LGE2024 Kama lile ndio Daftari la kujiandikisha kupiga kura, Professor Assad yuko Sahihi kuwa hatapiga kura

LGE2024 Kama lile ndio Daftari la kujiandikisha kupiga kura, Professor Assad yuko Sahihi kuwa hatapiga kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kuna wengine bature ya kazi zao ni za kutembea mitaa mbalimbali, leo yuko hapa kesho yuko pale na sio rahisi kujua exactly ni mtaa upi anaishi.
Huyu anaweza kujiandikisha hata mitaa kumi kama ndio iko hivyo.
 
Ukipitia comments za baadhi yetu humu ndani unagundua watu wanashindwa kutofautisha kati ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambao uandikishaji wa wapiga kura ndo unaondelea sasa na unasimamiwa na Tamisemi na uchaguzi mkuu (wa madiwani, wabunge na Rais) unaosomamiwa na Tume "huru"
ya uchaguzi ambao mchakato wake ni hapo mwakani
kwanini chaguzi zote zisisimamiwe na tume huru ya uchaguzi wakati ndo kazi yake
 
Na kuna ile mtaa mmoja kuna sehemu kadhaa za kujiandisha, au ile mitaa iliyokaribiana sana na vituo vipo karibu karibu.

Kama hawatumii mfumo wowote wa kompyuta basi hiyo wakulungwa husema ni kazi ya "kunkuna pusi kufyima"
 
Nina biashara yangu mtaa x na ninaishi mtaa mwingine b, kote nimejiandikisha kupiga kura
 
Jana nilienda kujiandikiasha ili kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa. Nikakuta kumbe unataja majina yako matatu, unaweka sahihi, msimamizi nae anaweka sahihi halafu ndio imetoka hivyo.

Yaani Nikajiuliza na kucheka tu, ni Watu wangapi wataingizwa ambao ni fake? Waandaaji wameshindwaje hata kutumia akili za kawaida Tu nyingine kuchukua tahadhari ya Watu wasiostahili kutokuingizwa au kuandikwa?

Kwa muktadha huu, Watu WA CCM wataenda kujifungia na hili daftari na kuandika majina yoyote kwa idadi yoyote ile na HAKUNA kitu kitatokea.

Nishauri Tu kuwa, ni muhimu sana kutumia akili zetu KULIKO SIASA kwenye kitu muhimu kama hiki.
.
Daftari gani huulizwi hata unaishi wapi, huulizwi kitambulisho, huulizwi taarifa zozote zile zaidi ya kutaja jina na kusaini?

Leo nitaenda kujiandikisha kituo kingine tena na nitawapa mrejesho na mniambie kama kuna umuhimu WA uchaguzi wa kipumbavu namna hii
Halafu hilo daftari wameliprint hapo kiuta. Wakiona kura hazitoshi wanaprint mengine wanajaza kura na kijipigia
 
Leo nikijiandikalisha Juma nikakaa siku tatu nikaenda nikajiandikisha kama John? inakuaje hapo?
Ikitokea hivyo, hao mawakala namuandikishaji watakuwa wameshindwa kazi. Pia na wewe uliyefanya Kitendo hicho huna tofauti na fisadi mwenye tamaa ya fisi na huitakii mema Tanzania. Kwa utatakiwa upewe ushauri nasaha juu ya tabia yako usiporekebika watatafuta sheria na miongozo wakuweke sawa kwa haki.
 
Mimi nilienda na kadi yangu ya kupigia kura nikakuta kule ni majina matatu, umri na kusign tu. Hamna mahali pa kuhakikisha mtu ana miaka 18+. Lazima kutakua ma uchakachuaji
 
Ndomana tunasema huu uchaguzi kushiriki ni ujuha tu

Ova
Muhimu kushiriki na kulinda kura ili kuepuka kulalamika baadae. Inabid wanaogombea wawaweke wasimamizi imara na wanao ogopeka
 
Neno hili! Lakini, wanasema pale unachangia maendeleo ya Mtaani na Wala hakuna kiwango. Mambo haya, inabidi tushiriki vikao vya Mtaani tupate ufafanuzi.
Hizo sio hela za maendeleo ni hela za kuingia mifukoni mwao sababu hawapokei kwa utaratibu maalumu kama kutoa Control number tulipie.

Kapige kura then turudi kusota wote
 
Unajua kuna namna ya kupinga kitu kwa njia ya kukipotezea kama njia ya mezani na haki imeshindwa kufanya kazi.
CCM ndiyo wanataka hivyo, nadhani tushiriki kwa wingi na kuwadhibiti kwa njia zote ikiwezekana hata kwa kutumia waganga wa jadi
 
Back
Top Bottom