nyboma
JF-Expert Member
- Aug 29, 2021
- 2,308
- 7,366
Hakika nimeamini vita dhidi ya ugaidi inahitaji akili kubwa mno kuliko matumizi ya nguvu, ni miezi michache tu iliyopita tulitangaziwa na kuaminishwa ya kwamba magaidi ambao walikuwa wameshikilia jimbo la Cabo delgado walipigwa na kumalizwa na jeshi kutoka rwanda.
Ila hivi karibuni tena kumeripotiwa mashambulizi ya kushtukiza kutoka kwa hao magaidi wakitokea mafichoni katika mapori ya cabo delgado na kuja kushambulia/ kufanya uhalifu vijiji vilivyopo mpakani mwa Tanzania na kutokomea kusikojulikana
Hapa chini ni picha ikiwaonesha viongozi wa ngazi za juu za ulinzi wa Tanzania na Mozambique walipokutana mwanzoni mwa wiki hii kujadili suala hili nyeti, hii inatoa tafasri ya kwamba mpakani hali si shwari na tutegee task force mpya kwenda kupambana na hawa magaidi.
Swali langu kwa wajuzi wa mambo haya ni kwamba hawa magaidi ni kweli tumeshindwa kuwatokomeza ama kuna mchezo unachezwa kuwanufaisha watu fulani fulani ili watimize malengo yao kwa kivuli cha ugaidi katika nchi husika?