Rais ni hatari kufanya operation ya kuondoa wamachinga barabarani (uamuzi sahihi) na wakati huo huo kuzuia raia haohao essentially wasitumie maji ya mito inayopita kwao kulima mbogamboga, umwagiliaji mdogo mdogo, ufugaji samaki, nk nk. Hapa kuna real danger ya kuleta maafa, njaa, magonjwa na vita haswa ambayo hakuna atakayeiweza. Ni vema muwaache raia watumie mito kwa uangalifu. Viongozi msitake kuleta mtafaruku maisha ya tozo yanatosha kuwa fimbo kwa viumbe hawa. Huku mtaani utawala umeshafitinika mno mambo si shwari kabisaaa. Maneno ni mengi saidieni mama. Mabango ya sura ya rais kila kona yanageuka kejeki mjue. Acheni watu watumie maji ya mito ni haki yao nyie endeleeni kula vya makopo ya supermarket toka Kenya na Ulaya msiwachokoze!