Kama majeshi ya Rwanda yaliwamaliza magaidi wa Cabo Delgado ndani ya wiki moja, hawa viongozi wetu wa ulinzi walienda kufanya nini Msumbiji?

nyboma

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2021
Posts
2,308
Reaction score
7,366
Hakika nimeamini vita dhidi ya ugaidi inahitaji akili kubwa mno kuliko matumizi ya nguvu, ni miezi michache tu iliyopita tulitangaziwa na kuaminishwa ya kwamba magaidi ambao walikuwa wameshikilia jimbo la Cabo delgado walipigwa na kumalizwa na jeshi kutoka rwanda.

Ila hivi karibuni tena kumeripotiwa mashambulizi ya kushtukiza kutoka kwa hao magaidi wakitokea mafichoni katika mapori ya cabo delgado na kuja kushambulia/ kufanya uhalifu vijiji vilivyopo mpakani mwa Tanzania na kutokomea kusikojulikana

Hapa chini ni picha ikiwaonesha viongozi wa ngazi za juu za ulinzi wa Tanzania na Mozambique walipokutana mwanzoni mwa wiki hii kujadili suala hili nyeti, hii inatoa tafasri ya kwamba mpakani hali si shwari na tutegee task force mpya kwenda kupambana na hawa magaidi.

Swali langu kwa wajuzi wa mambo haya ni kwamba hawa magaidi ni kweli tumeshindwa kuwatokomeza ama kuna mchezo unachezwa kuwanufaisha watu fulani fulani ili watimize malengo yao kwa kivuli cha ugaidi katika nchi husika?

 
Unaufahamu ugaidi wewe ,


USSR
Siufahamu, ndio maana nimekuja kwenu wajuzi mniambie hii kitu inakuaje? Maana tuliaminishwa humu ndani kwamba jeshi kutoka kagame walimaliza ndani ya wiki moja.

Pia kwa kazi nzuri waliyofanya jeshi la Rwanda, Mh. Paul Kagame alipewa mualiko maalamu na Mh. Nyusi wa kuonana nae kumpa pongezi za dhati kwa kuwafutilia mbali hao magaidi.

Sasa baada ya Kamanda Sirro alivyoongea na vyombo vya habari na kukiri kuwa na mashambulizi mpaka nikawa sielewi kabisa imetokea vipi? Ilihali hawa majamaa walimalizwa na jeshi la rwanda
 
Kubwa mno
Sasa mkuu, kwanini vyombo hivyo vilipambe jeshi la rwanda? Ili hali halikufanikiwa kuwaondosha magaidi wote kama tulivyoaminishwa?

Why Rwanda?
 
Ruvuma Basin kuna mafuta na gesi nyingi sana
Kampuni ya South Africa inachimba mafuta hapo ila wananchi hawana hata Milo miwili na wengine kulala njaa

Ukisema kuwa PK jeshi lake liliwamaliza kwa uhakika sio kweli!
Bali ni naona ni maingezi na mapatano kuwa nitapata % ngapi hapo?

Kila kwenye vurugu kuna chanzo cha vurugu hiyo na Cabo Delgado chanzo ni mafuta hayo ambayo yametokea kuwa mpakani ( uwe makini na hapo)

Sasa mafuta ya mpakani sisi tunafaidika vipi ingawa yapo kwao?

Je, kuna mikono mingapi inataka kula hapo?

Je, PK ameangamiza au wanakula meza moja nao?

Ukiona sehemu kuna mlo lazima kuwe na mpambano ila waarabu waliishinda vita na kukaa meza moja na wenye mitambo na kuamua kula nao chochote wanachotaka ili mradi nao wale kiasi na kupata mahitaji yote wanayotaka

Nyerere angesema Mwadui mining chukueni ila tujengeeni kila kitu kuanzia miji, barabara, ma hospitali na vyuo vikuu kwa miaka, Williamson angekubali maana kulikuwa na almasi nyingi sana na utajiri mkubwa sana pale

Hapo CD tuwaache wale ila na maskini wa hapo muwajengee pia
 
Ndio maana PK anatudharau.

Uganda alitusaidia yeye,na uko Mozambique pia!

Jeshi la Rwanda ni very special force lakini la kwetu liko busy kubadili makomandoo kuwa magaidi kwenye kesi za kubumba, shame!
 
Iko hivi,hawa Magaidi hawakai sehemu moja,ni vikundi vilivyotapakaa sehemu tofauti.Kweli Rwanda wamewasambalatisha Kwa sehemu kubwa,lakini hawajawamaliza.
Kwa sasa hivi magaidi wamekimbilia jimbo la Niassa wilaya ya mikula na wako sehemu tofautitofauti
 
Unaposikia magaidi au Ugaidi ni Kama upele mwilini haukai sehemu moja ukatulia ukijikuna mapajani mwingine unaibukia mgongoni .
 
Propaganda mkuu
Kama ni propaganda, ni muda sasa tumekuwa tukipambana na hawa watu na taarifa nyingi tu zimekusanywa kuhusiana na watu hawa ni kitu gani kinapelekea kutokuwasambaratisha na ikiwezekana kuwafuta kabisa maana naona wanazidi kujijenga na siku zinavyosonga watakuja kuwa tishio hasa kwenye mikoa yetu ya kusini huko?
 
Hao jamaa siyo wepesi and they are heavily funded na mabeberu
 
Hao jamaa are everywhere just like magugu

Wakipata chance wanakua

Makinga yameshavuka border

Ni test ngumu Kwa samia kuliko hata ya uchumi
 
Kilichofanyika ni kuwanyamazisha wanyarwanda...maana walianza kampeni za matangazo kama wafanyavyo magaidi.kwa protokali za SADC promo za mapambano haziruhusiwi...so Kigali hawana jinsi zaidi ya kufuata hiyo pase
 

Aisee watz wengi hamuelewi chochote

kilichompeleka PAKA kule ni ufaransa ambae analipa bill ya majeshi kuoperate mozambique kwa ajili ya kulinga uwekezaji wake wa gesi.

Ni nafasi nzuri kwa PAKA kuivamia Tanzania kupitia mozambique na kujichanganya na magaidi!! Ndicho anachofanya kongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…