zaidi ya wewe mwenyewe na majina yako.
Nikauliza utathibitisha vipi kama haya ni majina yangu wakasema sio lazima kuthibitisha muhimu niweke saini yangu.

Sijajua kwanini wameondoa kipengele cha kadi ya mpiga kura ila naona ni udhaifu au inafanyika bora liende.
 
Hata mimi nimejiandikisha juzi. Makarani hawanijui wala mimi siwajui, hawakuniuliza chochote mbali na majina matatu na umri. Nikaona kabisa naweza kwenda kujiandikisha mtaa mwingine tena. Kuna uwezekano mkubwa wa daftari kujaa majina ya kubumba.

Sintapiga kura.
Aliyedizaini hili daftari alaaniwe yeye na Watoto na ukoo wake na vizazi vyake
 
Mwenyewe nilienda jumapili nilishangaa sana.
Niliwauliza vitu gani nahitaji kuwa navyo iliniweze kujiandikisha, nikaambiwa huhitajiki chochote zaidi ya wewe mwenyewe na majina yako.
Nikauliza utathibitisha vipi kama haya ni majina yangu wakasema sio lazima kuthibitisha muhimu niweke saini yangu.

Sijajua kwanini wameondoa kipengele cha kadi ya mpiga kura ila naona ni udhaifu au inafanyika bora liende.
Ndio matokeo ya kuweka siasa kwenye kila kitu
 
H ha hahahaha aaa! Mkuu najaribu kuwa objective ili tueweze kusonga mbele, Mkuu. Tukisusa watakula wao tu! Tunatakiwa kula wote njia ya kufanikisha hili ni kushiriki sote kwa umoja wetu kushughulikia masuala yetu kama nchi.
===
Wakuu Asubuhi njema, sitaweza kuendelea kujibu hoja kwa Sasa hadi wakati mwingine. Mbarikiwe.
Nimekuelewa vizuri, nimejiandikisha nitapiga Kura
 
Nilipo nimemsikia kiazi(mjumbe) wa eneo letu akipayuka kwa jazba akijaribu kuwatisha watu kwamba watafuatilia wale wote wasiokwenda kujiandikisha na hatimaye kupiga kura basi watakapohitaji huduma za wenyeviti wa mitaa hawatowahudumia! Binafsi naona wanazidi kuchanganyikiwa na mgomo wa watu kutokwenda kujiandikisha kwenye daftari lao la mchongo.
 
Inaumiza Sana sana
 
hata mm mtaani sijulikani naweza kujiandikisha sehemu zaidi ya moja
 
Unakwenda kupiga kura sehemu unapojulikana! Tunajuana Mtaani!
Ulitaka utumike utaratibu upi?
Njia Rahisi na uhakika ni kujipanga mbele ya mgombea unayemtaka! Kwanza hiyo, ingepunguza gharama nyingi za uchaguzi!
Wewe unawajua wote mtaani kwako? Unamjua kila mtu mtaani kwako?

Watanzania sijui nani katuloga. Tunaishi kizamani hadi mtu unashangaa. Anyways sio uzamani ni namna ya ccm kushinda.

Sijui lini tutaamka watanzania! Kila kitu kiko wazi kabisa ila tunafanyana wajinga tu
 
Jana nilienda kujiandikiasha ili kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa. Nikakuta kumbe unataja majina yako matatu, unaweka sahihi, msimamizi nae anaweka sahihi halafu ndio imetoka hivyo.

Yaani Nikajiuliza na kucheka tu, ni Watu wangapi wataingizwa ambao ni fake? Waandaaji wameshindwaje hata kutumia akili za kawaida Tu nyingine kuchukua tahadhari ya Watu wasiostahili kutokuingizwa au kuandikwa?

Kwa muktadha huu, Watu WA CCM wataenda kujifungia na hili daftari na kuandika majina yoyote kwa idadi yoyote ile na HAKUNA kitu kitatokea.

Nishauri Tu kuwa, ni muhimu sana kutumia akili zetu KULIKO SIASA kwenye kitu muhimu kama hiki.
Daftari gani huulizwi hata unaishi wapi, huulizwi kitambulisho, huulizwi taarifa zozote zile zaidi ya kutaja jina na kusaini?

Leo nitaenda kujiandikisha kituo kingine tena na nitawapa mrejesho na mniambie kama kuna umuhimu WA uchaguzi wa kipumbavu namna hii.

Pia soma:
LGE2024 - Uzi Maalum wa Kasoro na Rafu kwenye zoezi zima la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Prof. Assad: Sitapiga tena kura labda mfumo uwe wa kidigitali
hata akiacha kura yake ni moja tu ,tuna watanzania miloni 60 kwahiyo hata akiwaambia na nduguzake wote wasipige kura haina shida
 
Vile vishikwambi vya sensa ilitakiwa vihifadhiwe vitumike katika mambo kama haya,katika zama hizi wanatumia daftari wakati ni suala la kuunda database na mfumo wa uandikishaji kidigitali,ni mbinu tu
 
Back
Top Bottom