Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Kweli Dunia ina maajabu yake,kweli kuna watu wana matatizo sana vichwani Mwao,kweli kuna watu hawajitambui,kweli kuna watu wana uwezo mdogo sana wa kufikiri na kupambanua mambo.
inasikitisha ,kushangaza na kufikirisha sana kwa mtu mwenye akili Timamu na anayejitambua kama Mimi naposikia makelele na mayowe ya Wafuasi kiduchu wa lissu mitandaoni.
Wafuasi wa Lissu walikuwa wakiongea kwa Madaha na kujibetua midomo kuwa lissu anakubalika na ana ushawishi kwa CHADEMA na wakamtaka agombee Uenyekiti wa CHADEMA Taifa badala ya Umakamu Kama alivyokuwa anataka Mwenyewe.
Lakini cha kuchangaza walikuwa hawataki na kuogopa sana kuona au kusikia Mwamba akichukua Fomu ya Uenyekiti kutetea nafasi hiyo. Ambayo hata hivyo ni Kiu ya wengi na mahitaji ya wana CHADEMA wengi ambao ndio wanahitaji Mwamba Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti.
Sasa mwenye akili Timamu unajiuliza maswali machache kati ya mengi kuwa kama Lissu Anakubalika na ana ushawishi na anaaminika na wana CHADEMA.
Sasa kwanini wanaogopa Lissu kupambana na Mwamba kwenye sanduku la Kura? Kwanini walikuwa hawataki Mwamba agombee ilihali wana amini mtu wao atamshinda Mwamba? Kwanini hawataki sanduku la kura liamue Mshindi? Kwanini wanataka mtu wao apite kimserereko kama jiwe lililoanguka kutoka juu? Kwanini wanaogopa mtu wao kushindana kwa hoja na sera na Mwamba Mbowe na hatimaye wajumbe waamue wa kuwaongoza.?
Nini maana ya Demokrasia? Kwanini hawataki demokrasia iamue mshindi? Kwanini wasijivunie kuwa mtu wao lissu atapita kwa kishindo Kikuu badala yake tunaona vilio na kwikwi za majonzi baada ya Mwamba kutangaza Kugombea? Kwanini wanataka vya kunyonga na siyo vya kuchinja? Kwanini wanataka Lissu arithishwe uenyekiti badala ya kuchaguliwa kwa sera na hoja dhidi ya Mwamba?
Kwanini inakuwa hivyo?hofu inatoka wapi? Kiwewe cha nini? Mayowe ya nini? Makelele ya nini? Kwanini wanataka ushindi wa mezani? Kwanini? Jibu ni kuwa Wafuasi wake kiduchu wa Lissu siyo wajinga ,siyo kwamba hawana akili kabisa.
Jibu ni kwa kuwa wao wenyewe kwa ufahamu wao wanatambua ya kuwa lissu hakubaliki ndani ya chama,hana ushawishi,haungwi mkono na wengi,hawezi kuiongoza CHADEMA,hawezi kupata kura za ndio hata robo tu ya wajumbe,hawezi kuungwa mkono na viongozi wenye kujitambua na wenye uchungu na CHADEMA na ustawi wake.
Wafuasi wake wanatambua ya kuwa lissu ni mropokaji, mkurupukaji na mwenye tamaa ,uchu na uroho mkubwa wa madaraka. Ndio maana hata katika nafasi hii ya kuonba Uenyekiti amekurupuka na kukurupushwa tu maana hata awali aliseme hawezi na hana mpango wa kugombea uwenyekiti wa CHADEMA.
Wafuasi wake wanajua ukweli huu na ndio maana hofu imewajaa na kukata tamaa kabisa.ndio maana hakuna mfuasi wake yeyote yule mwenye ujasiri wa kutamka hadharani kuwa Lissu atamshinda Mwamba kwa kura .badala yake utawasikia wakilalamika kuwa kwanini Mwamba Amegombea . Utafikiri kiti cha uenyekiti ni cha mapokezano na kurithishana kama uchifu au mikoba ya uganga wa kienyeji au uchawi.
Kila mtu ashinde mechi zake Mwenyewe na kwa sera zake Mwenyewe na siyo kuanza kupiga mayowe hapa. Lissu Aache kuhangaika na kuongea ongea hovyo hovyo na uzushi na uongo.yeye asubirie Ujumbe wa wajumbe kwenye sanduku la kura ambao wengine tayari wameshaanza kutuma kabisa kuwa wapo upande wa Mwamba na wanasimama na Mwamba mpaka Dakika ya Mwisho.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.