Kama Mama Malecela hafai, je Mbowe anafaa?

Tunaomba cv yako kada mpinzani wa maendeleo

UNAOMBA WEWE NA NANI ??mie nimekuwa mbowe anayegombea uongozi asioujua ?? nitakupa cv pale nitakapotaka kukutawala, but for the moment sina haja ya kukupa so siwezi kuitoa nitaibana, mwambie mbowe anayetaka kukutawala akupe cv yake !! kuwa makini na unayetaka akutawale kijana !!
 


Mama Anne Kilango Malecela, Mbunge,

kwanza Mwalimu wa Sekondari ya Kisutu, huku akiwa mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kionondoni, akawa Accountant ATC, akawa Senior Accountant Gulf Air, huku akiwa mmoja wa Directors wa Casino pale Sea View, akawa mbunge wa kuteuliwa na rais, baadaye akaw mbunge wa kuchaguliw na wananchi hadi sasa, pia ni mfanya biashara maarufu wa bidahaa mbali mbali toka USA na Europe, akimiliki maduka makubwa ya bidhaa hizo kati ya Dar, Dodoma, na Same, sasa hivi pia ni makamu mwenyekiti kamati ya bunge ya Miundo Mbinu, na pia mwenyekiti wa kamati ya maadili ya viongozi ya bunge,

Toka awe mbunge wa kuchaguliwa amekuwa kiongozi hodari wa kukataa ufisadi, ndiye aliyeongoza mapambano ya kumuondoa madarakani aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Lowassa, baada ya hapo ndiye aliyepigana sana mpaka kuufuta mkatba wa kifisadi ulikouwepo bandarini kwa miaka kumi na ulikuwa uwepo kwa miaka 15 zaidi, akiwa kama mwenyekiti wa muda wa kamati ya Miundo Mbinu ya bunge kutokana na mwenyekiti wa kamati Ndugu Misanga, kutoweza kushiriki kikamilifu kwenye kamati hiyo kutokana na kuumwa sana ugonjwa wa kisukari, Mama mbunge pia kwa sasa yupo Chuo Kikuu Huria akimalizia Degree ya Uchumi.

Sasa mnyonge mnyongeni lakini haki apewe, ningeomba mtoa mada hii atuwekee qualifications za hao anaosema kuwa wameangalia CV ya huyu mbunge wetu wa taifa na kuona hafai, maana nina wasi wasi kuwa sio rahisi mwananchi mwenye CV ya wasi wasi kuweza kuielewa CV inayofaa au isiyofaa, au kuelewa kuwa ni kiongozi yupi anafaa na yupi hafai, halafu ikiwezekana atupe historia ya hao wanachi jinsi ambavyo wamewahi kulisaidia taifa letu na hizi hukumu, ambazo pia watuambie wamezi-base on CV za viongozi wapi hao wa taifa letu wanaofaaa!

Ninasema kuwa Mama Anne Kilango Malecela, anazo qualifications zote anazozihitaji kuwa na nafasi aliyonayo sasa, yaani mbunge wa kuchaguliwa na kuwawakilisha wananchi bungeni.
 
watu wabaya kweli, wanamdisqualify mama kilango? why people why ?
 


Can you show the forum what is skewed in, either my questioning or the Mbowe CV I posted? If not can you help MwK to answer the posed Qs because she seem to be of the lower level of education to the CV bearer?
 
Can you show the forum what is skewed in, either my questioning or the Mbowe CV I posted? If not can you help MwK to answer the posed Qs because she seem to be of the lower level of education to the CV bearer?

gat you questions answered

..... next!
 
watu wabaya kweli, wanamdisqualify mama kilango? why people why ?

Mama Kilango,

Is doing just fine, sasa hivi anamalizia mitihani ya nusu term, na anatuma salam sana hapa kwa ushirikiano aliopewa kuhusiana na ile interview na hasa kwa Mkulu Mwanakijiji, na anasema kuwa kuanzia sasa yupo open at anytime akitakiwa kuja hapa kutupa maelezo ya any ishu inayoendelea huko bungeni au taifa,

Yaliyojiri mpaka kuchelea kwa hizi attakcs tunayajua, kuna member mmoja kutoka hapa alijaribu majuzi kwenda kwake kujikomba akafukuzwa naye ni kwa sababu hakufuata protocol, mama alipotuarifu tutoe okay ya kukutana na huyu member tukamwambia hapana asimpe nafasi, sasa ndio yamekuwa haya, I hope huyu mkuu anajua anachokifanya, na yeye tumeshamfahamisha yanayojiri hapa na huyu member.

Be my guest bro!
 


http://www.parliament.go.tz/bunge/Mp_Cv3.asp?PTerm=2005-2010&fpkey=112&vusername=GUEST")



CV ya mama Malecela ni nzuri sana hasa kwa mwanamama wa rika lake na haiwezi kulinganishwa kabisa na CV tupu ya Mbowe, ingawa Mbowe was more priviledged than 99% ya watanzania.





[/quote]


CV ya Mbowe

 

kwi kwi kwi kwi,

inatia huruma maana huyo memba hakujua kuwa habari zake zitafika JF kama kawa... sasa ni huruma tu na si kingine.
 
CV ya mama Malecela ni nzuri sana hasa kwa mwanamama wa rika lake na haiwezi kulinganishwa kabisa na CV tupu ya Mbowe, ingawa Mbowe was more priviledged than 99% ya watanzania.

Umeanza lini kujikomba komba kwa mama malecela? jambo moja tu nina hakika nalo kuhusu Mbowe ambaye bado anaendeleza biashara zake, kuendesha chama, na kupigania haki za wananchi na huku akijiendeleza accordingly ni kimoja - Mbowe hana chuki za kidini kama zako.
 
Mugabe Robert ana degree za kusoma kama nne hivi, na kapewa za bure tu kama sita vile kwa hiyo anazo za kutosha, lakini Uchumi wa Zimbabwe ndio tunaousoma wa quadrillion kununua sijui mkate au embe.

Bila kusahau mafisadi wengi wa Tanzania waliosoma Havard kwa pesa ya walipa kodi Mramba, nk. Lakini wapi? Kwa hiyo basi elimu ndio ufunguo wa maisha lakini sio elimu ya degree tu. Elimu iko kwa namna mbali mbali sio elimu ya kikasumba tu.
 
Hapana mkuu wangu, sio Kubwajinga wala Kada, au mtoa hii topic, yupo mwenyewe kwa pembeni pembeni, yaani side kick!

Ninamjua ila nimempa kubwajinga dosier yake pia hapa hapa maana kwa vile leo ameanza kujikombakomba kwa mama Malecela wakati huyu mama hapendi watu wenye chuki za kidini kama yeye.
 

Dua, unajua hata Kichaka amesoma ivy league.... huyu kubwa jinga ana chuki zake na Mbowe na Chadema kwa ujumla na zinahusu vitu vingine kabisa ila kila mara akitokeza kichwa hapa JF anaumbuliwa.
 



Kama hayo ndio majibu uliyoona yanafaa kuelezea mapungufu ya Mbowe, basi tukiogope Chadema. Maana hayo uliyotupa ni majibu ya darasa la saba la kijiweni.
 
Kama hayo ndio majibu uliyoona yanafaa kuelezea mapungufu ya Mbowe, basi tukiogope Chadema. Maana hayo uliyotupa ni majibu ya darasa la saba la kijiweni.

ukileta maswali ya kijiweni unapata majibu ya kijiweni. Ukileta hoja za maana nawe utapata hoja za maana. Kwa sasa watu wabaguzi na wenye chuki za kidini kama wewe hawaitaji majibu ya maana. Wanapata majibu yanayolingana na level ya maswali yao.

Next.....
 
ukileta maswali ya kijiweni unapata majibu ya kijiweni. Ukileta hoja za maana nawe utapata hoja za maana.


I like this one, maana yake in short ni kwamba hoja hujibiwa kwa hoja, na sio viroja! Mimi siku hizi mambo ya vyama niliaacha kabisaa niko taifa tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…