Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Nimejaribu kuangalia mechi ya Simba na Namungo kule Ruangwa ambako nilikwenda kushuhudia live mtanange huo, nikaangalia Simba vs Mtibwa na jana Simba vs Tabora naona wachezaji wanaotumika ni wa kawaida mno lakini Simba inapata matokeo chini ya Mgunda, kwa mfano kule Namungo nilivyoona listi na wachezaji waliopo benchi nikasema mh Mgunda kapewa zigo la mavi, wachezaji hawa wamfunge Namungo, lakini mpira ulipigwa na bahati mbaya jamaa wakasawazisha mwishoni.
Gemu na Mtibwa nako hivyo hivyo wachezaji sio wale tuliokuwa tunawategemea kama akina Chama ambaye amefungiwa, Kapombe, Inonga, Micquisone, Onana, Babacar, Saido na hata Kibu lakini timu ikashinda, jana tena na Tabora ndio ilikuwa balaa kila nikiangalia wachezaji wa kikosi cha kwanza na kule benchi sipati picha, benchi wa maana ni Karabaka tu.Yaani Mzamiru jana alikuwa akicheza namba 10!
Kama Simba itaingia dimbani na wachezaji wale waliocheza vs Tabora nna uhakika Azam watatufanyia mauaji.