Kama maandamano Chadema yamewezekana chini yake. Ni uthibitisho wa uwezo wake KTK kutenda haki. Hata ile haki kuu pia ataitenda. Tuvute tu subra!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Kitu chanye nguvu kuliko kitu chochote duniani ni imani!, faith, ukiamini unafungulia milango ya nguvu fulani zilizoko ndani yako zinazoitwa "will power" ni nguvu za nafsi ambazo zina uwezo wa kufanya kila kitu.

Wengi imani zetu tuezielekeza kwenye imani za dini kwa kuamini Mungu, lakini imani ya kweli iko ndani yako kwasababu binadamu wote wana UMungu ndani yao, na hata Yesu alipokuwa anafanya Miujiza, aliwaambia watu "ni imani yako ndio imekuponya"

Imani hiyo sio lazima iwe ni imani ya Mungu Baba, The Almighty God, hata Allah, hata Yesu, hata Mtume, hata Buddha, hata Mizimu, hata Mlima, hata Mti, hata Jiwe, hata chochote unachoamini, alimradi unaamini, then imani yako itatenda!

Sala yetu ya kuliombea Bunge, huwa tunasema "Mungu ndio huweka serikali za mataifa" hivyo hata marais, Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia, wote ni chaguo la Mungu kwa Tanzania!.

Hivyo mimi nina Imani kubwa sana na Rais Samia kuwa ana uwezo wa kuleta haki zote zilizoporwa Tanzania, ikiwemo kutuletea katiba mpya!

Imani kwenye kitu haichipuki tuu kama uyoga, au kudondoka kama love at first sight, Wasukuma tunaita "Moyo wangu umekudondokea", imani inajengwa kwa kuainishwa kisha ndipo unaamini.

Humu JF kuna mtindo, ukimsifu kiongozi Mkuu wa nchi, unanyooshewa vidole vya tuhuma za kufanya uchawa, hivyo nikisema mimi nina imani na Rais Samia kuwa anaweza, naomba niwatembeze kidogo, huyu Samia, nilianza nae wapi na nilianza nae lini, ili mwisho wa siku nikisema namuaminia, uujue msingi wa imani yangu.

The same applies to urais wa Samia, hakuna mtu yoyote alijua kuwa kuna siku rais wa JMT anaweza kufa akiwa madarakani!, hivyo siku zote Makamo wa rais alikuwa anateuliwa tuu bila kumhesabia anaweza kuja kuwa rais wa JMT kwasababu hakuna aliyewahi kufikiri rais wetu anaweza kufa!

Hivyo naamini hata wakati Samia ni Makamo wa JPM, hakuwahi kuwaza kuwa kuna siku JPM anaweza kuitwa kwa Baba yake na yeye kuwa rais wa JMT!, hivyo ilivyotokea JPM akaitwa kwa Baba yake na Samia kuwa rais wa JMT, watu wote wanajua imejitokea tuu, ni mipango ya Mungu, ukweli ni kwamba hakuna kitu chochote kinachotokea tuu, wala hakuna bahati mbaya, everything that happens ni kilikuwa kitokee, it's a pre meditate move, kuna watu wenye powers wamewezesha, walitoa kauli zenye nguvu ya kuumba, waliomuomba Mungu, wakamuumbia Samia urais wa JMT ili Samia awe rais na kweli Mungu akasikia hizo kauli, zikamuumbia Samia urais, ndio Samia akawa rais hivyo usikute hata Samia mwenyewe hafahamu wala hajui kuwa huo urais wake alionao, kuna watu waliousababisha kwa kauli umba, zikamuumbia urais akawa rais bila yeye kujua, huku yeye anajihesabu amekuwa rais wa JMT kwa kudra tuu za Mwenyeenzi Mungu, kumbe hajui sio kudra tuu, kuna watu waliomba, wakaumba ndipo hizo kudra zikaja!.

Mimi ni mtu wa mastori mastori, kwa wale wa mastori watu tulianza lini na Samia, enzi hizo hajawa hata Waziri, mnaweza fuatilia hapa, wale wa short and clear, nenda mwisho

Baada ya Rais Samia kuupata urais wa Tanzania, na kuja na falsafa yake ya 4R, tumempigia kelele sana kuhusu kuruhusu mikutano ya siasa na maadamano, hatimaye akaruhusu, tukampongeza Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?

Hitimisho
Hivyo Kama Maandamano ya Chadema yamewezekana chini yake Rais Samia!, huu ni uthibitisho wa uwezo wa Rais Samia kutenda haki!, Hivyo nina imani kabisa na Rais Samia kwa asilimia 100% zile haki mbili kuu zilizotolewa na katiba yetu, haki ya kupiga kura na haki ya kupigiwa kura, zilitolewa na ibara ya 5 na ibara ya 21, kisha zikaja kuporwa na ibara ya 39, na 67, Ajabu Hii ya Haki Iliyotolewa na Ibara Moja ya Katiba, Kuporwa na Ibara Nyingine, Ilifanyika Vipi Huku Tuna Washeria Manguli, Wabobezi na Wabobevu?

Naamini Rais Samia ana uwezo kabisa wa kuzirejesha!, kitu tunachotakiwa kukifanya ni tuvute tuu subra!. Kila jambo na wakati wake! Kwa vile mikutano na maandamano ni haki ya vyama, wao waendelee kukutana na kuandamana, muda muafaka wa haki hizo kutolewa ukiwadia, haki hizo zinatolewa.

Mungu Mbariki Rais Samia aweze kutenda haki bin haki.

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali.
 
Maisha ni

1. Siasa
2. Kijamii
3. Kiuchumi

Shida ya nyie akina Paschel Mayala mnadhani hitaji kubwa la watanzania ni siasa tu masaa 24!!! Yani nyie hata nchi iporomoke kutoka uchumi wa kati au viwanda vifungwe kwa kukosa umeme nyie ni Sawa tu ili mradi chadema wameruhusiwa kuandamana, hii ni sawa?

Nchi za wenye akili rais anapongezwa kwa kukuza uchumi , na kwenye nchi hizo raia wake masaa 24 wanazungumzia namna ya kukuza uchumi na siyo hizi porojo zenu za 4R zinazolenga kufisadi mali za Uma kupitia kulipana posho.

Hitaji la watanzania 90% uchumi na hizo siasa zenu ni 5% elewa hivyo ewe mzee Mayala.
 
Rais Samia tayari ameingia katika Kitabu Cha KUMBUKUMBU, Marais wa kiume wote waliogopa maandamano, mama mlezi ameweza bila hata sisimizi kuumizwa. Rais aliyepita alisema uchaguzi ukiisha hakuna mikutano mpaka miaka 5 ipite, mama mlezi alimruhusu mikutano. Rais aliyepita alisema mwanafunzi anayezaa akiwa shule asirudi shuleni, Mama mlezi ameruhusu warudi shuleni. Rais aliyepita alisema mkurugenzi ambaye eneo lake atachaguliwa mpinzani, hana kazi, hili mama mlezi aangalie chaguzi zijazo aruhusu sanduku la kura lichague aliyechaguliwa na Wananchi siyo achague yeye kama aliyepita. HONGERA sana mama mlezi kwa kuyaweza yaliyowashinda Marais wa kiume, umeingia katika Kitabu Cha KUMBUKUMBU.


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza maandamano si fadhila za Sa100,
Pili kutozuiwa na police ni calculation ndefu zimefanywa na kuna vitu vipo nyuma ya pazia vingi tu. Unajua watu na vikao alivyofanya mbowe kabla ya maandamano. Nan alikutana nao na wamemsaidiaje? Je unajua conditions ilizopewa Tanzania na wakubwa baada ya kuvuta Mpunga na wakatia mfukoni matapeli Hawa? Sa100 is nothing and should not be hailed for this political right. Poor president,visionless and aimless. Vote her not plz.
 
Kuwa huru mkuu paskali kwa kuwa upo nchi huru kutoa maono yako atakayekuita chawa nae pia hayo ni maoni yake kwa kuwa yupo nchi huru na yenye iliyotamalaq demokrasia kama tulivyoshuhudia afande Muliro kumsindikiza Mbowe na Lissu!
 
Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
Kama maandamano ya January yaliwezekana, kilichofanya maandamano haya yazuiwe ni neno "Samia Must Go"!. Hili ni kosa Chadema wasilirudie tena!.

CCM tunaandaa maandamano ya Samia Mitano Tena, sijui kama yataruhusiwa!.
P
 
HBD Rais Samia!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…