Kama Lissu angekuwepo huu udhalimu dhidi ya Mbowe usingetendeka

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Lissu ni defence lawyer mzuri anajua njama zote za polisi na waendesha mashitaka.

Lissu angewapiga maswali mazito mawakili wa serikali wasiojitambua na mashahidi wa uongo na Jamhuri ingeumbuka.

Kwani watu walioacha kazi jeshi la wananchi yaani JWTz kuomba kazi ya kumlinda mtu ni kosa?

Hii kesi ipo kwa ajili ya kukimaliza chama chetu cha CHADEMA.
 
Lissu ni defence lawyer mzuri anajua njama zote za polisi na waendesha mashitaka...
Lisu alikuwepo hapa na Mbowe kila siku alikuwa hakosi mahakamani, wanasheria wanasiasa wanapenda Sana kesi ndio mtaji wao mkubwa

USSR
 
Wahafidhina waliopo ndani ya chama tawala wamepoteza dira na muelekeo. Silaha pekee iliyobakia kwao ni kutumia vibaya vyombo vya dola ili kuzidi kuahirisha "CCM natural death".

Chama tawala kinaonyesha dalili zote za kuwa maiti mtarajiwa, ndiyo maana kinafanya kila aina ya hila na kuwabambikizia viongozi wakuu wa vyama vya upinzani.

Uwepo wa kesi za kizushi zenye uelekeo wa kijinga jinga kama ya kina Mbowe ni jitihada ya kuviondoa vyama makini vya ushindani kutoka katika reli. Hata kama Lissu angalikuwapo hapa nchini pengine naye angeunganishwa katika kesi hii ya ugaidi wa ajabu wa gharama ya shilingi laki sita!
 
Kwani kafukuzwa nchini? Mbona wakati wa kampeni ameishi nchini kwa miezi mitatu huku akijichanganya hadi kwenye mwendojasi.
 
Baada ya kampeni kuisha mkafanyaje?Lissu alikuwa calculated,alijua hawezi kukamatwa akiwa mgombea Urais ila uchaguzi ukiisha tu angeshughulikiwa!

Uzuri tayari alikuwa ameshapewa taarifa hivyo akakimbilia ubalozini!Huku nje dola ikimtolea macho,ikawa inamfuatilia mpaka airport kama fisi anavyosubiri mkono uanguke!

Mngemgusa akiwa chini ya Balozi wa ujerumani ndio mngejua,shwain!
 
Baada ya kampeni kuisha mkafanyaje?Lissu alikuwa calculated,alijua hawezi kukamatwa akiwa mgombea Urais ila uchaguzi ukiisha tu angeshughulikiwa...
Serikali ingemhitaji ingemkamata muda wowote. Isipokuwa alichofanya lissu ni kucheza na akili za nyie wachache msiojielewa, ili apate nafasi ya kuondoka bila nyie wafuasi wake kuhoji maana hadi familia yake alishaiamishia ubelgiji ambako wanakula, kusoma na kulala bure.

Unadhani hao ujerumani hawajui kama nchi ina taratibu na sheria zake? Au unadhani serikali ya Magu ilikuwa inawaogopa hao watu?
 
Kwani kafukuzwa nchini? Mbona wakati wa kampeni ameishi nchini kwa miezi mitatu huku akijichanganya hadi kwenye mwendojasi.
Baada ya kampeni kuisha mkafanyaje?Lissu alikuwa calculated,alijua hawezi kukamatwa akiwa mgombea Urais ila uchaguzi ukiisha tu angeshughulikiwa!Uzuri tayari alikuwa ameshapewa taarifa hivyo akakimbilia ubalozini!Huku nje dola ikimtolea macho,ikawa inamfuatilia mpaka airport kama fisi anavyosubiri mkono uanguke!
Mngemgusa akiwa chini ya Balozi wa ujerumani ndio mngejua,shwain!
Serikali ingemhitaji ingemkamata muda wowote. Isipokuwa alichofanya lissu ni kucheza na akili za nyie wachache msiojielewa, ili apate nafasi ya kuondoka bila nyie wafuasi wake kuhoji maana hadi familia yake alishaiamishia ubelgiji ambako wanakula, kusoma na kulala bure.

Unadhani hao ujerumani hawajui kama nchi ina taratibu na sheria zake? Au unadhani serikali ya Magu ilikuwa inawaogopa hao watu?
Tuliona jinsi polisi walivyokuwa wanamsubiri nje ya Geti la ubalozi!Balozi akaona isiwe kazi,akamsindikiza yeye mwenyewe mpaka airport!Mngevamia basi huo msafara kama mna mbavu,shwain!
Serikali ilishindwa kumkamata wakati wa kampeni kwani ingejichafua na kuwekewa vikwazo vyenye mbinyo mkali!Wakategesha uchaguzi ukiisha,kumbe kuna masnitch humo humo yakampa infoz Lissu,Lissu akawala chenga ya mwili!
Juzi tu hapa ndio DPP anajifanya kumfutia kesi😁😁😁!
 
Baada ya kampeni kuisha mkafanyaje?Lissu alikuwa calculated,alijua hawezi kukamatwa akiwa mgombea Urais ila uchaguzi ukiisha tu angeshughulikiwa!Uzuri tayari alikuwa ameshapewa taarifa hivyo akakimbilia ubalozini!Huku nje dola ikimtolea macho,ikawa inamfuatilia mpaka airport kama fisi anavyosubiri mkono uanguke!
Mngemgusa akiwa chini ya Balozi wa ujerumani ndio mngejua,shwain!

Tuliona jinsi polisi walivyokuwa wanamsubiri nje ya Geti la ubalozi!Balozi akaona isiwe kazi,akamsindikiza yeye mwenyewe mpaka airport!Mngevamia basi huo msafara kama mna mbavu,shwain!
Serikali ilishindwa kumkamata wakati wa kampeni kwani ingejichafua na kuwekewa vikwazo vyenye mbinyo mkali!Wakategesha uchaguzi ukiisha,kumbe kuna masnitch humo humo yakampa infoz Lissu,Lissu akawala chenga ya mwili!
Juzi tu hapa ndio DPP anajifanya kumfutia kesi[emoji16][emoji16][emoji16]!
Wangemshika basi siku mliyompokea airport pale. Ye kama mwanasheria anaogopaje sheria.? Ndio ilikuwa nafasi nzuri ya kuonyesha umahiri wake. Haya sasa amefutiwa kesi arudi basi mzee wa miga.
 
Unaonesha umahiri wako wa kisheria wakati mmetengeneza loop holes za kuwaweka watu ndani bila dhamana?Kesi ikikaribia mwisho,unasikia DPP anasema,"sina nia ya kuendelea na kesi",shwain!
Suala la kurudi au kutokurudi ni uamuzi wake na intel zake!
 
Basi atulie tu huko ughaibuni. Aache kelele sasa.
 
Unampangiaje cha kufanya?Apige kelele au asipige ni uamuzi wake,huna haki ya kuingilia uhuru wake!
Akikukera acha kifuatilia makelele yake!
 
Back
Top Bottom