Kama mna dada wa kazi nyumbani kuna shida gani akifua na kupika chakula anachokula mume?

Kama mna dada wa kazi nyumbani kuna shida gani akifua na kupika chakula anachokula mume?

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wazee wa mahaba mpo?

Huwa sielewi ambavyo huwa kunakuwa na mjadala kuhusu dada wa kazi kufua nguo za baba mwenye nyumba au kupika chakula chake, yaani ishu ni nini?

Kama anafanya kazi nyingine ikiwemo kufua na kupikia wengine kama mna mtoto/watoto kwanini ni ishu zikifuliwa nguo za wenye nyumba na hasa baba au yeye kupika chakula cha familia ikiwemo baba? Kama mna mashine ya kufulia na kazi inazidi kuwa nyepesi, ni kuziweka kwa mashine na kwenda kuanika kama mashine inafua pekee.

Wanaweza kuamua kufuliana au kupikiana mara moja moja kwa mapenzi, lakini kwanini iwe lazima yaani?

Sasa wakwe na mawifi wakute dada wa kazi anafua nguo za ndugu yao au wajue chakula anachokula kinapikwa na dada wa kazi ni kisanga, why?

Na hapa nieleweke sizungumzii nguo za ndani, hizi wanatakiwa kujifulia au kufuliana kwa mapenzi yao.

Eti ishu huwa inakuwa wapi? Ni mpaka mke afue nguo za mume na kumpikia ndio anaonekana ana mpenzi sana?
 
Wazee wa mahaba mpo?

Huwa sielewi ambavyo huwa kunakuwa na mjadala kuhusu dada wa kazi kufua nguo za baba mwenye nyumba au kupika chakula chake, yaani ishu ni nini?

Kama anafanya kazi nyingine ikiwemo kufua na kupikia wengine kama mna mtoto/watoto kwanini ni ishu zikofuliwa nguo za wenye nyumba na hasa baba au yeye kupika chakula cha familia ikiwemo baba? Kama mna mashine ua kufulia na kazi inazidi kuwa nyepesi, ni kuziweka kwa mashine na kwenda kuanika kama mashine inafua pekee.

Wanaweza kuamua kufuliana au kupikiana mara moja moja kwa mapenzi, lakini kwanini ike lazima yaani?

Sasa wakwe na mawifi wakute dada wa kazi anafua nguo za ndugu yao au wajue chakula anachokula kinapikwa na dada wa kazi ni kisanga, why?

Na hapa nieleweke sizungumzii nguo za ndani, hizi wanatakiwa kujifulia au kufuliana kwa mapenzi yao.

Eti ishu huwa inakuwa wapi? Ni mpaka mke afue nguo za mume na kumpikia ndio anaonekana ana mpenzi sana?
Kufua chakula cha baba mwenye nyumba hapo kuna mjadala
 
Sijui ni umaskini lakini binafsi huwa sipendi kabisa toka moyoni mwangu kufuliwa, wala kutengewa chakula, au kuengewa maji ya kuoga, nina njaa hakujapikwa naingia kwa jiko napika.

Mtazamo wangu mke sio mtumwa wangu, kabla yake niliishije na baada ya ujio wake ni badalishe mfumo wa maisha.
 
Huwa sielewi ambavyo huwa kunakuwa na mjadala kuhusu dada wa kazi kufua nguo za baba mwenye nyumba au kupika chakula chake, yaani ishu ni nini?
Hivi unawajua vizuri hao Watu mpaka wafue nguo za mumeo, Wewe Dada yako au mdogo wako wa tumbo 1 unaweza mpa nguo za mumeo akufulie?
 
Sio kupika tu, amfulie, amuandalie maji ya kuoga, ampelekee maji bafuni, amtandikie kitanda na hata kumpa unyumba ni sawa tu kwani we si mfanyakazi. Ni mke na unatakiwa ufugaji na kubandika makucha na makope ya bandia na kuchat insta tu.

Mke sio kibarua, mke wajibu wake ni kupiga maselfie na kuchat tu instagram au sio?

Sijasoma ulichoandika ila ni mada za kipumbavu kabisa.
 
Sijui ni umaskini lakini binafsi huwa sipendi kabisa toka moyoni mwangu kufuliwa, wala kutengewa chakula, au kuengewa maji ya kuoga, nina njaa hakujapikwa naingia kwa jiko napika.

Mtazamo wangu mke sio mtumwa wangu, kabla yake niliishije na baada ya ujio wake ni badalishe mfumo wa maisha.
Watakuja kukusifu na reaction ya nzuri
 
Back
Top Bottom