Mama Anne Kilango Malecela, Mbunge,
kwanza Mwalimu wa Sekondari ya Kisutu, huku akiwa mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kionondoni, akawa Accountant ATC, akawa Senior Accountant Gulf Air, huku akiwa mmoja wa Directors wa Casino pale Sea View, akawa mbunge wa kuteuliwa na rais, baadaye akaw mbunge wa kuchaguliw na wananchi hadi sasa, pia ni mfanya biashara maarufu wa bidahaa mbali mbali toka USA na Europe, akimiliki maduka makubwa ya bidhaa hizo kati ya Dar, Dodoma, na Same, sasa hivi pia ni makamu mwenyekiti kamati ya bunge ya Miundo Mbinu, na pia mwenyekiti wa kamati ya maadili ya viongozi ya bunge,
Toka awe mbunge wa kuchaguliwa amekuwa kiongozi hodari wa kukataa ufisadi, ndiye aliyeongoza mapambano ya kumuondoa madarakani aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Lowassa, baada ya hapo ndiye aliyepigana sana mpaka kuufuta mkatba wa kifisadi ulikouwepo bandarini kwa miaka kumi na ulikuwa uwepo kwa miaka 15 zaidi, akiwa kama mwenyekiti wa muda wa kamati ya Miundo Mbinu ya bunge kutokana na mwenyekiti wa kamati Ndugu Misanga, kutoweza kushiriki kikamilifu kwenye kamati hiyo kutokana na kuumwa sana ugonjwa wa kisukari, Mama mbunge pia kwa sasa yupo Chuo Kikuu Huria akimalizia Degree ya Uchumi.
Sasa mnyonge mnyongeni lakini haki apewe, ningeomba mtoa mada hii atuwekee qualifications za hao anaosema kuwa wameangalia CV ya huyu mbunge wetu wa taifa na kuona hafai, maana nina wasi wasi kuwa sio rahisi mwananchi mwenye CV ya wasi wasi kuweza kuielewa CV inayofaa au isiyofaa, au kuelewa kuwa ni kiongozi yupi anafaa na yupi hafai, halafu ikiwezekana atupe historia ya hao wanachi jinsi ambavyo wamewahi kulisaidia taifa letu na hizi hukumu, ambazo pia watuambie wamezi-base on CV za viongozi wapi hao wa taifa letu wanaofaaa!
Ninasema kuwa Mama Anne Kilango Malecela, anazo qualifications zote anazozihitaji kuwa na nafasi aliyonayo sasa, yaani mbunge wa kuchaguliwa na kuwawakilisha wananchi bungeni.