Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
Pengine tunachochanganya hapa ni umuhimu (effect) ya elimu katika ufanisi (effectiveness) na maadili (ethics) ya kiongozi. Elimu inaweza kukusaidia uwe effective lakini sio lazima ikusaidi kuwa ethical! Kwa kweli nchi yetu haina kabisa tatizo la viongozi wenye elimu ya kutosha, kama tukitumia idadi ya degree kama kigezo cha elimu kubwa au ndogo.
Kwa hiyo, kwa maoni yangu, tatizo la nchi yetu kwa sasa ni lack of ethical leaders.Kwa sababu hii utaona kwamba kiongozi kuwa na elimu kubwa sana inaweza ikawa sio jibu sana la matatizo ya uongozi wa nchi yetu yanayotukabili kwa sasa. Thus, to me, when we try to judge Mbowe whether or not he is an effective leader on the basis of his educationa level, we are definetely asking wrong questions and therefore we must get wrong answers!
In any case, kwa wale wanaojua historia ya CHADEMA hawawezi kupuuza mafanikio ya Mbowe kama kiongozi. Wanaofuatilia mambo ya siasa Tanzania wanajua kwamba Mbowe kaitoa CHADEMA from a docile NGO to a respectable and winnable political party. So far sisi tunajua kwamba Mbowe amekwisha kuipeleka CHADEMA kwenye macho, masikio, akili na nyoyo za watanzania. Kinachofanyika sasa ni kuhakikisha kuwa CHADEMA inafika kwenye vidole vya watanzania ili ifikapo 2010 waweza kukunjua hivyo vidole katika sanduku la kura, na yote haya yanafanyika chini ya uongozi shupavu na imara sana wa Mhe Freeman Aikael Mbowe.
Mkuu Kitila,
- Nakubaliana na wewe kuwa kuna tatizo la maadili ya viongozi. Lakini hili halina mipaka ya kielimu, bali ni kulingana na nafasi walizoshikilia wahusika. Mwenye digirii na wa diploma wote wanaweza kuwa mafisadi k.m. Dr. Ballal na afande Zombe. Kwangu mimi naliona tatizo zaidi lipo katika mfumo wa uongozi nchini ambao unakosa check and balances. Serikali imekuwa na nguvu sana kuliko bunge, mahakama na jumuia za kiraia, kiasi kuwa, inakuwa rahisi kwa viongozi kula rushwa kwa vile wanaelewa wazi kuwa wanaweza kukwepa hukumu. Mkapa alifanya kazi nzuri serikalini katika ngazi mbalimbali kwa miaka zaidi ya 35 bila kuwa mbadhilifu. Lakini alipoingia ikulu, vishawishi na upenyo uliokuwepo vikamfanya abadilike na kuwa jangili. Kwa hiyo licha ya historia yake ndefu ya usafi, vitamanisho vya mfumo mbaya viliweza kumuingiza pabaya. Hivyo watu wasio na historia ndefu ya usafi kama Mbowe wanaweza wakawa ni wabaya mara nyingi zaidi kwani mfumo unaruhusu kuwa hivyo.
- Sikubaliani na wewe unaposema kuwa Mbowe amekuza Chadema. Chadema imekua kutokana na umaarufu wa akina Zitto na Slaa. Kama kipo alichofanya Mbowe kilichosababisha kukua kwa Chadema, zaidi ya kumuingiza Zitto na wengine chamani, mimi binafsi sijaliona. Hakuna lingine kubwa la kutufanya tuache kuangalia failures zake za kielimu na kibiashara na kumkubali kwa hayo mafanikio yake. Moja kati ya aliyoboronga Mbowe ni kutumia ruzuku karibu yote kwa ajili yake binafsi na kujirusha na helikopta, wakati wagombea ubunge wengi wakiwa hawana resources za kufanyia kampeni. Matokeo yake wagombea kama Dr.Kaborou wakashindwa na kuhama chama na Mbowe akapata kura chini ya nusu ya zile alizopata Lipumba. Hii pekee ilipaswa imlazimishe kujiuzulu uongozi.
Kwa kifupi ni kuwa, Mbowe hajafanyia nchi lolote lile, hata alipokuwa mbunge, tunaloweza kumfanya tukamsamehe sifa zake ndogo za kielimu.