Kama Mama Malecela hafai, je Mbowe anafaa?

Kama Mama Malecela hafai, je Mbowe anafaa?

Pengine tunachochanganya hapa ni umuhimu (effect) ya elimu katika ufanisi (effectiveness) na maadili (ethics) ya kiongozi. Elimu inaweza kukusaidia uwe effective lakini sio lazima ikusaidi kuwa ethical! Kwa kweli nchi yetu haina kabisa tatizo la viongozi wenye elimu ya kutosha, kama tukitumia idadi ya degree kama kigezo cha elimu kubwa au ndogo.

Kwa hiyo, kwa maoni yangu, tatizo la nchi yetu kwa sasa ni lack of ethical leaders.Kwa sababu hii utaona kwamba kiongozi kuwa na elimu kubwa sana inaweza ikawa sio jibu sana la matatizo ya uongozi wa nchi yetu yanayotukabili kwa sasa. Thus, to me, when we try to judge Mbowe whether or not he is an effective leader on the basis of his educationa level, we are definetely asking wrong questions and therefore we must get wrong answers!

In any case, kwa wale wanaojua historia ya CHADEMA hawawezi kupuuza mafanikio ya Mbowe kama kiongozi. Wanaofuatilia mambo ya siasa Tanzania wanajua kwamba Mbowe kaitoa CHADEMA from a docile NGO to a respectable and winnable political party. So far sisi tunajua kwamba Mbowe amekwisha kuipeleka CHADEMA kwenye macho, masikio, akili na nyoyo za watanzania. Kinachofanyika sasa ni kuhakikisha kuwa CHADEMA inafika kwenye vidole vya watanzania ili ifikapo 2010 waweza kukunjua hivyo vidole katika sanduku la kura, na yote haya yanafanyika chini ya uongozi shupavu na imara sana wa Mhe Freeman Aikael Mbowe.

Mkuu Kitila,
  1. Nakubaliana na wewe kuwa kuna tatizo la maadili ya viongozi. Lakini hili halina mipaka ya kielimu, bali ni kulingana na nafasi walizoshikilia wahusika. Mwenye digirii na wa diploma wote wanaweza kuwa mafisadi k.m. Dr. Ballal na afande Zombe. Kwangu mimi naliona tatizo zaidi lipo katika mfumo wa uongozi nchini ambao unakosa check and balances. Serikali imekuwa na nguvu sana kuliko bunge, mahakama na jumuia za kiraia, kiasi kuwa, inakuwa rahisi kwa viongozi kula rushwa kwa vile wanaelewa wazi kuwa wanaweza kukwepa hukumu. Mkapa alifanya kazi nzuri serikalini katika ngazi mbalimbali kwa miaka zaidi ya 35 bila kuwa mbadhilifu. Lakini alipoingia ikulu, vishawishi na upenyo uliokuwepo vikamfanya abadilike na kuwa jangili. Kwa hiyo licha ya historia yake ndefu ya usafi, vitamanisho vya mfumo mbaya viliweza kumuingiza pabaya. Hivyo watu wasio na historia ndefu ya usafi kama Mbowe wanaweza wakawa ni wabaya mara nyingi zaidi kwani mfumo unaruhusu kuwa hivyo.
  2. Sikubaliani na wewe unaposema kuwa Mbowe amekuza Chadema. Chadema imekua kutokana na umaarufu wa akina Zitto na Slaa. Kama kipo alichofanya Mbowe kilichosababisha kukua kwa Chadema, zaidi ya kumuingiza Zitto na wengine chamani, mimi binafsi sijaliona. Hakuna lingine kubwa la kutufanya tuache kuangalia failures zake za kielimu na kibiashara na kumkubali kwa hayo mafanikio yake. Moja kati ya aliyoboronga Mbowe ni kutumia ruzuku karibu yote kwa ajili yake binafsi na kujirusha na helikopta, wakati wagombea ubunge wengi wakiwa hawana resources za kufanyia kampeni. Matokeo yake wagombea kama Dr.Kaborou wakashindwa na kuhama chama na Mbowe akapata kura chini ya nusu ya zile alizopata Lipumba. Hii pekee ilipaswa imlazimishe kujiuzulu uongozi.
Kwa hiyo ukitaka kujua dalili mbaya za kiongozi, ni kuangalia jinsi anavyoongoza na kutumia mali wakati akiwa na rasilimali chache. Chadema chini ya Mbowe imeongezeka ukabila katika kugawa madaraka na pia matumizi mabaya ya pesa. Sasa kiongozi kama huyu atakapokuwa na nafasi kubwa serikalini si ndio itakuwa vurugu?

Kwa kifupi ni kuwa, Mbowe hajafanyia nchi lolote lile, hata alipokuwa mbunge, tunaloweza kumfanya tukamsamehe sifa zake ndogo za kielimu.
 
Tatizo lenu hamjui hata karne inamiaka mingapi. Mko hapa kwa ajili ya ubishi na sio kutaka kujenga hoja zenye mantiki. Kwanza jina MJINGA ni zuri kuliko mpumbavu kama mlivyokuwa mkitaka kulenga. Mjinga ni mtu ambaye yuko tayali kujua mambo na hakuna haja ya kumdharau mjinga
 
Mkuu KJ,

Ninakuelewa sana, tatizo ni kwamba Mama Theresa alisema kuwa "..Binadamu useiympenda hata kabla humjui, basi huwezi hata kumhukumu kwa lolote...", wewe unaonekana una chuki binafsi na Mbowe, na sio kwamba una a serious ishu against his education kwa sababu ungekuwa, basi ungeipanua hii ishu kwa mapana na marefu, badala ya kui-limit on Mbowe only,

Ungetufahamisha level ya elimu ya form Six ya zamani aliyoisoma Mbowe na ya sasa, halafu ungetuambia nini hasa maana ya form six kwa taifa letu, eti kweli ni mambu mbu ambao hawezi kuwa competitive kwenye accademic World? Je kwa kawaida mtu akimaliza form six next anaenda wapi? Form six ya bongo inachuliwaje accademically nje ya taifa letu hasa Europe na USA?

Mkuu FMES,
Nashukuru kwa kunibambikizia chuki, lakini sitaacha kujadili ubora wa viongozi tunaowataka maana kuna wengi mnaotaka kutubambikizia mauozo kwa manufaa yenu binafsi. Kwa vile Mbowe mlikuwa wote shuleni hii haimfanyi awe kiongozi wetu, ni sifa zake tu ndio zitamuwezesha kufikia kileleni. Mbowe anafahamika kiasi cha kutosha, kama kuna tusilofahamu ambalo ni muhimu basi tufahamishe.

Pia usijidanganye kuwa eti form six ya miaka ya 80-90s ni bora kuliko ya 2008. Huku ni kujidanganya maana mfumo bado ni ule ule. Kaangalie mitihani yake utaona inavyoshabihiana. Form 6 wa 90s alichofaidika ni kuwa na nafasi zaidi za ajira za ukarani bila kwenda kuusomea lakini uwezo wao wa kufikiria ni sawa sawa tu na huyu wa 2008 au wa 2008 anaweza akawa better kwa sababu ya internet n.k.

Kwa mtu aliyekuwa priviledged kama Mbowe alitakiwa hivi sasa awe na degree zaidi ya mbili, hasa ukitilia maanani pia kuwa ametokea kijiji ambacho elimu ilifika siku nyingi na kuna wasomi wengi. Lakini akaishia kuwa karani ikionyesha upungufu mkubwa wa uwezo wake kubukua. Kwa taarifa yako, form six ya bongo sio spesheli huko US na UK, ni ya kawaida kama sio questionable wakati mwingine.
 
1.
Kwa vile Mbowe mlikuwa wote shuleni hii haimfanyi awe kiongozi wetu, ni sifa zake tu ndio zitamuwezesha kufikia kileleni. Mbowe anafahamika kiasi cha kutosha, kama kuna tusilofahamu ambalo ni muhimu basi tufahamishe.

Mkuu hakuna mahali popote ambapo nimesema kuwa nimesoma na Mbowe, usiweke maneno mdomoni mwangi ili tu ufanikishe nia yako ya kumtukana bila sababu, the matter of fact ni wewe ndiye uliyefanya kazi naye kule BOT, pamoja na kwamba hujasema lakini ninalijua hilo, sasa ukisema sifra sielewi unasema nini wakati kila mtu hapa anajua sifa za Mbowe kama mwenyekiti wa Chadema, kama umeshindwa hoja mkuu sio vibaya ukakaa pembeni badala ya kujaribu kulazimisha hoja!

2.
Pia usijidanganye kuwa eti form six ya miaka ya 80-90s ni bora kuliko ya 2008. Huku ni kujidanganya maana mfumo bado ni ule ule. Kaangalie mitihani yake utaona inavyoshabihiana. Form 6 wa 90s alichofaidika ni kuwa na nafasi zaidi za ajira za ukarani bila kwenda kuusomea lakini uwezo wao wa kufikiria ni sawa sawa tu na huyu wa 2008 au wa 2008 anaweza akawa better kwa sababu ya internet n.k.

Mkuu nimekupa hoja nzito kuhusiana na hoja zako kuhusu form six ya bongo, naomba niziweke tena hapa chini kama umeshindwa kujibu basi acha badala ya kujaribu kutafuta short cut!

Kwa mtu aliyekuwa priviledged kama Mbowe alitakiwa hivi sasa awe na degree zaidi ya mbili, hasa ukitilia maanani pia kuwa ametokea kijiji ambacho elimu ilifika siku nyingi na kuna wasomi wengi. Lakini akaishia kuwa karani ikionyesha upungufu mkubwa wa uwezo wake kubukua. Kwa taarifa yako, form six ya bongo sio spesheli huko US na UK, ni ya kawaida kama sio questionable wakati mwingine.

Bill Gates hana Degreee yoyote mkuu na alikuwa tajiri mkubwa kuliko wote duniani mpaka alipopitwa na M-mexico, Freeman hakuhitaji kuwa na degree ili kufanya anayoyafanya sasa hivi, halafu kwenye kugombea urais alitimiza masharti ya sheria za bongo na Chadema, je anahitaji kuwa na elimu zaidi ni kweli, eti kwamba ana upungufu mkubwa ni too much of a language ambayo haifanani kabisa na ishu ta hand ndio unapoonyehsa chuki zako na Mbowe,

Mkuu sasa tizama maswali niliyokupa hapa chini na majibu yako uone jinsi ilivyo mbali kabisaa na ukweli!
 
Ninakuelewa sana, tatizo ni kwamba Mama Theresa alisema kuwa "..Binadamu useiympenda hata kabla humjui, basi huwezi hata kumhukumu kwa lolote...", wewe unaonekana una chuki binafsi na Mbowe, na sio kwamba una a serious ishu against his education kwa sababu ungekuwa, basi ungeipanua hii ishu kwa mapana na marefu, badala ya kui-limit on Mbowe only,

Ungetufahamisha level ya elimu ya form Six ya zamani aliyoisoma Mbowe na ya sasa, halafu ungetuambia nini hasa maana ya form six kwa taifa letu, eti kweli ni mambu mbu ambao hawezi kuwa competitive kwenye accademic World? Je kwa kawaida mtu akimaliza form six next anaenda wapi? Form six ya bongo inachuliwaje accademically nje ya taifa letu hasa Europe na USA?

Mkuu nilitegemea ungefanya angalau a min-case study kwa ajili ya the future ya taifa letu, kwamba viongozi wa bongo wenye elimu tazama mazuri waliyoyafanya kutokana na elimu yao, na mabaya ya elimu yao, halafu tizama uzuri wa viongozi wasiokuwa na elimu na mabaya yao, je form six ya bongo ni sawa na mtu asiyekuwa na elimu kabisa? Then ndio ungehitimisha kwa kuangalia pia mafanikio ya Mbowe kimaisha na kiuongozi, lakini so far I am not convinced kuwa una a strong argument against Mbowe education kwa sababu ni lazima kuwa na mifano inayozidi angalua kumi ya wananchi wa bongo waliomaliza form six ya zamani na kufikia level ya Mbowe kisiasa na kibiashara, my point ni kwamba uiweke kwenye big picture na ielewekae then ishu ya Mbowe ambayo ni very isolated nkwenye hiyo big picture itaonekana na hutakuwa na hizi struggle unazo go through so far ili kuhitimisha na kuelimisha hoja yako mkuu.

I mean una some points lakini tatizo ni kwamba umeweka big points kwenye maneno ambayo yanajadili hii ishu yako kwenye level ya Yanga na Simba, sasa mkuu hebu jaribu ku-deal na the extremes na baadaye ujaribu ku-reconcile na ku-balance, kabla huja-conclude, Mbowe ni Mtanzania mmoja tu kati ya wa-Tanzania 35,000,000 sasa unapoamua kuongelea elimu yake kwa faida na madhara ya taifa kutokana na nafasi yake kisiasa, basi ni lazima study yako iwe au ilenge national level sio Yanga na Simba like dicussions!

I hope umenielewa mkuu!
 
Mkuu KJ,Mkuu nilitegemea ungefanya angalau a min-case study kwa ajili ya the future ya taifa letu, kwamba viongozi wa bongo wenye elimu tazama mazuri waliyoyafanya kutokana na elimu yao, na mabaya ya elimu yao, halafu tizama uzuri wa viongozi wasiokuwa na elimu na mabaya yao, je form six ya bongo ni sawa na mtu asiyekuwa na elimu kabisa? Then ndio ungehitimisha kwa kuangalia pia mafanikio ya Mbowe kimaisha na kiuongozi, lakini so far I am not convinced kuwa una a strong argument against Mbowe education kwa sababu ni lazima kuwa na mifano inayozidi angalua kumi ya wananchi wa bongo waliomaliza form six ya zamani na kufikia level ya Mbowe kisiasa na kibiashara, my point ni kwamba uiweke kwenye big picture na ielewekae then ishu ya Mbowe ambayo ni very isolated nkwenye hiyo big picture itaonekana na hutakuwa na hizi struggle unazo go through so far ili kuhitimisha na kuelimisha hoja yako mkuu.

I mean una some points lakini tatizo ni kwamba umeweka big points kwenye maneno ambayo yanajadili hii ishu yako kwenye level ya Yanga na Simba, sasa mkuu hebu jaribu ku-deal na the extremes na baadaye ujaribu ku-reconcile na ku-balance, kabla huja-conclude, Mbowe ni Mtanzania mmoja tu kati ya wa-Tanzania 35,000,000 sasa unapoamua kuongelea elimu yake kwa faida na madhara ya taifa kutokana na nafasi yake kisiasa, basi ni lazima study yako iwe au ilenge national level sio Yanga na Simba like dicussions!

I hope umenielewa mkuu!

Mkuu FMES,
Shule au NO Shule sio suala la Simba na Yanga na huhitaji kulifanyia mini study. Inaeleweka vema kuwa shule inamsaidia mhusika kushinda vikwazo vingi ukilinganisha na NoShule or Less-Shule. Hili ni suala la wazi kwa mtu kuelewa tofauti zake. Na ndio maana licha ya kuwa na form six leaver wengi, bado ni wachache sana walio katika ngazi za uongozi hata kwenye mashirika na makampuni.

Uongozi wa TZ tatizo lake sio shule kubwa, bali ni kutokuwepo kwa maadili ambayo yanasababishwa kwa kiasi kikubwa na mfumo mbaya wa mgao wa nguvu kati ya Serikali, Bunge, Mahakama na Jumuiya za wananchi. Hivi sasa mtu yeyote akiingia madarakani kuna nafasi kubwa kwa yeye kuwa fisadi kwani mianya iliyopo ni mingi na inatamanisha wao kuwa fisadi.

Kwa hiyo hatuwezi kusema kuwa kwa kuingiza wapumbavu au wenye shule ndogo kwenye uongozi wa juu, basi suala la ufisadi litaisha. Kama vishawishi bado viko pale pale, na viliweza kumbadilisha mkatoliki safi kwa zaidi ya miaka 35 (Mkapa), akawa fisadi, then tatizo lipo kwenye structure na sio elimu kubwa.

Madhara ya elimu ndogo sio umbumbu wa kutojua anachoambiwa na wataalam tu, bali pia ni pamoja na maamuzi ya kujinga-kijinga. Zaidi ya yote elimu ndogo pia haiondoi wizi.
 
1.
FMES,
Mtu anapochukia elimu huwa kwa kawaida anakuwa either naye hana elimu au anashaka na elimu yake. Sijui wewe tukuweke kwenye kundi lipi ingawa nafahamu kuwa ulipata Associate Degree na ukajiendeleza baada ya hapo. Kama hukuona umuhimu wa elimu baada ya kuelimika, basi either elimu yako haikusaidii au una maslahi kwa kumtetea asiyesoma.

Mkuu unajua vyema kuwa elimu yangu haishii Associate Degree, kama vile na wewe elimu yako ambavyo haikuishia Urusi, sasa usijaribu kwenda personal maana kama that is an ishu ni kwamba ninajua kuwa wewe sio hata raia wa bongo, sasa ni kipi kinachokupa nguvu na chuki namna hii ya kujadili viongozi wetu wa taifa? Ninarudia tena kuwa kama umeishiwa hoja za Mbowe na elimu yake basi acha personal mkuu kwa sababu nitakupatia right back kama ilivyo! Elimu inayokusaidia wewe mkuu iko wapi, kazi kutema sumu tu hapa za kuwatukana viongozi wetu wa taifa tena wasio wa taifa lako bila sababu?

Mimi wala sitishiki na hiyo elimu yako mbuzi kama unayo kweli maana maneno yako hayaonyeshi kuwa unayo au kama inakusaidia binafsi! eti mkuu wewe unayo elimu?
 
Mtu anapochukia elimu huwa kwa kawaida anakuwa either naye hana elimu au anashaka na elimu yake au hajui kabisa umuhimu wa elimu. These are just facts, sikuzitunga.
 
1.
Mbowe hana rekodi yoyote inayovutia ili angalau kipimo cha elimu kwake kipindindishwe au kuondolewa kama ilivyo kwa viongozi wengine wasioenda shule. Hata uongozi wake ndani ya Chadema aliopewa na mkwe wake, hivi sasa unakabiliwa na ukabila na matumizi mabovu ya ruzuku ya chama. BOT alichofanya ni ukarani tu licha ya kuwa BoT walikuwa wanasomesha sana wafanyakazi wake. Pia haionyeshi huko BOT kama kuna mchango wowote maalumu alioleta au hata kupandishwa cheo.

Hizi ni sumu zako tu ambazo tunaita kelel za mlango ambazo hazimzuii binadamua kulala ndani, kwa sababu deep inside unajua ukweli wa mafanikio ya Mbowe kimaisha mpaka kisiasa, wewe mwenye alimu kubwa kama unavyodai sijui ulichofanya kwa taifa letu ambalo sio lako so far ni kipi mkuu? Mbowe ameshakuwa mbunge wa kuchaguliwa na wananchi sasa hiyo vipi nayo jue wewe umeshawahi kuwa angalua katibu tarafa?

Bilcanas aliyorithi yeye pamoja na ndugu zake, imeshindwa kutanuka kwa miaka nenda rudi, licha ya kupata msaada wa kifedha kutoka kwenye mabenki. Lau kama angekuwa amesoma, sio ajabu hivi sasa angekuwa mbali sana kibiashara kwa kuwa mtaji tayari alisharithishwa na labda angemiliki hata Kilimanjaro Hotel.

Bilicanas haihitaji kukua zaidi ya ilipo sasa, hela alikopa benki kuifikisha ilipo sasa, je wewe mkuu umewahi kujenga hata choo cha wananchi wapi?

Kwa kifupi ni kuwa, zaidi ya urafiki uliosema mlikuwa nao shuleni au kwa kusoma wote shule moja, hakuna sababu nyingine yeyote uliyoleta inayoeleweka ya kumfanya Mbowe aaminiwe kuwa hata Mkuu wa Wilaya licha ya uraisi. Ndio maana sikushangaa alipotumia pesa yote ya chama kukodisha helikopta badala ya kuimarisha chaguzi za wabunge kama za akina Dr. Kaborou ambao hatimae wakaamua kukiacha chama. Hii inaonyesha kikomo cha fikara zake sawa na mwanga wa Kibatari.

Mkuu wewe na yeye, mlimaliza form six mkaenda wote kufanya kazi BOT, sasa haya ya mimi kusoma naye sijui unayatoa wapi bro, mimi hakuna mahali nimesema kuwa nimesoma naye nashangaa sasa unaigeuza kuwa ishu wakati mimi sijayasema hayo mkuu, kubali tu kuwa huna hoja zaidi tu ya michuki imekujaa rohoni, unajua ndio maana ninasema kuwa JF ni very interesting thing kwa sababu wewe ni mtu ambaye sikutegemea hata siku moja kuwa uko capable of this hate ambayo nimeiona ukiitema sana humu, lakini niliwahi kumuonya my wife kuwa huyu jamaa something is not right sasa mkuu nimekupata live yaani sina hamu mkuu, kila nikimuonyesha wife wangu anashindwa kuamini mkuu, lakini ndio dunia maana tunaishi kuona mengi, na haya yako kweli ni maajabu makubwa sana mkuu!

Lakini mkuu umeshindwa kujbu hoja za msingi on Mbowe, labda niziweke tena, au? saidia taifa na elimu nzito sio chuki za binafsi mkuu!
 
Mtu anapochukia elimu huwa kwa kawaida anakuwa either naye hana elimu au anashaka na elimu yake au hajui kabisa umuhimu wa elimu. These are just facts, sikuzitunga.

Mkuu mimi nina elimu ndio maana sichukii watu bila sababu za msingi, siwezi tema sumu kiasi kama chako eti kwa sababu tu ya elimu ya kiongozi ambaye hajaiba wala hajalikosea taifa, eti wewe unayo hiyo elimu? Uwezo mdogo wa kufikiri ni pamoja na kuwachukia watu bila sababu za msingi eti kisa tu hana elimu unayotaka wewe awe nayo that is low mind mkuu!
 
Shule au NO Shule sio suala la Simba na Yanga na huhitaji kulifanyia mini study. Inaeleweka vema kuwa shule inamsaidia mhusika kushinda vikwazo vingi ukilinganisha na NoShule or Less-Shule. Hili ni suala la wazi kwa mtu kuelewa tofauti zake. Na ndio maana licha ya kuwa na form six leaver wengi, bado ni wachache sana walio katika ngazi za uongozi hata kwenye mashirika na makampuni.

Sasa mkuu unaanza kujichanganya sana kwa sababu kwanza umesema kuwa form six sio elimu kabisaa, sasa tena ndio ni elimu na kwamba kuna form six leavers wengi wako kwenye uongozi na mashirika ya umma, mkuu can you make up your mind bro kama unataka kusuka au kunyoa?

Uongozi wa TZ tatizo lake sio shule kubwa, bali ni kutokuwepo kwa maadili ambayo yanasababishwa kwa kiasi kikubwa na mfumo mbaya wa mgao wa nguvu kati ya Serikali, Bunge, Mahakama na Jumuiya za wananchi. Hivi sasa mtu yeyote akiingia madarakani kuna nafasi kubwa kwa yeye kuwa fisadi kwani mianya iliyopo ni mingi na inatamanisha wao kuwa fisadi.

Hiyo mianya mbona kina Sokoine wasiokuwa na elimu hawakuiona? Acha kurukia idea za Kitla simaia zako mkuu, viongozi wa bongo wana elimu na ni wezi wakubwa sasa jaribu basi ku-reconcile na hizi idea zako badala ya kujaribu kuruka viunzi na maneno mengi!

Kwa hiyo hatuwezi kusema kuwa kwa kuingiza wapumbavu au wenye shule ndogo kwenye uongozi wa juu, basi suala la ufisadi litaisha. Kama vishawishi bado viko pale pale, na viliweza kumbadilisha mkatoliki safi kwa zaidi ya miaka 35 (Mkapa), akawa fisadi, then tatizo lipo kwenye structure na sio elimu kubwa.

Hapa ndipo unapoonyehsa chuki na uwezo wako mdogo wa kufikiri, kuwa na elimu ya form six maana yake kuwa mpubavu? Hebu tuambie ni elimu gani kwako inakuwa sio upumbavu, maana form six kwako ni pumbavu? Kwa hiyo wabongo wote waliomaliza form six na kuihsia hapo basi ni wapumbavu?

Madhara ya elimu ndogo sio umbumbu wa kutojua anachoambiwa na wataalam tu, bali pia ni pamoja na maamuzi ya kujinga-kijinga. Zaidi ya yote elimu ndogo pia haiondoi wizi.

Maamuzi ya kijinga jinga yemfanywa na Mkapa mwenye elimu ya Columbia na Makerere, kwa hiyo mkuu huna hoja hapo ila una chuki binafsi, wezi wakubwa wa taifa letu kina Lowassa wana elimu kubwa kwa hiyo mkuu naona huna hoja hapa ila chki tu as usual!
 
hivi ile orodha ya wagombea wa ccm
ya urais 2005 ni msomi zaidi ya wote aliyechaguliwa?
mi nauliza tu?
 
Nionavyo mimi kuhusu Mbowe na elimu yake.
1. Mwanzoni hakuona umuhimu wa kusoma zaidi ya Form 6, akafanya kazi BOT baadaye akawa mfanya biashara, tena mwenye mafanikio mazuri tu, reportedly, yote bila ya tertiary education, now nothing wrong with the path he chose, it worked for him, he should be proud of himself.

2. Sasa pamoja na mafanikio yake yote kibiashara na kisiasa, kitendo cha kurudi darasani (albeit kwa kuungaunga, again nothing wrong with that) huko UK at this point in time nadhani kinaashiria kuwa mwenyewe ametambua umuhimu wa elimu zaidi ya Form 6 aliyokuwa nayo, otherwise kwanini apoteze muda na pesa zake kuwekeza kwenye kitu ambacho hakina manufaa kwake, remember this man is supposed to be a savvy businessman from what I've gathered in here(his business ventures and accomplishments).

3. Hata mseme nini Mbowe knows his educational credentials (or lack thereof) could very well be a liability against him politically ndio maana anajitahidi kupandisha shule. All of you who are insinuating that he doesn't need to upgrade himself are not doing him any favors, if anything, and if you really support/admire(take your pick) the guy, you should support his quest for higher educational credentials.
 
hivi ile orodha ya wagombea wa ccm
ya urais 2005 ni msomi zaidi ya wote aliyechaguliwa?
mi nauliza tu?

Kafara mkuu acha spin,

Unajua fika hakuchaguliwa aliyeishia form 6 au mwenye diploma tu, for that matter.
 
Mkuu acha kubadili maneno, hakuna aliyesema kuwa asijiongezee elimu hayo ni maneno yako wewe, tunachosema ni kuwa hana kosa lolote katika sheria za taifa letu kuwa mwenyekiti wa Chadema au kugombea urais wetu akiwa na elimu ya form six,

Na tena tunasema hivi kuwa na elimu ya form six sio kuwa mpumbavu, na kwamba sio wote walimaliza form six bongo wanamiliki Casino kama yeye, sasa akiamua kuongeza elimu yake ni sawa, lakini hatum-condemn kwa kuwa na elimu aya form six na kuwa mwanasiasa mwenye mafanikio na mfanya biashara mwenye mafanikio makubwa, hatumlamu for that!
 
Hapa ndipo panapokuwa pagumu discussing anything with you, pray tell, where and how have I been inconsistent? Au bado kivuli chako kinakutoa jasho?

Na tena tunasema hivi kuwa na elimu ya form six sio kuwa mpumbavu, na kwamba sio wote walimaliza form six bongo wanamiliki Casino kama yeye, sasa akiamua kuongeza elimu yake ni sawa, lakini hatum-condemn kwa kuwa na elimu aya form six na kuwa mwanasiasa mwenye mafanikio na mfanya biashara mwenye mafanikio makubwa, hatumlamu for that!

Again, you're totally missing the point!

Huo mfano unaoung'ang'ania wa form 6 na Casino is skewed and misplaced at best, if anything with a background such as his alitakiwa awe na chain ya hotels and restaurants all over africa but then that would perhaps have required MBA type strategic planning. He's done good but he could've done better and he knows it.

Yeye mwenyewe, being the savvy businessman that he is(I know, I know I'm being overly generous here) ameona umuhimu wa kuongeza elimu at this point. Kifupi ni kwamba kaona anakoelekea anahitaji zaidi ya form 6, unless uniambie vinginevyo.
 
FMES,
Mtu anapochukia elimu huwa kwa kawaida anakuwa either naye hana elimu au anashaka na elimu yake au hajui kabisa umuhimu wa elimu. These are just facts, sikuzitunga.

Tena hizi facts zinatesa sana
 
Acheni kuzungusha maneno, shule ni muhimu tena sana. Huyo mheshimiwa mhimizeni amalize hiyo degree yake vinginevyo itakuwa ngumu kwake kisiasa tunapoenda huko mbele. Hatutampima kwa kufanikiwa kuendesha hizo biashara zinazotajwa hapa. Kama ni mafanikio kibiashara kwa nini tusimpe urais Mengi?

Mwenzake Mbatia tupo naye hapa Uholanzi na mambo yake yanakwenda vizuri. Naona huyu kijana Mbatia kwa kweli anajipanga vizuri kishule, tena hana papara kabisa.
 
Acheni kuzungusha maneno, shule ni muhimu tena sana. Huyo mheshimiwa mhimizeni amalize hiyo degree yake vinginevyo itakuwa ngumu kwake kisiasa tunapoenda huko mbele. Hatutampima kwa kufanikiwa kuendesha hizo biashara zinazotajwa hapa. Kama ni mafanikio kibiashara kwa nini tusimpe urais Mengi?

Mwenzake Mbatia tupo naye hapa Uholanzi na mambo yake yanakwenda vizuri. Naona huyu kijana Mbatia kwa kweli anajipanga vizuri kishule, tena hana papara kabisa
.

Binti Maria,
hongera sana kwa kuwatolea watu humu uvivu maana wengine wabishi kama....!!
 
Back
Top Bottom